Kigoma sio ndondocha

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Kila mtu atawashangaa watu wa Kigoma akisikia kuwa watu wa Kigoma wamejiunga kwa wingi na chama kipya cha siasa cha ACT. Ingawa kila mtu anayo haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa katika mfumo wa vyama vingi lakini haki hiyo lazime iwe na uhalisia ndani yake. Zitto alipata umaarufu kupitia chadema chama ambacho sasa kimekuwa hadi kufikia kuwa chama kikuu cha upinzani nchini ambacho kinaogopwa sana na chama cha CCM pamoja na watu wengine ambao wanadhani kuwa kama CCM kitashindwa na maslahi yao nayo yatakuwa yako hatarini.

Chadema pamoja na Zitto ndani ya chadema na mikakati yao walikuwa wanakaribia sana kulishika makalio dume la nyati. Juhudi hizi za kulipapasa dume makalio zinadhoofishwa na akina Zitto na washirika wake kwa kuanzisha tuhuma nzito kwamba chama ambacho alijiunga nacho akiwa na umri wa miaka 16 tu eti hakina demokrasia. Hii sio kweli hizo ni juhudi mahususi za kulikwepesha dume na aibu ya kushikwa makalio yake kirahisi japo kwa kuondoa angalau hata kura 100 tu kutoka kwa wapinzani.

Wananchi wa Kigoma kujiunga na chama kinda cha ACT kwa kumfuata Zitto watakuwa wanaingia kwenye historia ya watanzania waliopinga na kuchelewesha kuondoa dhuluma nchini sawa na akina Zuberi Mtemviu enzi za TANU na Nyerere. Zitto anatumia ukabila (U-Kigoma) na uelewa mdogo wa wananchi katika kufanya biashara ya kuchelewesha kuing'oa CCM madarakani.

Hakuna mtu mwenye akili lazini ambaye ataamini kuwa Zitto amefanya yale aliyoyafanya ya kudai uongozi ndani ya chadema kwa njia za pembeni na kukipeleka chama mahakamani kwasababu ndani ya chadema hakukuwa na demokrasia ya kutosha, hii sio bahati mbaya tu, bali kuna jambo.

Kigoma kuweni macho na wanasiasa hawa wanaowarudisha nyuma juhudi zenu za kutafuta nafuu za kisiasa kwa kuanzisha vyama vipya vitakavyowachelewesha kuwafikisha nchi ya ahadi. Kataeni kuwa ma-ndondocha. Binafsi ninawasikitikia wananchi watakaonaswa na mtego wa kitoto kama huu kwa kujiunga na ACT.
 

bavicha poleni sana naona mnameza dawa taratibu lakini sioni mkipata nafuu
 
bavicha poleni sana naona mnameza dawa taratibu lakini sioni mkipata nafuu

Duh!! naona umekuwa mshabiki tena wa Zitto wakati wa suala la ESCROW ulikuwa unatoa maneno ya kumdhihaki na kumtukana leo hii yupo ACT unajifanya mshabiku wake na mpo wengi kweli dizaini hiyo kimwili na kiroho mpo CCM eti kinadharia mnajufanya kuishabikia ACT na Zitto nyie ni MAJUHA.
 

uniombe radhi na suluhu
 
Inaonesha ni rahisi sana kuwafinyangafinyanga wana kigoma ukiwa umepata elimu kidogo. Yaani wapo km bendera
 
Wanakigoma ni wakabila sana na wanasiasa za ukabila ,hawafuati sera wanafuata mtu alikuwepo Dr Kaboul naye walimoenda akawatema ,sasa huyu ndumilakuili Mungu atusaidie amtoe kwenye siasa hili tupate ukombozi tulio wanyonge.
 
Ma CCM wakati wa ESCROW yalimtukana ZZK kila aina la tusi. Leo yanamsifia kisa Kaenda Act.
 
wakati zzk anakipeleka chama mahakamani mlisema atoke na aanzishe cha kwake sasa kaanzisha mnaanza kuwashwa makalio, kwa akili zenu mlitegemea zzk aungwe mkono na wachaga? mna akili ndogo sana ni lazma aungwe mkono na watu wa kwao hata chadema ndivyo ilivyo kwahiyo ondoeni matapishi yenu hapa.Na bado itawauma sana.
 
ujumbe wako wana kigoma wameusikia lakini kuingia chama kingine kwa kutumia utashi wako huo sio undondocha kukaa kwenye chama bila kutumia utashi wako huo ndo undondocha by the way una define vipi undondocha????
 

Ukishakuwa ACT so what? chama chenye mbunge mmoja bungeni? chama cha wasiopenda kufuata taratibu za chama? Sisi sote tunajuwa umuhimu wa chama kuwa na wabunge wengi bungeni katika kupitisha ajenda zake, hivi ACT itawachukuwa miaka mingapi ili ipate wabunge japo 5 bungeni? Zitto ni mhaini wa nguvu na rasilimali za wananchi walizowekeza ndani ya chadema. Ni ndondocha tu anayeweza kukubali kuziacha, kuzisamehe na kuzipoteza nguvu, hela, na muda wake aliouwekeza chadema hasa katika zama hizi za escrow, richmond, epa, meremeta, migogoro ya ardhi, madini, gesi, mafuta na katiba mpya ambayo vyote vinahitaji nguvu kubwa na ya haraka sana kutoka vyama vya siasa mbadala. Itashangaza kusikia mtu mwenye akili timamu ameanzisha chama kipya leo huku taifa likiwa linahitajii nguvu kubwa sana ya pamoja leo leo bila kusubiri kesho. Ni nguvu ya rushwa, mbinu chafu, ujinga na maslahi binafsi tu ndivyo vinavyoweza kupelekea mtu kuanzisha na kujiunga na chama kipya kabisa katika wakati huu tete.
 
Teh teh, nasikia zitto ana akili kuliko wanakigoma wote. Ndo maana amesema mwezi wa kumi watamchagua tena kuwa mbunge wao.
 
Sijawahi kumuamini mtu wa Kigoma...

Me mwenyewe sijawahi kuwaamini wachaga kwani niwazurumatii balaa, wakiona pesa wapo tayar kukutoa roho, je wakiingia ikulu c ndo wananchi watakula nyasiii
 

mkuu nilikua sijajua hivi kumbe zito kabwe ni muanzilishi wa chama cha ACT??
naomba vizibitisho,napenda kulifahamu hili
 

kwa hiyo hata sisi wa rock city ni wachaga? wewe ni mpuuzi, na peleka ujinga wako Lumumba
 
Inaonesha ni rahisi sana kuwafinyangafinyanga wana kigoma ukiwa umepata elimu kidogo. Yaani wapo km bendera

Hapo kuhusu elimu umepiga penyewe. Mwenye ufahamu atakuelewa. Hili jambo ndilo lililo chelewesha sana maendeleo ya Kigoma mpaka wakalalama kuwa wao wanaonekana kama sio Watanzania bali watu wa Burundi, kumbe sababu ni wao wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…