Kigogo TRA adaiwa kumtapeli JK

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
Kigogo mmoja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga, anadaiwa kula njama na kufanikiwa kupata Sh. milioni 2 kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.

Kigogo huyo aliyetajwa kwa jina moja la Masingisa anadaiwa kufanya njama hizo akishirikiana na uongozi wa Serikali ya kijiji cha Chongoleani kumuingiza mkenge Rais wakati alipokwenda kufanya ziara kijijini hapo.

Hayo yalibainika baada ya wananchi wa kijiji hicho kulalamikia kitendo hicho walichodai kuwa ni cha utovu wa nidhamu kwa watumishi wa serikali ambao walitakiwa kuonyesha mfano katika kukemea vitendo vya kihuni kama hivyo.

Wakielezea sakata hilo, wananchi hao walidai kuwa kigogo huyo kwa kushirikiana na uongozi wa serikali ya kijiji walimpeleka Rais kwenye shamba lake ambalo ameanzisha ufugaji samaki na kumdanganya kuwa ni kikundi cha wanakijiji jambo ambalo si kweli.

Omar Mustaph alieleza kuwa wanakijiji hao walidai kuwa Rais alipofanya ziara mkoani Tanga, waliomba atembelee kikundi chao cha ufugaji wa samaki na kwamba uongozi wa kijiji uliwahakikishia kuwa ombi lao la kutembelewa na Rais limekubaliwa.

Mustaph alidai kuwa baada ya Rais kufika wakiwa wamejiandaa kumpokea, walishangaa kuona uongozi wa kijiji kumpeleka Rais katika shamba la kigogo huyo badala ya lile ya kikundi chao.

“Unajua tuliona kama miujiza, tukajiuliza vipi!?. Rais apelekwe katika kikundi kingine badala ya kile cha kijiji?...tulikosa jibu” alisema Mustaph.

Alidai kuwa Rais alichangia Sh. 2 milion katika kikundi hicho fedha ambazo ziliwastahili wanakijiji hicho kuimarisha mradi wao wa ufugaji wa samaki unaosuasua.

Walisema kuwa baada ya Rais kuondoka waliufuata uongozi wa kijiji kuuliza kulikoni Rais kutembelea kikundi kingine badala ya cha kwao na kudai kuwa walipata majibu ya vitisho ya kuwa wasijaribu kuchokonoa mambo ya wakubwa.

Akijibu madai hayo kwa njia ya simu ya kiganjani, mtumishi huyo wa TRA aliyejitambulisha kwa jina moja la Masingisa alikiri kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Rais Kikwete na alipoulizwa kwanini alipelekwa katika kikundi chake badala ya kile cha wanakijiji alidai kuwa yeye pia anastahili kupata fedha hizo na ni haki yake ya msingi.

Alipotakiwa kufafanua madai ya kumtapeli Rais, Masingisa alieleza kuwa kikundi hicho kipo kisheria na kina usajili wake na uongozi na kwamba yeye ni mtunza hazina na kuna mwenyekiti na katibu wake ambao alimshauri mwandishi kuzungumza nao pia.

“Wewe bwana sikiliza, kwanza Rais Kikwete kaja kwangu akijua anakuja kwa Masingisa na wala si kwenye kikundi cha wanakijiji kama inavyodaiwa…usihoji kajaje huu ni urafiki wetu,” alisema afisa huyo.

Aidha alidai kuwa si ajabu kwa Rais huyo wa nchi kutembelea mradi huo kwa kuwa wao ni marafiki wa karibu na kwamba alikuja kama kwa jamaa yake.

“Wewe andika tu! Lakini ukiandika vibaya nitakushitaki, mimi niko nyuma ya wakubwa na wala sina hofu na madai hayo wala kuandika kwako, hata hii kazi niliyonayo aliniwezesha yeye kuipata…wee! andika tu hakuna tatizo,” alisema Masingisa.

Naye Katibu wa kikundi hicho kinachojulikana kwa jina la Kigomen fish farm, Omar Kombo, alieleza kuwa Rais hakupelekwa kwenye kikundi cha wanakijiji kwa kuwa hakukuwa na maandalizi ya kutosha kumpeleka mkubwa wa nchi.

“Ni kweli Rais hakupelekwa, lakini ni kutokana na mazingira hayakuwa mazuri huwezi kumpeleka kiongozi sehemu isiyovutia bwana, hiyo ndiyo sababu kubwa,” alisema Kombo alipozungumza kwa njia ya simu ya kiganjani.



CHANZO: NIPASHE
 
Yeye mbona anacheza madili kama hayo kila siku acha alizwe......kwani viongozi wa ikulu wao hawakwenda mapema kujua sehemu za kutembelea.....Ukiendesha mambo kiswahili lazima ................
 
Hii ndo Bongo bana! Kila kitu possible ila kwa usahihi hajatapeliwa Jk limetapeliwa Taifa kile kijisent cha 2m hakitoki kwenye Wallet ya mtoto wa msoga ni pesa ya serikali so mkusanya mapato kakwapua pesa alokusanya!
 
Wewe soma tu hapa...hata habari hii kataka yeye iandikwe. Ha ha ha ha. Kikwete haishi vituko!
 
Hata kama siyo shamba la kikundi bado linaweza kuwa shamba la mfano wengine wakajifunze hapo
 
"Ikulu imejaa vibaka manzese wanawakamata,meya amekua rais ikulu imejaa wagambo"..........Ashazoea kudanganywa/kupigwa huyo!
 
Duh.., maskini rais wetu. Hivi mpaka mhesimiwa anadanganywa maana yake watu wa itifaki wanakuwa wamedanganyika x2? Au yy ndo aliamua adanganywe?
 
Aiseee babaangu wamekataa kumleta mweshimiwa kwenye kikundi chetu kisa ni kibovu amesahau 2limpigia kura katika mazigira magumu hama kweli 2mesahaulika

ngoja nishushie na mbege wakuu
 
Raha ni aje raisi kuingizwa mjini na watoto wa mjini? Safi sana afisa jk kashatuumiza sana sasa unapopata mwanya fanya kweli mwana
 
Wivu wa Kike...shilingi milioni mbili ndo zaleta kelele zote hizi ....ujinga mtupu... nahamu ya kuporomosha maneno ila tatizo ban...**#?&fK
 
Back
Top Bottom