Wakuu, ki ukweli, Prof. Issa Shivji kanena ukweli mtupu! Nimefurahi sana binafsi. Pia akina Prof. Lipumba, Mzee Butiku, Kingunge, na wengineo wanaonekana kabisa kukubaliana na hoja za Shivji.
Na katika hoja kubwa ambayo hata mimi ilikuwa inanipa tabu, ni kuhusu aina ya Katiba Wananchi waliyokuwa wanatolea maoni. Prof. Anasema, tulitaka Mlima, tukaletewa Kichuguu. Kwa maana ya kwamba, Tulijua kabisa tunataka katiba ya Bara pamoja na ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa Tume imekuja na katiba moja, tena yenye mkanganyiko kibao.
Na alienda mbali zaidi na kusema kuwa, je, kama siyo hujuma kwa tume kutumia pesa yote na kuja na rasimu moja tu, ni lini Wananchi wataitwa tena kutoa maoni ya Katiba ya Zanzibar na Bara, kwa gharama zipi na muda gani???.
Inaonekana Jaji Warioba na timu yake ndo wanataka kufanya hicho kijiwe cha kuvuna.
Wataalam wakiipata wailete hapa ili tuisikilize tena!