Kifurushi cha Tigo Home Internet

utakuja

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Posts
1,062
Reaction score
996
Habari za asubuhi wakuu! Kwenye pita pita zangu kwenye menu ya tigo *147*00# nimekutana na hichi kifurushi cha Home Internet, na kwa bei hii nimeona kama kizuri kwa GB wanazotoa kwa mwezi especially hapo kwenye GB 100. Ningependa kujua kwa waliokitumia, experience yenu ilikuwaje kabla sijapoteza elfu 85 zangu; kwa kuwa nina miaka isiyopungua 3 line yangu ya Tigo sijawahi tumia kwa internet. Sasa naona vodacom hakuna vifurushi vizuri, na TTCL spidi yao sio nzuri kivile.
 
Nimeshajaribu kwenda kwa haya makampuni yanayo toa huduma za Fibre to home, na Majibu yao ni kuwa hawafikii maeneo nje ya city centre. Wateja wao ni Masaki, Oyster Bay n.k
Na of course hiyo line itakaa kwenye Wi-Fi router.
jaribu TTCL mkuu kwa bajeti hio nizaidi ya kitonga labda kama eneo ulilopo sio rafiki
 
This is excellent! Kudos Tigo.

Kwenye router yangu nimeweka SIM ya Voda, though expensive speed inaeleweka. Niliachana na halotel sababu ya speed.

TTCL ni non competitive, smile too expensive.

Please mitandao mingine wekeni hivi vifurushi. Siku hizi nyumba nyingi ni IT enabled. Tunahitaji constant internet connection to share across multiple devices bila woga wa kuangalia salio la MB.
 
Nilienda ofisini kwao Ijumaa wakaniambia leo ndio zitakuwepo. It's interesting sema kuna kamchezo kachafu sana nimekagundua wanakacheza hapa...
Your browser is not able to display this video.
 
Huu sio usanii kweli. Kuna vifurushi vya wiki na vya mwezi, vya wiki unapata cha 25k-40GBs ila only 20Gigs ndio unaweza kuzitumia mchana, zingine zote zinatumia usiku saa sita mpaka saa kumi na mbili. Same goes kwa package zingine za juu ya hapo. Ni unapata nusu ya size hiyo mchana. I mean i am a night owl and will probably use zote hizo za usiku lakini this is cheating ase. Wanadanganya watu kwa kutoweka this fact clear.

cc: Chief-Mkwawa utakuja

 
Hata Mimi niliona mkuu, Kuna usanii Fulani, Hapo Ni nusu kwa nusu, hivyo vinakuwa sio value for money kucompare na vifurushi vyengine.
 
Aisee niliona, sasa mbaya zaidi ni huo muda walioweka saa 6 usiku yani dah! Zamani huu muda ulikuwa sio tatizo kwangu lakini now labda Friday na Saturday ndiyo hizi GB nitaweza kuzifahidi.
 
Aisee niliona, sasa mbaya zaidi ni huo muda walioweka saa 6 usiku yani dah! Zamani huu muda ulikuwa sio tatizo kwangu lakini now labda Friday na Saturday ndiyo hizi GB nitaweza kuzifahidi.
Hata Mimi niliona mkuu, Kuna usanii Fulani, Hapo Ni nusu kwa nusu, hivyo vinakuwa sio value for money kucompare na vifurushi vyengine.

Dah yani wizi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…