KB THE DON
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 250
- 117
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Miaka tofauti tofauti yamekuwa yakitolewa maandiko mbali kuhusu lugha inayotakiwa itumike kwa ajili ya ufundishaji.
Ambapo wengi wamekuwa wakishauri ama kitumike Kiswahili kuanzia Elimu ya awali/msing hadi vyuo vikuu wengine wamekuwa wanapendekeza tuendelee na mtaala wa sasa wa elimu msingi kwa Kiswahili na secondary na vyuo kitumike Kiingereza.
Changamoto za mtaala huu wa elimu msingi kwa kiswahili na secondary na vyuo kitumike kingereza ni nyingi hususani mojawapo kati ya hizo ni kwamba tunampotezea mtoto miaka 7 ya kusoma kwa Kiswahili then anaenda sekondari anaanza upya nikiwa na maana kwamba kama hakuna uwiano ama mwendelezo flani wenye ufanano kielimu ikizingatiwa kwamba lugha ndiyo msingi pekee katika kujifunza.
Binafsi yangu ninaona ni serikali yetu kuamua jambo moja ama kuwa moto au kuwa baridi nikimaanisha kwamba haijalishi ni kwa muda gani mfumo wa elimu uliopo umetumika kwa muda mwingi kiasi gan pia haijalishi ni manufaa mengi kiasi gani tumeapata kwani ingekuwa tunao mfumo bora zaidi ya huo huenda tungekuwa tumefaidika zaidi na zaidi ila ni bora kufanya marekebisho haya yafuatayo:
1. Ama Elimu ya Tanzania ifundishwe kwa lugha ya kiswahili kuanzia msingi had vyuo
2. Ama Elimu ya Tanzania ifundishwe kwa ENGLISH medium kuanzia msingi hadi vyuo
Kuliko kutumia mfumo huu uliopo mm nimefanya study ndogo sana hasa kwa wanafunzi ambao wamesoma elimu inayofuata mfumo mmoja wa lugha hususani ENGLISH MEDIUM nimeona wanakuwa na mwendelezo mzuri kitaaluma kwakuwa vile alivyovisoma msingi kwa english atakutananavyo sekondari kama mwendelezo wake zaidi ya yote ugumu wa shule kwa watoto wetu umeongezeka kutokana na mzigo wa kutoifahamu lugha inayotumiwa.
NAOMBA KUWASILISHA. Ni mtazamo wangu tu jamani.
Karibu kwa maoni