Kigogo wa UVCCM atiwa mbaroni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo wa UVCCM atiwa mbaroni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Averos, Aug 31, 2011.

 1. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Zainab Shaaban, ameburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kukata miti eneo la hifadhi ya misitu.

  Shaaban, ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu, alifikishwa kortini Ijumaa iliyopita na kupelekwa rumande Gereza la Kiruru lililopo wilayani Mwanga baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

  Diwani huyo maarufu wilayani Same, ana mkataba wa kukiuzia magogo kiwanda kipya cha kuzalisha Spirits kwa matumizi ya viwandani cha Kilimanjaro Biochem, kilichopo eneo la Kifaru, wilayani Mwanga.
  Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Mwanga, Hussein Mareng, kigogo huyo wa CCM anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 2, mwaka huu saa 12:30 jioni.

  Inadaiwa kuwa, siku hiyo mshtakiwa ambaye hadi jana alikuwa akisota Gereza la Kiruru, aliingia eneo hilo la hifadhi ya misitu lililopo Kivisini, wilayani Mwanga na kukata miti hiyo.

  Mshtakiwa alikanusha mashtaka hayo na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni na mmoja wa wadhamini hao lazima awe mtumishi wa Serikali.

  Diwani huyo na Mwenyekiti wa UVCCM Same, alishindwa kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa Serikali na hadi jana viongozi wa CCM walikuwa wakihaha kutimiza sharti hilo.
  Source: Mwananchi[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  heko kwa watendaji wetu nchi imeanza kufunguka
   
 3. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  hivi mwenyekiti wa wilaya (uvccm) naye ni kigogo?
   
 4. B

  Bakeza JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 328
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Wacha akafie mbali.
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Namimi nimeshangaa!! Ila kwa vitisho wanavyofanyaga hawa viongozi wetu, ndo hali iliyojengeka. Anaiba, anawanywesha pombe wanamuogopa, na kuanza kumuita kigogo. Haya ni baadhi ya majina kwenye sehemu za burudani kama Bar.
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Aug 31, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  hiyo ni kawaida ya ccm kwahiyo sioni cha ajabu. wizi wao, ufisadi wao, ubabe wao.
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  huyu naye ni kigogo..? au kilemba cha ukoka
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  wizi,ufisadi wa rasilimali ipo kwenye ilani ya ccm ni ruksa!
   
 9. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Ingawa tumeaambiwa hakuna aliye juu ya sheria, kuna wengine wana nguvu kuliko sheria hizo
   
 10. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii wala sio habari hapa Mwenyekiti UVMagamba! Akafie huko
   
 11. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wacha nao wajichukulie pale penye mamlaka napo kama wengine juu wanafanya hayo kwanini isiwe wao?
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kiini macho tu hki sio mda utaskia hana hatia...................
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,026
  Likes Received: 2,675
  Trophy Points: 280
  Chama cha majangili.
   
Loading...