SoC03 Kijiji kilichoumbwa usiku

Stories of Change - 2023 Competition

allan_gobe_tz

New Member
May 31, 2023
3
3
Hapo mwanzo kipindi bado nakaa kijijini nilitamani sana siku nikimaliza elimu yangu ya sekondary basi nikasomee elimu ya juu katika jiji la Dar es Salaam kwani mama yangu Rebeka Kilomba, alinisisitiza nisome Sana na kwa bidii. Kweli sikukata tamaa katka masomo yangu ya sekondary.

Mungu si athumani nlimaliza Salama na Kwa ufaulu mzuri mpaka kujiunga elimu ya chuo kikuu Cha Usafirishaji(NIT). Baada ya kufika katika jiji la Dar es salaam nlitamahaki Sana Kwani ndiyo siku ya kwanza kuliona jiji lenye mvuto wa pekee nchini na lenye kuchangamka kama nchi za ughaibuni, sikuwa na sehemu ya kufikia kwani sikuwa na ndugu Bali Jamaa na rafki wa karbu ndugu Regan anuar baada ya kunpokea na kunhifadhi Kwa mda Ili nweze kufanya maandalizi ya chuoni.

Siku hazikuwa na foleni ya kusubiri utayari wako Bali zilisonga mpaka kuelekea kureport chuoni tayari Kwa usajili Kwa wanafunzi wote waliochaguliwa, Mwenyewe pia skuwa mbali na Hilo kwaani nlitamani Sana kusoma na kuelimika nimalizie npate ajira nisaidie ndugu zangu na mama yangu huko kijijini Nyarukongogo. Baada ya taratibu zote sikuweza kufanikisha kumaliza kwaani sikuwa na Pesa ya malipo ya ada kutokana na familiya yangu masikini Bado sikuweza kukata tamaa ya maisha ya elimu kwani nlijua elimu ndiyo msingi mkubwa wa maisha ya umasikini.

Siku moja nliomba Sana mwenyezi Mungu anijalie Kwa hili nweze kufanikiwa kwani nmepitia mengi mpaka nafika hapa bila ya kupoteza mda nlimfata Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ndgu. Eli James Kwa sababu ya msaada wa kimasomo baada ya kumuelezea matatizo yote kweli Kiongozi huyo alinskiliza Kwa umakini bila ya kujali tabaka Wala kabila langu na aliweza kunsaidia kiasi Cha shilling 200,000/= Kwa maana ya kunsaidia kulipa ada Nlimwona Kiongozi Bora mwenye kujali na kusaidia wananchi wenye matatizo Kwa moyo wake nlitamani katika nchi yote viongozi wote wangekuwa kama Mh. Eli Jemes Kwani alinpa moyo Sana wa kupambana zaidi.

Baada ya kufanikisha yote nkamshukuru Mungu lakini Bado changamoto hazikuweza kuisha kwani Ukosefu wa hostel za chuoni hazikuweza kuwatosha wanafunze wote ikalazimika wengine kupanga mitaani kama wananchi wa kawaida wenye familia zao ikiwepo na Mimi katika msafara huo sikuchoka kwani tayari nliweza kuwa na utayari kikubwa nmalize yaliyonleta katika jiji lenye udongo mweusi, siku zikapita kero za mtaani hazikuisha kwani mwanafunzi naye alitakiwa atoe michango kama mwananchi wa kawaida wakati huo huna kipato Wala ajira nkajiuliza nkwanamna gani viongozi wanawajibika Kwa raia wao?

Kwani haikuwa haki Mwanafunzi anaetegemea malipo ya chakula na maladhi sh. 500,000/= ajikimu mwenyewe pamoja na hiyo michango ya serikalini sikuwa na namna ilibidi nwajibike katika uchangiaji kwani Tanzania ni moja na wote lengo letu moja la kuijenga nchi yetu Kwa pamoja.

Maisha yangu yalikuwa ya simanzi na majonzi makubwa kwani nlitamani kuacha masomo Kwa sababu ya Hali ya kiuchumi, Basi likabaki ni jukumu letu sote wanafunzi kusimama kipaumbele katika kuhimiza na kupinga mifumo potofu ambayo ipo kinyume na matakwa ya wananchi, aidha Serikali iondoshe kero za mtaani Kwa mwanafunzi wa elimu za vyuo na vyuo vikuu kwani huwezi kusababisha athari kama za kujiuza Kwa mabinti, mpenzi ya jinsia moja(Ushoga) Kwa wanaume Ili tu mwanafunzi ajipatie kipato pamoja na pesa ya kutoa michango ya serkali kama pesa ya taka pamoja na ulinzi mtaani.

Nliishi Kwa mapambano makubwa Sana katika kujituma huku na kule mpaka nahitimu shahada ya awali kwani mama Angu alitamani Sana hatima yangu aione kabla hajapoteza uhai wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom