Jana kama sikosei Mhe. Rais alisema kuwa ataunda Kikosi Kazi ya kupitia na kubaini kodi zote ziizo na kero kwa wananchi. Ninaiomba kikosi hiki kisisite kupitia kodi zote za HALMASHAURI zilizo kero kwa wananchi kama zifuatazo:- (1) Kodi ya Hotel Levy (2) Kodi ya Zima Moto (3) Kodi ya Mabango nk. Wananchi wanaonewa sana huku kwenye Halmashauri kutokana na kodi hizo nilizozitaja na nyinginezo nyingi. Wakati wa Mhe. Mkapa kodi kama hizo hazikuwepo na wananchi waliishi kwa amani. Kodi hizi zimeanza kwenye awamu ya nne. Tusaidie Mhe. Rais.