Kigogo Chadema aliyetekwa afichwa

Kigogo Chadema aliyetekwa afichwa

Status
Not open for further replies.

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
JUMAMOSI, JANUARI 11, 2014 10:16 NA PATRICIA KIMELEMETA

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Temeke, Joseph Yona ameondolewa hospitali alikokuwa akipatiwa matibabu na kufichwa kusikojulikana. Chanzo cha habari kimelieleza MTANZANIA Jumamosi kwamba, Yona ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), amehamishwa na familia yake kutokana na sababu za kiusalama.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, familia imefikia uamuzi wa kumhamisha baada ya kuona watesi wake (wabaya) wanamfuata Yona hospitalini hapo.

Kutokana na mazingira hayo, familia hiyo ililazimika kumuomba daktari aliyekuwa akimhudumia mgonjwa huyo kumruhusu ili waweze kumtibu nyumbani kwao.

“Kutokana na hali hiyo, daktari alimruhusu baada ya kuona hali yake inaendelea kuimarika, licha ya kuwepo kwa majeraha ambayo yasingeweza kumletea matatizo makubwa.

“Familia ya Yona ilimuomba daktari aliyekuwa akimtibia kumruhusu kuondoka, ili aweze kutibiwa na daktari binafsi chini ya uangalizi maalumu wa familia, kwa sababu watesi wake walikuwa wakimfuata hospitalini hapo.”

Chanzo hicho kilichopo karibu na familia hiyo, kilieleza kuwa Yona alitolewa siku ile ile aliyofikishwa hospitali na kufichwa kusikojulikana kwa sababu za kiusalama, baada ya kuwataja watesi wake hadharani.

Hata hivyo, Ofisa Habari wa MOI, Patrick Mvungi alithibitisha kutolewa kwa mgonjwa huyo siku hiyo alipolazwa na kudai kuwa mgonjwa huyo alikuwa akiendelea vizuri.

“Baada ya daktari kumpima na kumuona anaendelea vizuri, wameamua kumruhusu kurudi nyumbani na kwamba mpaka sasa hajarudi tena katika taasisi hiyo,” alisema Mvungi.

Yona alitekwa, kupigwa, kuteswa na watu aliodai ni baadhi ya wanachama wenzake wa chama hicho, kwa madai kuwa amekuwa akishirikiana na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Zitto Kabwe.

Baada ya kupigwa, Yona alipelekwa katika eneo la Ununio, Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kuokotwa na wasamaria wema wanaoishi karibu na maeneo hayo.

Kutokana na hali hiyo, mgonjwa huyo alipelekwa MOI kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo alipimwa kwa kipimo cha CT-Scan pamoja na kufanyiwa vipimo vingine vya kitabibu.

Awali akielezea mkasa huo, Yona alisema aliingia katika mgogoro huo baada ya kuitisha kikao cha waandishi wa habari na kuiomba Kamati Kuu ya Chadema kuitisha mkutano wa kujadili suala la Zitto na wenzake.

Mbali ya Zitto, watuhumiwa wengine walikuwa ni aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba.

Alisema kutokana na hali hiyo, viongozi wakuu wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa walimuita na kumwambia ajitoe ndani ya chama hicho kabla ya kumfukuza, jambo ambalo alilipinga.

Hata hivyo, Dk. Slaa amekanusha madai hayo na kueleza kuwa hajawahi kuwasiliana na Yona kwa lengo la kumshinikiza ajiuzulu wadhifa wake huo.

c.c
kibogo

Haya ni mazingaombwe mengine ya kuwahadaa watanzania na vitendawili visivyo teguka.
 
chadema kuweni wavumilivu musilazimishe mambo siyo mbaya mtu kutoa ushauri unajua nyie mupotofautiana kitogo tu na mtu anakuwa adui yenu nakibaya zaidi nipale munapoaza kumuchogea kwa umma mzima eti msaliti. sasa hivi huyu bwana alikuwa mwezenu lakini kule kutoa ushauri kuhusu munavyo mufanyia kijana zitto imekuwa nongwa. kwanini?
 
Mkuu naona unalalamika unataja chadema hivi chadema ni kina nani sababu unavyo taja utadhani kunamtu unamhamu anaitwa chadema.
 
wewe ukigombana na mumeo unaitisha press conference?
 
Joseph Yona ameondolewa hospitali alikokuwa akipatiwa matibabu na kufichwa kusikojulikana.
Hivi kafichwa au kajificha?.... Hali aliyokuwa nayo angeweza kutoka hata kusafiri safari yas mbali, tofauti na yaliyomkuta Dr. Ulimboka.
 
Mi nasubiri kibogo ajibu ili nijue chanzo cha mada hii kuwa 'cc' kwake!!!!

Anaejua alipo ni Zzk, mshirika wake!! Alafu inakuwaje watesi wake wawe CDM wakati hawakuwemo kwenye "mgao" uliotoka kwa ZZKCCM!!!??
 
Haya ni mazingaombwe mengine ya kuwahadaa watanzania na vitendawili visivyo teguka.

Kipi ni mazingaombwe na kitendawili kisichoteguka hapo! Kasema ameingia mgogoro na Mbowe na Slaa kuhusu Zitto na wenzake, yeye alikuwa upande wa Zitto. Hapo tunangojea nini? Kamata Mbowe na Slaa tupa kureeeeee!
 
Upelelezi kwanza, kama ni lazima kuwakamata itakuwa baadaye. Hata hivyo sio kila jambo linalosemwa na mwathirika ni la kweli, ndio maana licha ya kuwepo kwa hear say nying kuhusu kibanda na ulimboka hakuna aliyewekwa mkononi!! Tuwaache Polisi wafanye wanayoona au wanavyoweza! HERI YA MWAKA MPYA!
 
JUMAMOSI, JANUARI 11, 2014 10:16 NA PATRICIA KIMELEMETA

Kwa mujibu wa chanzo hicho, familia imefikia uamuzi wa kumhamisha baada ya kuona watesi wake (wabaya) wanamfuata Yona hospitalini hapo

“Familia ya Yona ilimuomba daktari aliyekuwa akimtibia kumruhusu kuondoka, ili aweze kutibiwa na daktari binafsi chini ya uangalizi maalumu wa familia, kwa sababu watesi wake walikuwa wakimfuata hospitalini hapo.”

Kama wabaya wanajulikana kwanini hawakamatwi.
Isijekuwa hii nayo ni sinema nyingine!
 
chadema kuweni wavumilivu musilazimishe mambo siyo mbaya mtu kutoa ushauri unajua nyie mupotofautiana kitogo tu na mtu anakuwa adui yenu nakibaya zaidi nipale munapoaza kumuchogea kwa umma mzima eti msaliti. sasa hivi huyu bwana alikuwa mwezenu lakini kule kutoa ushauri kuhusu munavyo mufanyia kijana zitto imekuwa nongwa. kwanini?

Omba uraia ufundishwe kiswahili
 
Operation Kimbunga njooni huku,kuna muhamiaji haramu,amesalia...na ili msimgundue amejivika uanachama wa chama dola....Kamata huyuuuu!!!
 
hiki chama cha ajabu sana kinataka uwe jiwe usihoji wala kuuliza afu wanataka nchi waende zao uchagani huko.
 
Huyu jamaa alitibiwa mapema,na Chadema walimgharamia ghalama zoooote za matibabu.....akaruhusiwa arudi nyumbani mana hali yake ilikuwa njema bila mawaa....lkn kuna ”wahuni“ wachache wakamrudisha hospitali ili apate nafasi ya kuongea na magazeti aina ya MTANZANIA na kupewa maneno ya kuongea.
Gazeti linajichanganya,mara liseme ametoka sbb hakukuwa na haja ya kubaki wodini, hapohapo linasema ametoroshwa....utamtoroshaje mtu ambaye alisharuhusiwa na ikaonekana hana tena sbb za kubaki wodini???
Kuna kikundi cha watu wapo radhi kufitinisha nchi na watu wake kwa udini,ukabila na ukanda ili kiendelee kukaa madarakani..
 
Tamthilia inaendelea....kuna watu ndio wanelekea mwisho wa safari. Sasa wanatafuta wakumaliza nao.
 
Huyo yuko nyumbani kwa gaidi savimbi anafundwa ili akitoka wamtembeze nchi nzima kama walivyofanya kwa ule msukule wa Igunga.
 
Mkuu naona unalalamika unataja chadema hivi chadema ni kina nani sababu unavyo taja utadhani kunamtu unamhamu anaitwa chadema.

Ah! Mkuu chadema ni Mbowe, hilo likowazi Hao wengine ni vifaranga vyake tu,hilo linazihirika pale mtu anapptofautiana na Mbowe pasi mtu huyo huandamwa na chadema yoote. Inamaana akili za wana chadema zoote zimeshikiliwa na Mbowe.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Hivi kafichwa au kajificha?.... Hali aliyokuwa nayo angeweza kutoka hata kusafiri safari yas mbali, tofauti na yaliyomkuta Dr. Ulimboka.

Kinachoshangaza ni kwamba Yona alishatoka hospitali (MoI) na alilipiwa matibabu na mratibu wa kanda ya pwani Bw Tugara kiasi cha shilingi elfu 50,000/ na akakodiwa na kulipiwa Tax mpaka nyumbani kwake, Lakini baadae akarudishwa tena na waliokuwa wanapanga njama za ugaidi.

Tanzania haiishi vituko! yaani ugaidi unalazimishwa kwa kupangwa kama mafungu ya nyanya!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom