elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,261
- 9,732
Mouawiya Syasneh alikuwa na umri wa miaka 14, mwaka 2011 akiwa anaishi katika mji wa Deraa, Syria.
Mouawiya Syasneh alianza kwa kuandika ujumbe wa kuiponda na kuikosoa serikali kwenye kuta za shule aliyokuwa akisoma kwa kutumia rangi za ku spray.
Hakujua kuwa kitendo kile kingezua maandamano ambayo yangepelekea vita kubwa ambayo ingeendelea kwa miaka mingi.
Leo ni zaidi ya miaka sita, vita imekuwa kubwa na isiyo kwisha huku yeye Mouawiya Syasneh akiwa mstari wa mbele akipigana upande wa waasi.
Watu zaidi ya nusu milioni wamekufa akiwemo baba yake, ndugu marafiki na jamaa.
Mouawiya Syasneh anasema laiti angejua kuwa matendo yake yangeleta maafa haya, wala asingethubutu kuandika ujumbe ule uliobadili historia ya nchi yake.
Usikose kutazama documentary ya the boy who started the syrian war kupitia aljazeera.