Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema ushindi wa chama hicho katika chaguzi unatokana na kuwa na mfumo imara na mtandao mpana wa wanachama kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Maswa mkoani Simiyu Machi 7, 2026, Kihongosi amesema Katiba ya CCM inaitaka chama hicho kushinda chaguzi zote, huku akieleza kuwa uimara wa muundo wake ndio msingi wa mafanikio hayo.
Amesema katika ziara yake ametembelea shina lenye wanachama zaidi ya 150 na kubainisha kuwa mkoa wa Simiyu una mashina zaidi ya elfu mbili hadi tatu, hali inayodhihirisha idadi kubwa ya wanachama waliopo ngazi ya chini.
“Mikoani tuna watu, wilaya tuna watu, kwenye kata tuna watu, kwenye matawi tuna watu, kwenye mashina tuna watu na mabalozi tunao. Huwezi kutufananisha na wengine,” amesema.
Kihongosi amedai kuwa vyama vingine vya upinzani havina mfumo mpana wala uongozi thabiti kama CCM, akitaja baadhi ya vyama kuwa vinaendeshwa zaidi kwa ushawishi wa mtu mmoja mmoja badala ya taasisi imara.
Amesisitiza kuwa tofauti na vyama hivyo, CCM inaendeshwa kama taasisi yenye mizizi imara inayotegemea wanachama wake kuanzia ngazi ya chini kabisa.