kijana atoa mpya ya mwaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kijana atoa mpya ya mwaka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 17, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  KIJANA aliyetambulika kwa jina la Kizito Mwashala (29), mkazi wa Mbagala Kilungulile, ametoa mpya ya mwaka kwa kuchimba makaburi ili amzike baba yake ambaye yu hai kwa kile kilichodaiwa kumchelewesha kurithi mali zake.
  Katika hali ambayo haikuweza kuaminiwa na walio wengi, kijana huyo aliamua kuchimba makaburi matano ndani ya nyumba yao ili aweze kumzika baba yake kwa siri aliyetambulika kwa jina la John Mwashala(87).

  Ilidaiwa kuwa wakati kijana huyo alipokuwa akiandaa makaburi hayo alionekana na baadhi ya majirani na walimuibia siri hiyo baba yake ndipo ripoti ikatolewa ofisi za serikali za mtaa.

  Baada ya kuona siri hiyo imetolewa alianza kumpiga baba yake huyo kwa vitu mbalimbali kwa lengo la kummaliza na majirani walikusanyika kumkamata na kumfunga kamba kisha kutoa taarifa kituo kidogo cha polisi cha maturubai.

  Ilidaiwa kuwa kijana huyo alikuwa akimpa mateso baba yake huyo kwa kumnyima chakula huku akivuta bangi akiwa ndani humo na kumpulizia moshi wa bangi na ndugu zake walikuwa wakihofia kufika hapo kutokana na ubabe wa kijana huyo, ukatili, utukutu na hata kuwatishia kuwaua.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema kuwa atafikishwa mahakamani siku yoyote.
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  eeeh:smash:
   
 3. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180

  Bado sijapata point ya mtuhumiwa kuchimba makaburi ma5 tena ndani ya nyumba? hiyo nyumba ilikuwa kubwa kiasi gani? na je hapakuwa na watu katika nyumba hiyo? Kwakweli tabia ya wavuta bangi inabidi serikali iwaandalie gereza lao
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  bange au ganja ni hatari unakua na nguvu kuliko kawaida
   
Loading...