Kijue kisiwa cha Mnemba, kilichopo Zanzibar, kinachodaiwa kumilikiwa na Bill Gate

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,836
Watanzania wengi hawajawahi kusikia kuhusu hiki kisiwa kilicho maarufu kwa wapenda bata wa kimataifa.

Mnemba Island ni kisiwa kidogo kinachojitegemea , kilichopo kaskazini masharaki yapata umbali wa kilometa 3 kutoka Unguja. Mkabala na ufukwe wa Muyuni (Muyuni Beach).

Kisiwa hiki chenye umbo linalofanana na pembe tatu kina kipenyo cha 500 metres (1,640 ft) na mzingo wa 1.5 kilometres (0.9 mi) .

Kisiwa hiki cha maraha inasemekana kinamilikiwa na Bill Gates na ili uende huko yakupasa ulipie kabla huduma za malazi na chakula kwa siku saba, ambapo gharama za kitanda peke yake ni kati ya US$1155 hadi US$1600 kwa mtu mmoja kwa siku.

Ukifika kwenye kisiwa hiki utaweza kuwaona kwa jirani kabisa pombe (dolphins) wakiruka kwa furaha.

Pia utaweza kufanya scuba diving.

Wanaoruhusiwa kuingia kisiwani hapa ni wageni wale tu waliolipia na kuorodheshwa hotelier.
 
images.jpeg-19.jpg
 
Back
Top Bottom