Kikao cha NEC CCM Arusha chaahirishwa tena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikao cha NEC CCM Arusha chaahirishwa tena!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jan 10, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  KIKAO cha Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM mkoani Arusha, kilichokuwa kimepangwa kufanyika kesho, kimeahirishwa tena hadi Januari 14 katika kile kilichoelezwa kuwa ni kutokamilika kwa maandalizi.

  Kikao hicho, kinasubiriwa kwa hamu na wanachama wengi wa CCM mkoani humo kwa sababu inasemekana kuwa kitapenyezwa ajenda ya kumng'oa madarakani Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda.

  Hii ni mara ya pili kwa chama hicho kinachotawala kuahirisha kikao hicho ambacho awali kilipangwa kufanyika Desemba 29 mwaka jana, lakini Katibu wa Uenezi wa Itikadi wa CCM wa Mkoa, Loota Sanare alisema kimeahirishwa hadi kesho.Habari za uhakika kutoka miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya mkoa, zilisema kuahirishwa kwa kikao hicho, kunatokana na kutokamilika kwa maandalizi.

  Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka juzi, hali ndani ya CCM mkoani humo, imekuwea si shwari hasa kutokana na siasa za makund.

  Katika siku za karibuni mgogoro huo, ulivuka mipaka na kuwakumba Katibu na Mwenyekiti wake, Onesmo Nangole baada ya kutokana na kutofautiana katika matumizi ya mali za chama, mikataba na endeshaji wa shughuli mbali mbali.

  Kabla ya Kuibuka kwa mgogoro huo, Arusha kulikuwa na mgogoro baina ya katibu huyo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya CCM wa Mkoa wa Arusha, James Ole Millya na wenzake.

  ::Mwananchi
   
 2. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mary chitanda ------------- James Ole Millya ------------- Onesmo Nangole === Kuzikwa kwa ccm arusha
   
 3. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wazid tu kuahirisha,for real nawahate sana hawa magamba
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kumg'oa Mary Chitanda siyo rahisi kama wanavyofikiri.
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Wanataka kungoa chakula ya wazee?
   
Loading...