Kigogo Muhimbili Adaiwa Kufanya Ufisadi

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Kigogo Muhimbili Adaiwa Kufanya Ufisadi
3110830.jpg

Thursday, September 17, 2009 9:07 AM
Kigogo mmoja wa hospitali ya Muhimbili anadaiwa kutaka kuvunja ajira 38 za askari ulinzi na usalama wa kampuni iliyopo sasa ili kuiweka kampuni yake ya ulinzi.Kigogo huyo ambaye jina linahifadhiwa anadaiwa kuanzisha kampuni yake ya ulinzi inayoitwa Diamond ambayo itakuwa mbadala wa kampuni ya ulinzi ya Auxiliary iliyopo sasa kuanzia oktoba mosi mwaka huu.

Wakitoa malalamiko yao wafanyakazi wa kampuni itakayoondolewa walidai kuwa kigogo huyo ameamua kufanya hivyo kwa sababu tayari anategemea kustafu mwezi ujao wa oktoba.

Wafanyakazi hao walisema tayari menejimenti ya hospitali ya Muhimbili imeshaandaa mchakato na ratiba kwaajili ya kuipisha kampuni hiyo.

Wafanyakazi hao walisema kuwa wameshangazwa na hatua hiyo kwasababu wamekuwa wakifanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Wafanyakazi hao walisema kuwa tayari
wameshapeleka shitaka lao katika chama cha wafanyakazi ambapo siku ya
ijumaa kutakuwa na kikao cha pamoja cha wafanyakazi wote wa idara hiyo ya
ulinzi.

Aidha walisema kuwa kampuni ya ulinzi ya kigogo huyo inatarajiwa kuanza kazi tarehe mosi oktoba na hadi sasa hawajui mustakbali wa kazi zao utakuwaje.

"Yeye anastaafu mwezi huu na anataka Kampuni ya Diamond ndio ishike
malindo hapa, wanasema kuwa lengo ni kufanya mabadiliko kufanya maboresho jambo ambalo siyo kweli ila ni maslahi tu ya mtu binafsi baada ya kuona muda wa kustaafu umefika hivyo amebuni njia ya kujipatia kipato" alisema mfanyakazi mmoja wa kampuni hiyo.

Hata hivyo wafanyakazi hao walisema kuwa wanasubiri maamuzi ya chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na Afya tawi la Muhimbili (TUGHE).

"Uamuzi wetu kama wafanyakazi hiyo tarehe moja hatuondoki kwa sababu
tupo hapa kisheria na tunasubiri tusikie Tughe inasema nini kuhusiana na suala hili", alisema mfanyakazi mwingine wa idara ya ulinzi ambaye hakutaka kutaja jina lake.


http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3110830&&Cat=1
 
baada ya kustaafu ndo ananza biashara age yake ni miaka 65, utafanya biashara gani hiyo kama siyo kufanya mambo ya ajabu ajabu tu kama haya
 
Kama mkataba wenu umekwisha mtaondoka tu hata kama mkijisifia kwamba mlifanya kazi nzuri. Mara nyingi mwanzo wa majungu ni kuogopa mabadiliko.
 
Hiyo nayo ni nnshu sio,ila mabadiliko ni muhimu sana ila yawe yenye kuleta tija,kama kuna madhaifu yameonekana basi hawo jamaa waondoke tuu,kustahafu sio hoja ya kuingelea kabisa
 
Back
Top Bottom