Kihongosi: Wanaohoji kwanini nazunguka mikoani 'ni wajibu wangu'

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amesema kuwa kuna watu wanaohoji sababu za yeye kutembelea mikoa mbalimbali nchini, akasisitiza kuwa jukumu hilo lipo wazi kikatiba.

Akihutubia wananchi wa Ikungi, Kata ya Puma, Mkoani Singida leo Januari 22, 2026, amesisitiza kuwa chama kina wajibu wa kuhakikisha serikali inatekeleza kikamilifu ahadi ilizotoa kwa wananchi.

“Najua wapo baadhi ya watu watasema, ‘kwanini Mwenezi anazunguka-zunguka? Mwenezi anafanya nini mikoani?’ Jibu ni moja tu—waambieni Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi kwa mujibu wa Katiba ya CCM ana uwezo wa kwenda popote nchini kuangalia uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Sisi ndiyo tulioiweka serikali madarakani, hivyo tuna wajibu wa kwenda kuisimamia serikali yetu ,” amesema.
Your browser is not able to display this video.
 
Hiki chama kimechokwa kwasasa kinafosi tu kukubalika kwa wananchi, imagine kampeni za uchafuzi mkuu walifanya wao peke yao (achana na akina chauma) lakini bado wananchi wakaungana na chadema kuususia!.
 
Kelele nyiingi...matumizi makuuubwa ya fedha za umma afu mnakuja kuiba kura!

Hamna jipya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…