Kigogo wa CCM kortini kwa kulawiti wanawe

Kigogo wa CCM kortini kwa kulawiti wanawe

ALU255

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
2,089
Reaction score
2,126
Moshi. Katibu Msaidizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Rogers Msangi (44), amepandishwa kizimbani mjini Moshi akituhumiwa kuwalawiti watoto wake wawili. Msangi, ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Mwanga, alipandishwa kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi, Anthony Ngowi.

Msangi alikanusha tuhuma dhidi yake na alipelekwa rumande katika Gereza Kuu la Karanga, Moshi baada ya wadhamini wake wawili kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Makosa anayodaiwa kutenda kigogo huyo yanaangukia katika shtaka la kumwingilia binadamu kinyume cha maumbile kinyume cha kifungu 154 cha Kanuni ya Adhabu. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Novemba 16 mwaka huu, katika eneo la Mwangodi wilayani Mwanga, mshtakiwa alimlawiti mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu.

Katika shtaka la pili, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alidai kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu katika eneo hilo, mshtakiwa alimlawiti mtoto wake mwingine mwenye umri wa miaka mitano. Mshtakiwa huyo anayetetewa na Wakili Ralph Njau alikanusha mashtaka hayo.

Hakimu Ngowi alimweleza mshtakiwa kuwa dhamana yake iko wazi kwa masharti kwamba asaini hati ya dhamana ya Sh6 milioni na awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambao ni watumishi wa umma na wenye vitambulisho halali.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na hivyo alipelekwa rumande hadi Desemba 7 kesi hiyo itakapotajwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Atakuwa alishauriwa na mganga wa kienyeji ili apandishwe cheo. Hiyo fedha itamsaidia nini baada ya kuwaharibu watoto wake? Anastahili kufia.jela kwani ni hatari kwa watoto.
 
Hivi kiongozi "kigogo" inaanzia level gani

Kila ukisoma title "kigogo" inakuvuta lakini ukisoma habari yenyewe hamu inaisha.

Napenda kuamini "kigogo" angalau awe kwenye ngazi ya taifa kwenye taasisi husika.
 
Moshi. Katibu Msaidizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Rogers Msangi (44), amepandishwa kizimbani mjini Moshi akituhumiwa kuwalawiti watoto wake wawili. Msangi, ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Mwanga, alipandishwa kizimbani
jana mbele ya Hakimu Mkazi, Anthony Ngowi. Msangi alikanusha tuhuma dhidi yake na alipelekwa rumande katika Gereza Kuu la Karanga, Moshi baada ya wadhamini wake wawili kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Makosa anayodaiwa kutenda kigogo huyo yanaangukia katika shtaka la kumwingilia binadamu kinyume cha maumbile kinyume cha kifungu 154 cha Kanuni ya Adhabu. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Novemba 16 mwaka huu, katika eneo la Mwangodi wilayani Mwanga, mshtakiwa alimlawiti mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu. Katika shtaka la pili, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alidai kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu katika eneo hilo, mshtakiwa alimlawiti mtoto wake mwingine mwenye umri wa miaka mitano. Mshtakiwa huyo anayetetewa na Wakili Ralph Njau alikanusha mashtaka hayo. Hakimu Ngowi alimweleza mshtakiwa kuwa dhamana yake iko wazi kwa masharti kwamba asaini hati ya dhamana ya Sh6 milioni na awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambao ni watumishi wa umma na wenye vitambulisho halali. Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na hivyo alipelekwa rumande hadi Desemba 7 kesi hiyo itakapotajwa.
Naona mchaga kahamua kuwapiga ndonga watoto wake daah!
 
Nadhani watu kama hawa wanatakiwa wafyekwe nyeti zao maana hawawezi kizidhibiti
 
Naona mchaga kahamua kuwapiga ndonga watoto wake daah!
nilisikia mtaalam fulani akifafanua eti tezydumer ama busher ni urithi (genetic) dingi akiwa nalo lazima piga ua zaragaza zika fukua toto lake nalo atalipata tuu.
 
Naona mchaga kahamua kuwapiga ndonga watoto wake daah!

Ritz;
Naona umeamka tu usingizini na kuikuta hii thread. Kanawe uso ndo uje kabla hao wachaga hawajaingia humu kukutukana.
Jina lenyewe tu, si la kichaga hilo. Ni kama mtu akiwa anaishi au hata kujenga Manerumango si Mzaramo. Pole sana
 
Sio mchagga wewe pimbi. Jufanya kazi kule haina maana ni mwenyeji panua ubongo wako. Uko kwenye enzi ya ujima
 
Duuh ilo jamaa lingedanganywa na Huyo Mganga aue mtoto lingeua tuu..izo kesi sio za kukaa ni wiki au wiki mbili tuu kutotengeneza mianya ya Rushwa..ila sio kigogo ni msaka nyoka tuu huyo..
 
Back
Top Bottom