Kigogo 'kizimbani' kwa kumiliki bodaboda 420

Kigogo 'kizimbani' kwa kumiliki bodaboda 420

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423
Baraza la Maadili limeombwa kupendekeza kwa mamlaka inayohusika adhabu kali dhidi ya Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Ghulamhussein Dewji, kwa tuhuma za kumiliki mali mbalimbali, zikiwamo pikipiki 422 bila kuzitolea tamko katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kinyume cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Mali nyingine ambazo Dewji anatuhumiwa kuzimiliki bila kuzitolea tamko katika sekretarieti hiyo, ni viwanja vitano; vinne kati yake, vikiwa katika eneo la Ipuli na kimoja Isule pamoja na nyumba moja yenye thamani ya Sh. milioni 16 iliyokuwapo katika eneo la Kazehili, katika manispaa hiyo. Ombi hilo liliwasilishwa na Wakili wa Sekretarieti hiyo, Getrude Cyriacus, wakati akihitimisha hoja za upande wa malalamiko ya ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma yaliyowasilishwa katika baraza hilo dhidi ya Dewji, wiki chache zilizopita.

Hata hivyo, Dewji (46), ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kanyenye katika manispaa hiyo, ameliomba baraza limtendee haki, lisimuumize, limuonee huruma kwa madai kwamba hajakiuka popote, hivyo lione kuwa anataka kukandamizwa kwa chuki za kisiasa.

Wakili Getrude aliwasilisha ombi hilo baada ya baraza hilo linaloongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Hamis Msumi, kusikiliza ushahidi wa uliotolewa na mashahidi wa pande zote mbili pamoja na utetezi wa mlalamikiwa, Ghulamhussein, katika baraza jana. Wakili Getrude alidai ushahidi wa uchunguzi pamoja na nyaraka za vielelezo vilivyowasilishwa katika baraza na upande wa malalamiko unaonyesha kuwa pikipiki hizo bado ziko katika umiliki wa mlalamikiwa.

Hata hivyo, alidai pikipiki hizo zikiwa ni mali yake pamoja na viwanja na nyumba hiyo, mlalamikiwa hakuvitamka katika fomu yake ya rasilimali na madeni ya sekretarieti hiyo, kama Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inavyotaka. Alidai zaidi ya hivyo, mlalamikiwa aliwahi kuitwa kuhudhuria Baraza la Maadili mkoani Tabora kwa barua, lakini hakuitikia wito huo. Pia alidai mali alizonazo mlalamikiwa, yakiwamo magari matatu na duka moja, bado zimeandikwa jina lake na kwamba, sheria iko wazi na kwa hiyo, hawezi kutumia madaraka yake vibaya.

Alidai Mbunge wa Rorya (CCM), Lameck Airo, aliwahi kuadhibiwa kwa kutozwa faini baada ya kubainika kutenda makosa kama hayo. "Hivyo, naliomba, baraza lipendekeze adhabu kali kwa mlalamikiwa ili iwe fundisho kwa viongozi wengine wa umma wenye tabia kama hiyo," alisema Wakili Getrude.

Awali, shahidi wa upande wa malalamiko, ambaye ni Diwani wa Kata ya Nsege katika manispaa hiyo, Kaombwe Mrisho, aliliambia baraza hilo jana kuwa Dewji anatumia madaraka yake vibaya kujilimbikizia viwanja hivyo. Alidai pia amekuwa akitumia madaraka yake kugoma kurejesha mkopo wa zaidi ya Sh. milioni 2.6 zilizochukuliwa kutoka kwenye mfuko wa halmashauri hiyo kwa ajili ya kugharimia safari yake ya kikazi nchini Marekani, mwaka 2011.

Vilevile, alidai kuwa Dewji pia amekuwa akitumia madaraka yake vibaya kufanya hila, ikiwamo kuzuia vikao vya madiwani vinavyoandaliwa vikiwa na ajenda ya kujadili juu ya matumizi yake mabaya madaraka na kuchukua hatua za kumng'oa madarakani.

Alitoa madai hayo akiongozwa na Wakili wa Sekretarieti hiyo, Hassan Mayunga, huku akiliomba baraza limsaidie kuhusu usalama wake kwa madai kwamba, wanakoishi (manispaa ya Tabora) wanajuana.

Kaombwe (65), ambaye amekuwa diwani katika manispaa hiyo tangu mwaka 1988, alidai Dewji alikwenda Marekani yeye na Afisa Mipangomiji wa manispaa kufuatia mwaliko walioupata kutoka Shirika la Changamoto za Milenia la nchi hiyo (MCI) kwa ajili ya kujifunza maendeleo yaliyoko nchini humo. Hata hivyo, alidai kipindi hicho baraza la madiwani halikuwa na uwezo wa kuwagharimia safari hiyo, hivyo wakalazimika kukopa kutoka kwenye mfuko wa halmashauri na Dewji na mwenzake wakalipwa fedha hizo.

"Walikwenda (Marekani) na kurudi, lakini kwa taarifa nilizonazo mpaka sasa fedha hizo hazijarudishwa," alidai Kaombwe. Alidai waligundua suala hilo katika moja ya vikao vya halmashauri, ambako mkurugenzi wa halmashauri alibanwa akitakiwa kurejesha fedha alizolipwa na halmashauri kwa ajili ya safari nchini Ethiopia na yeye kujitetea kuwa anaonewa peke yake, kwani kuna viongozi wengine waliochukua fedha za halmashauri, lakini hawabanwi kuzirejesha.

"Tulipogundua hilo, madiwani tuliandaa kikao maalumu kufahamu suala hilo, lakini hakikufanyika mpaka leo. Sababu ya (kikao hicho) kutofanyika ni pingamizi lililowekwa kwamba, (kikao) hakipo. Madhumuni ya kikao ilikuwa ni kujadili kuhusu matumizi mabaya ya madaraka na kuchukua hatua ya kumuondoa madarakani," alidai Kaombwe. Aliongeza: "Sababu ya kutaka kumuondoa madarakani ni matumizi mabaya ya madaraka, kujilimbikizia viwanja na kutorejesha fedha alizozitumia nje ya nchi.

Hata hivyo, Dewji akimhoji shahidi huyo, alidai kuwa akiwa yeye ndiye kiongozi wa vikao vya baraza la madiwani, hajawahi kusaini muhtasari wa kikao chochote kinachomtaka arejeshe fedha hizo. Pia Dewji alidai viwanja vyote anavyodaiwa kuvimiliki kwa kutumia madaraka yake, alivipata kabla ya kuwa diwani wala meya.
Alidai shahidi huyo ameamua kutoa madai hayo mbele ya baraza dhidi yake kutokana na chuki aliyonayo inayosukumwa na kumshinda katika kinyang'anyiro cha kuwania umeya wa manispaa hiyo.

Jaji Msumi alipomuuliza shahidi huyo kama kiongozi wa halmashauri akisafiri kikazi halipwi masurufu, alijibu analipwa, lakini akasema fedha alizolipwa Dewji halmashauri zilitakiwa zirejeshwe wka madai kwamba, waliambiwa na MCI kuwa wangegharimiwa huduma zote, ikiwamo usafiri.

"Hata mkurugenzi (wa halmashauri) alikwenda Ethiopia, akatakiwa arejeshe fedha alizolipwa, akajitetea kuwa mbona wenzangu hawajarudisha?" alidai Kaombwe. Aliongeza: "Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba usalama wetu, kwa sababu tunakotoka tunajuana."

Jaji Msumi alimtaka afafanue kauli yake hiyo na kudai kwamba, mwaka 2011 yeye na Dewji waligombea umeya katika manispaa hiyo akashindwa na kwa hiyo, hana tatizo naye, isipokuwa alichokuwa akikifanya jana kinahusiana na mambo ya kikazi, lakini anaona mwenzake bado ana dukuduku. Hata hivyo, Jaji Msumi alimweleza Kaombwe kuwa baraza halihusiki kumhakikishia usala wake na kwamba, wakazi wenyewe wa Tabora watajuana.

Akijitetea, Dewji alidai hesabu za halmashauri zilikwishakaguliwa na kwamba, hakuna hoja yoyote iliyotolewa na mkaguzi wa ndani wala na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inayomtaka meya kurudisha fedha hizo tofauti na mkurugenzi wa halmashauri, ambaye alidai kuwa alichukua fedha zaidi yao na kwamba, fedha walizolipwa zilikuwa kwenye bajeti.

"Vikao vya majungu ndivyo vilivyonitaka kurudisha hizo fedha. Nilikwenda (Marekani) kama meya na siyo kama Dewji, hivyo sikutumia madaraka yangu vibaya. Hakuna kikao chochote kilichonitaka nirejeshe fedha, ndiyo maana hakuna muhtasari wa kikao na (shahidi) ameshindwa kuthibitisha mbele ya baraza. Kwa imani yangu nililipwa sawa safari ya Marekani," alidai Dewji.

Alidai pia hana barua yoyote ya afisa uhasibu inayomtaka arejeshe fedha hizo na kwamba, anaamini kilichomponza hadi kufikishwa hapo, mbali ya chuki za kisiasa, pia kutokana na msimamo wake mkali wa kudhibiti mianya ya wizi katika halmashauri iliyokuwa ikitumiwa na baadhi ya watu pamoja na kufuta matibabu ya kienyeji, ambayo yangesababisha halmashauri kupata hati chafu.

Alisisitiza kudai kuwa kamwe hatumii madaraka yake vibaya, kwani amekuwa akitumia fedha kutoka mfukoni mwake na pia gari lake bila kutumia bendera ya meya kusaidia shughuli za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kurejesha moja ya miradi uliotaka kufa katika manispaa hiyo. Alidai kikao cha madiwani anachotuhumiwa kukizuia, hakikuwa halali, kwani waliokiandaa walighushia majina ya watu, ambao siyo madiwani.

Dewji alidai tuhuma zinazoelekezwa kwake na Kaombwe zinasukumwa na chuki binafsi za kisiasa, kwa madai kwamba, shahidi huyo aliwahi kuwa katibu wa kampeni za kumng'oa katika umeya, ingawa alimshinda kwa kura 25 dhidi ya kura nne alizoambulia katika uchaguzi huo na kwa hiyo, alikwenda kwenye baraza jana kwa nia mbaya ya kumkandamiza. Alidai ukiondoa gari moja kati ya magari aliyokuwa akiyamiliki, ambalo ni mali ya mkewe alilonunuliwa na mjomba wake kutoka Uarabuni, magari mengine yaliyosalia aliyamiliki akiwa hajawa diwani wala meya na kwamba, yote alikwishayauza, hivyo hakuna gari aliloficha kama alivyotuhumiwa. Alidai hapaswi kubanwa kuhusu uhamisho wa umiliki wa magari aliyoyauza, kwani hilo ni jukumu la aliyenunua na yeye hawezi kumkaba afanye hivyo.

Pia alidai viwanja vyote anavyovimiliki aliviomba kwa njia za halali na kuvilipia na pia nyumba anayodaiwa kuimiliki, aliinunua kwa mkataba na kuivunja na kubaki kiwanja na kwamba, vyote alivipata akiwa hajawa meya wala diwani na aliitamka nyumba hiyo katika fomu za sekretarieti hiyo kama kiwanja.

Vilevile, duka ambalo ni chanzo cha mapato yake, alidai kuwa alilitamka kwenye fomu hizo kama biashara na kwamba, halijafichwa, hivyo akaomba kama alikosea kisheria, anaomba aelekezwe usahihi. Kuhusu kumiliki pikipiki 422, alidai pikipiki zilizopo katika mkoa wote wa Tabora hazifiki idadi hiyo, siyo mali yake, bali ni ya kampuni moja ya Wachina, ambayo naye alikuwamo na kwamba, hata hivyo, biashara ya vyombo hivyo vya moto imekwishafutwa kwa kampuni hiyo.

Jaji Msumi alisema uamuzi wa baraza utapelekwa kama mapendekezo kwa mamlaka husika kama sheria inavyotaka.
chanzo: NIPASHE
 
boda boda 420 kama kila boda boda kwa siku ni shiling elfu kumi huyu jamaa anaingiza miloni mia nne ishirini kila siku
what a business....!!!
 
boda boda 420 kama kila boda boda kwa siku ni shiling elfu kumi huyu jamaa anaingiza miloni mia nne ishirini kila siku
what a business....!!!
mkuu...umechanganya mawazo mawili kwa wakati mmoja...
moja ni bei ulitakazungumzia na pili ukataka kupiga inngizo la siku kwa maana ya 10000×420=4,200,000..
 
boda boda 420 kama kila boda boda kwa siku ni shiling elfu kumi huyu jamaa anaingiza miloni mia nne ishirini kila siku
what a business....!!!
Dah! Hivi una akili timamu kweli wewe? Hizo hesabu zako una hakika nazo?
 
boda boda 420 kama kila boda boda kwa siku ni shiling elfu kumi huyu jamaa anaingiza miloni mia nne ishirini kila siku
what a business....!!!

Me sijui hesabu lakini wewe ni kilaza.... Sio kla uzi lazima ujibu ndugu
 
Wadanganyika, ndio sindano zenyewe hizo. Endeleeni kusikilizia maumivu bila kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom