Kigogo Chadema aliyetekwa afichwa

Status
Not open for further replies.
Chadema bwana.fukuza fukuza haikuzi.inadhoofisha.kinachoshangaza hawaoni km mwisho wao umefika wajipange.
 
kweli cdm kimekuwa ni chama cha kimafia, ukimtazama slaa ma mbowe huwez kudhan kama wanaweza kufanya unyama huu!! Hawa watu ni wauwaji na ikitokea bahat mbaya wakashka dola tumeumia watz tutakukuwa tunaomboleza vifo vya watz wenzetu kila kukicha.
 
unakuta jamaa alipokea zile laki mbili za zitto kwa propaganda kama hizi wakati zitto alipokea bilioni mbili kutoka ccm.
 
unakuta jamaa alipokea zile laki mbili za zitto kwa propaganda kama hizi wakati zitto alipokea bilioni mbili kutoka ccm.

hamna cha kupokea bil2 ni propaganda tu za akna mbowe na slaa lakn mipango yao imekwama
 
Kutokana na habari hii,nimejiridhisha kwamba huyu jamaa alijiteka mwenyewe na kujiburuza,ili asingizie wenzake aliokuwa na ugomvi nao
nasema hivyo kwasababu: wenzake waliotekwa kiukweli Dr,Ulimboka na Kibanda waliumizwa vibaya kiasi cha kupelekwa nje ya nchi,iweje huyu aliruhusiwa siku hiyo hiyo aliyofikishwa hospitali na Daktari anakiri kuwa alikuwa anaendelea vizuri.Naamini watu wote wanaoruhusiwa kurudi nyumbani kitaaluma ya udaktari huwa wanaendelea vizuri au matibabu yameshindikana,sasa huyu tunaambiwa anaendelea vizuri,pili Huyu jamaa tofauti na wenzake kwa maelezo ya kova alisema aliwatambua waliomtesa na kuwaambia palepale kwamba amewafahamu jambo ambalo lingemsababishia kuuawa au kuumizwa vibaya sana,cha kushangaza ndo akaumizwa kidogo akatupwa nje ya mji,akaokotwa na wasamalia na kupelekwa hospitali kisha akaruhusiwa siku hiyo hiyo?
Hadithi nyingine za kupika zinakuwa hazijaiva sawasawa.
 
Mtekwaji aanikumbusha yule shehe wa Uamsho Zanzibar. Yanaamwisho haya yote.
 

kuna haja ya chadema kuachana na hawa viongozi NJAA KALI wanarubuniwa kwa urahisi sana bhana !
 
Vijigazeti vingine bwana lol havina story wala habari za maana daily propaganda kweli bora kilipofungiwa tu.
 
Bahati nzuri waTZ asilimia kuubwa husahau sahau kama mataahira! mbona kwa kumbukumbu zangu toka vyombo vya habari huyu bwana alishatolewa hospitalini akiwa yupo fit!

Kuna mtu akaandika uzi humu kuwa kuna sanaa inataka kuandaliwa na kumrudisha huyo bwana hospital ili, tamthilia ya ugaidi ichezwe, sasa ndio naona inaanzia hapa! Acheni ushetani! adhabu yake toka kwa Mungu kwa usingiziaji ni kuubwa.
 

Mkuu nadhani ni wewe uliweka uzi wa,kuandaliwa tamthilia ya ugaidi kupitia kwa huyu bwana!

Naona mipango inaendelea vizuri na sasa imeanzia mtanzania, hivi hawa mabwana huwa wanajua consequnce za uingiziaji?
 
Huyu jamaa itakuwa aifanya mipango ya kujiteka mwenyewe ii kutengeneza muvie kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe. Sasa baada ya madaktari jumshtukia kwamba hana majeraha ns wala haumwi hawakuona hoja ya kuendelea kuwa nae wardini. Hapo ndipo zinakoanzia stori za kuhamishwa kwenda kutibiwa nyumbani.
.
 

Hii mipango inayopangwa na watu fulani kwa nia ya kuiumiza chadema kuna siku yote itakuja wekwa hadharani,hakuna siri ya watu wawili.

Huwezi ukawa unadhuru watu kijinga jinga tu kisa chadema,kama sera zako zimeshindwa toka madarakani kajipange upya,kwani nchi ipo miaka nenda miaka rudi why utese binadamu mwenzako kisa madaraka? Movie kama hizi mara nyingi huwa silipi kingilio naingia bure tu
 
Utekwe,uumizwe,utupwe halafu matibabu ya Elfu 50 na uruhusiwe.. THUBUTUU,muulizeni Dr Ulimboka maana ya kutekwa?

ikafotolewa picha moja Ununio ikasambazwa media zote..wataamini watoto hii tamthilia.NICK TV
 
Yona bana,anapenda sarakasi wakati hajui kuziruka,amejichubua mwenyewe arafu anadai wamemteka! watekaji gani hao hawajakutoa hata jicho? UNATUMIKA YONA!
 
Eeeh Mwenyezi Mungu iepushe Tanzania na hizi njama mpya za kubambikia watu kesi za uhaini.AMEN
 
Eeh Mungu iepushe tanzania na hiki chama.
 
Mbona Ulimboka na Kibanda familia zao hazikuwaficha? Tatizo la huyu mwenyekiti madai yake ya kuteswa na kuumizwa ni sawa na mcheza filamu sisi watazamaji tunapoiona tumwona kama kaumizwa vibaya kumbe uongo kajipaka rangi tu na kutengeneza kidonda. Haya Kova njoo na seaso 2, ya hii filamu tuone.

 

Umeme Bei juu, Maisha yamekua Magumu kupita maelezo yote sababu ya MaCCM. Watanzania tuwashughulikie hawa 2014/2015. Hakuna kucheka na Nyani.
 
Operation tokomeza haikutosha kuwaumiza wananchi....
 
Watu wanatafuta umaarufu,huyo Yona,hata alikuwa hafahamiki,tumeanza kumjua sasa.hongera zake
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…