Kikatiba uchaguzi wa marudio Zanzibar haupo

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,812
48,990
Katiba ya Zanzibar 1984/2010.

Ibara ya 90(1). Wakati baraza litakapovunjwa, Uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi utafanywa, na mkutano wa mwanzo wa baraza jipya utafanywa si zaidi ya siku tisini toka kuvunjwa kwa baraza.


Leo ni zaidi ya siku 120 toka baraza livunjwe, hadi leo hakuna mkutano wowote wa mwanzo ulioitishwa na haijulikani utaitishwa lini.

Ndiyo maana nasema kikatiba uchaguzi wa marudio hautakuwepo, kitakachotokea ni ZEC kuwatangaza washindi wawakilishi walioshinda kwenye uchaguzi uliopita.
 
Katiba ni kitu gani kwa mafisiem?

Wao wanafanya wanachotaka...muulize Jecha akutajie kifungu cha sheria alichotumia kuufuta huo uchaguzi..

hawa jamaa, wanaishi kwa ubabe tu hakuna lingine
 
Sasa kama Seif hamtambui Shein kama Rais wa zanzibar kwanini yeye anajitambulisha kama makamu wa Rais
 
Wewe nahao wajinga wenzio ccm uchwala sibilini chunvi ikolezewe mchuzi hakahuu znz hamtoki nilazima muutii ushindi harali wawanchi znz
 
Katiba ni kitu gani kwa mafisiem?

Wao wanafanya wanachotaka...muulize Jecha akutajie kifungu cha sheria alichotumia kuufuta huo uchaguzi..

hawa jamaa, wanaishi kwa ubabe tu hakuna lingine
Kweli kabisa mkuu ulichosema, kwa CCM wao wanaiona Katiba sawasawa na Dailynewspaper!
Kwao wao ni ubabe na utemi na kuivunja Katiba ya nchi wao wanaona ni jambo la kawaida sana kwao.
Wao pia wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu amewapa wao hati miliki ya kuitawala nchi hii hadi mwisho wa dunia.
 
Sasa kama Seif hamtambui Shein kama Rais wa zanzibar kwanini yeye anajitambulisha kama makamu wa Rais

Tina Turner alilipata jina lake kutoka kwa mume wake Ike Turner. Baada ya mfarakano na mateso ya muda mrefu kutoka kwa mume wake, Tina alifanikiwa kupata talaka mahakamani. Katika settlement mahakamani, Tina alikubali kumuwachia mume wake mali zote walizochuma pamoja na hasa kwa nguvu zake Tina, isipokuwa kitu kimoja tu, nacho ni jina, Turner, ambalo ni jina la aliyekuwa mumewe. Jaji akamruhusu.

Maudhui ya simulizi hii ni kuwa, serikali ya umoja wa kitaifa imejengwa kutokana na makubaliano baina ya Rais Karume na Maalim Seif. Dr Shein hakuhusika juu ya hili. Makubaliano haya yalipelekea kurekebishwa katiba ya Zanzibar na kuwepo Makamu wawili wa rais. Nukta ninayojaribu kuiwakilisha hapa ni ukweli wa.kwamba Seif kaufanyia kazi Umakamo wa rais, kwanza kwa kufikia muafaka na Karume, pili kwa kukubali matokeo ya 2010 ambapo kuna kila ushahidi kwamba alishinda uchaguzi ule, na kuepusha maafa.

Hitimisho ni kwamba you can take everything from Maalim Seif, but he has earned the title Makamu wa Kwanza wa Rais. Anayo haki ya kuitumia hiyo kwa vile that's the only thing CCM cannot take away from him. Like it or not!
 
Back
Top Bottom