MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 496
- 768
Tarehe 11 April, jijini Dar Es Salaam huko Tanzania, kilifanyika kikao cha dharula kinachohusu hatma ya jeshi la SADC, Mission (failed) ya SAMIDRC.
Kikao hicho kiliwahusisha:
-General Rudzani Maphwanya (SA National Defence Force),
-General Jacob Mkunda (Tanzania People’s Defence Force- TPDF) na
-General Paul Phiri (Malawi Defence Force). Kikako hicho kilichofanyika makao makuu ya jeshi la kulinda amani la Tanzania(TPDF) pia kilihudhuliwa na Professor Kula Theletsane, mkurugenzi wa SADC wa Siasa, Ulinzi na usalama.
Ni Baada ya kutuhumiwa na M23 kushiliki jaribio la kuukaba tena mji wa Goma kutoka mikononi mwa M23.
Ikumbukwe, huko nyuma walikuwa wamesaini makubaliano ya kuwezesha SADC kuondoa majeshi yake, lakini uongozi wa DRC, ulisema, SADC na SAMIDRC vitaondoka mashariki mwa Congo, ikiwa M23 imeshapokonywa maeneo yote yaliyo chini ya uangalizi wake.
Makubaliano hayo, yalikuwa yanaiwezesha SADC kutumia uwanja wa ndege wa Goma, na kuondoka na silaha zake, lakini kwa hali hii, M23 ilitangaza kusitisha na kujiondoa katika makubaliano hayo, na kuitaka SADC iondoke mara moja.
Kikao cha wakuu hao, kiliamua kuondoa wanajeshi wa SAMIDRC, kupitia njia ya ardhi, ambayo ni RWANDA, wakikusanyika huko Chato, mkoani Geita kwa maandalizi mengine.
Hata hivyo, zoezi kubwa lililobaki ni uwezekano wa majeshi hayo kuondoka na vifaa vyao na silaha. Ikisemekana hivyo hivyo ndo vilitumika kuishambulia M23, uwezekano wa kuviachia ni mdogo, na serikali ya Rwanda, kukubali kupitishwa kwa silaha hizo nchini, huku ikisemekana January zilikuwa zitumike kuishambulia, pia ni mdogo sana.
Kutokana na kuwa wanajeshi wa SAMIDRC waliokuwa wakitumia silaha hizo, kwa sasa wapo chini ya uangalizi wa M23, ina maana hizo silaha mpaka sasa ni mali halali ya M23. Lakini pia, kwa inavyosemekana, ni aibu kubwa kwa taifa la South Africa, ambalo lilikuwa tayari kufanya kila linaloweza kuhakikisha linaifukuza M23 na kurudi na vifaa vyao.
M23, pia inaituhumu MONUSCO kuwa kikwazo cha amani na usalama ukanda huo, baada ya kuachia wanajeshi wapatao 800 na siraha zao kisiri siri.
Mwezi January, MONUSCO iliitangazia M23 kuwa na wanajeshi wapatao 2000(Elfu mbili); wakiwemo Wazalendo, FDRL na wanajeshi wa serikali.
Lakini kwa sasa, MONUSCO imeitangazia M23 kuwa, wapo tu watu 1200(Elfu moja na mia mbili). Hivyo, kuisababishia pia MONUSCO ugumu wa kutembea huru.
Kambi za MONUSCO na SAMIDRC kwa sasa zipo chini ya uliinzi mkali wa M23, na kuongeza kuwa uhuru wa kutembea kwa sasa haupo tena, huku ulinzi ukikazwa mjini, na msako mkali mjini Goma ukiendelea.
Hali hii pia, ilitokea Kivu kusini, ambapo jeshi la Burundi ndo linasaidizana na Wazalendo na FARDC kukabiliana na M23. Uwanja wa ndege wa Kavumu uliokuwa ukitafutwa na upande wa serikali, baada ya mapigano, ulirudi mikononi mwa M23.