Kigwangalla Unangoja Nini Huko CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigwangalla Unangoja Nini Huko CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zulqarnayn, Feb 3, 2012.

 1. Z

  Zulqarnayn Senior Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zilizotufikia hivi punde na ambazo tumezithibitisha zinasema kwamba Mbunge wa Nzega yuko katika hali mbaya ndani ya chama chake. Kwenye Kikao cha Kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) hapo jana jioni ambacho pamoja na mambo mengine kilijadili sakata la mgomo wa madaktari, hakikusita kujadili suala la nidhamu ndani ya chama hususan miongoni mwa baadhi ya wabunge. Hapo mjadala kuhusiana na ushiriki wa Mbunge huyu kijana, msomi na mwanaharakati ambaye amekuwa akifanya mambo yanayosemekana kushabihiana na harakati za vyama vya upinzani kwa misimamo yake na michango mikali ndani na nje ya bunge. Kijana huyu alijikuta kwenye wakati mgumu pale hoja ya kumtaka ashughulikiwe, kama ile ya kikao cha namna hiyo cha jumapili iliyopita, ilirudi tena.

  Safari hii alipewa nafasi ya kujitetea na ndipo alivyoanza kupangua tu hoja za wabunge wenzake moja baada ya nyingine lakini kabla hajafika popote alikatizwa na mwenyekiti wa kikao hicho na kumtaka ake kwanza asomewe maelezo ya taarifa ya usalama aliyokuwa nayo Mhe. Pinda, baada ya hapo Mbunge wa Sikonge kwa kuangalia hali ilivyokuwa imechafuka mule ndani kufuatia baadhi ya wabunge wa CCM kusikitika, aliokoa jahazi na kmuomba waziri mkuu asitishe zoezi la kumtaka Kigwangalla kujieleza, na badala yake asaidiwe, alisema: 'mwenyekiti mimi ni mwenyekiti wa wabunge wa Tabora, naomba nikuombe sana umsaidie mdogo wangu Kigwangalla, ni kijana mzuri lakini sema ana spidi kali sana, anahitaji busara zenu, akina Mkuchika, Wassira, naomba mumsaidie mdogo wangu huyu jamani...hapa naona kama mnazidi kumbomoa tu hamumsaidii, mimi ningekuwa yeye kwanza nisingeongea humu hata kwa miezi sita hivi....' Waziri Mkuu alisitisha mchakato huu na Kigwangalla, ambaye alikuwa ameanza kwa kuomba radhi watu wote aliowakwaza kwa namna yoyote ile, na kusema anaomba aweke rekodi straight ili tatizo lionekane kwa uhalisia wake na siyo kumuangalia yeye kama msaliti ama 'Rebel' kwa chama........alionekana kutoridhika na uamuzi huu na hivyo alitulia na kusononeka.

  Kikao hicho kilikuwa kikali sana na kilijadili mambo mengi sana mazito likiwemo la posho na jinsi serikali inavyojichanganya. Wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema, sasa ni kwa nini anaendelea kubaki kwenye CCM wakati ananyanyasika kiasi hicho bila hata huruma, bila hata kupewa nafasi ya kujieleza kwa kina? CCM sasa inaonesha kuchoka na pengine kuanza safari ya kuelekea kuanguka, maana kama inawapiga vita vijana makini, wasomi na machachari kama Kigwangalla, inataka kutueleza nini kuhusu wapambanaji wake katika siku za usoni? Inabidi wawe ni watu wa ndiyo tu? Ili hiki chama kishamiri na kiendelee kushika hatamu za uongozi wa nchi, inabidi kijirekebishe, kiwakumbatie watu walioonesha vipaji vya uongozi wa kisiasa na wenye mvuto kwa umma kama akina Khamis Kigwangala!
   
 2. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tatizo hata yeye sio msafi msimuone hivyo anamachafu kibao kwanza kwani hajipendi amuulize Generali ulimwengu
   
 3. L

  Le Grand Alexei Senior Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi sioni kosa la Kigwangala hata kidogo, hivi kwani ni lazima atete serikali? Yeye si Mbunge wa wananchi sasa akitetea madaktari si maana yake analenga kuwatetea wananchi? Nadhani chama hiki kinaanza kukiuka maadili na kinataka kuvunja kati ya JMT inayotoa uhuru wa kuchanganyikana na wengine, uhuru wa kila mtu kuongea n.k. kwa kumsulubu Kigwangala kwa kuoa mawazo yake, na kwa kwenda kwenye mkutano wa MAT, chama ambacho watu wenye taaluma ya udaktari huwa wanakusanyika. Hlf kwa nini serikali inajadili watu badala ya kuliangalia tatizo lenyewe? Ama sasa tuanze kujadili watu walioufikisha mgomo huu wa madaktari huko...maanayake kama wangefanya kazi yao ipasavyo madk wasingegoma!
   
 4. L

  Le Grand Alexei Senior Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wewe una chuki binafsi, tumwagie machafu yake hapa hadharani siyo kumtuhumu mtu tu? Sisi tunamkubali walau yeye siyo kama wabunge wengine wa Magamba wanaodai posho bila kuwafikiria wengine, lakini HK ameonesha ana dhamira ya dhati ya kuwa mtumishi wa watu toka aingie bungeni, kuanzia kwenye kuwatetea wananchi wake, wale wachimbaji wadogo wadgo kule jimboni kwa dhati na kwa nguvu zake zote mpaka alishalala ndani kwa ajili ya wananchi wake!
   
 5. M

  Mbogo Junior Senior Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watu wa msimamo kama yeye wanapashwa kujindoa na kujiunga kwa vyama vyenye uchungu na nchi.
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hamis should stay in CCM!!!!
   
 7. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Nimewahi kushiriki kikao cha baraza la vijana wa CCm wilaya ya Same mwaka 2009. Mgeni Rasmi alikuwa ni David Mathayo. tulivyoenda kula kule Motel elephant. Kuna mtu mmoja nafikiri alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya mojawapo ya mkoa wa Kilimanjaro alimwambia live bwana mathayo kuwa nyie mawaziri na wabunge mmeshajijengea pepo hivyo lolote linalowahusu wabongo hamna time nalo! kwani watoto wenu hakuna anayesoma Saint Kata,Katizo la Umeme haliwahusu kwani mna majenereta automatic hivyo hamjui kwamba umeme umekatika ama lah! watu wanaowatetea wabongo nyie ni maadui zenu kwa 100%. Sijui mnamatumaini gani? sasa kwa hili ambalo sijui mwenyekiti wa Wabunge wa Tabora anasema H.K asaidiwe simwelewi yeye ndo anastahili maombezi kabisa . That MP chairman need more help than HK. May god bless HK na pia amwongoze kutoka huko Magambaz at least hata ajiunga na Mtikila sio mbaya sana kwani akijiunga na CDM tu basi atawekewa vikwazo kibao.
   
Loading...