Imetokea bahrain kijana ampiga mama yake mzazi kisa mkewe kakosana na mama yake na kuja kumwambia mumewe mama yako kantukana na kila siku anansimanga ndipo kijana akaingia hasira na kuanza kumpiga mama yake mzazi
Ndo mama huyo alivochakazwa hapo mkewe anajisikia burudan yaan anaona anapendwa hadi jamaa kumpiga mama yake hajui kama ni laana na huenda akaanza kuokota makopo mda si mrefu na asimkimbie akianza ukichaa
Thubutuuuuuu ninavyompenda mama yangu hivi naanzaje???? Hata kama ni hasira kiasi gani, kamwe kamwe siwezi hata kumkasirikia mama yangu Kisa papuchi, go to hell na papuchi yako. Nitampata atakayemheshimu mama yangu
Ni kweli kuna kina mama wengine wana gubu hatari ila kijana kumpiga mama yake ni laana kuu....bila kujali amekosa nini kumpiga mama ni zaidi ya kosa la jinai
Mama mkwe hapatanagi na mke wa mwanae, dawa ni kuwatenganisha kila mtu akae kwake, inasikitisha wewe na mkeo mnajinyima kuwatunza watoto mnajenga nyumba nzuri, baba anakufa watoto wanakula bata na wake zao ndani ya hiyo nyumba mama yao wanamfukuza anaenda kuomba hifathi kwenye pagala la mtu,maana hata hela ya kupanga chumba hana. kisa haelewani na mkamwana