Kifurushi cha Nyota cha Startimes

Kifurushi cha Nyota cha Startimes

steveachi

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2011
Posts
11,342
Reaction score
13,364
Habari wakuu,

Mimi ni mtumiaji wa hiki king'amuzi cha Startimes. Kuna hiki kifurushi kipya kilichoingia sokoni hivi karibuni kinachoitwa 'Nyota', Kiukweli kifurushi hiki kimejali hali ya mtu wachini kabisa kwani bei yake ni poa ni Tshs.4,000/= tu kwa mwezi.

Nawapa pongezi Startimes kwa kuangalia suala hilo. Kilichonisukuma kuweka uzi huu ni kuwa, nimejaribu kuangalia kwenye Facebook Page ya Startimes, tovuti ya Startimes, sijaona maelezo yoyote ya kutosha yanayoonyesha chaneli zilizopo katika kifurushi hiki.

Ombi langu kwenu ambao mnatumia king'amuzi hiki, naomba kujulishwa hiki kifurushi kina chaneli zipi ili kama vipi nijisubscribe huko nikiona zinanifaa.

Pia ushauri wangu kwa hii kampuni ya Startimes ni kuwa, wawe na taarifa za kutosha katika tovuti yao juu ya huduma mbalimbali wanazotoa kuliko kuja humu na kujaza seva ya JF tu kama nilivyofanya hapa wakati maelezo nayoyataka nilipaswa kuyapata katika tovuti yao. Tovuti yao ina taarifa za zamani sana tokea kifurushi cha 'KILI' kilipokuwa hakipo.

Ni vema watu wao wa IT wafanye kazi yao sio wanalipwa mishahara tu huku tovuti ikiwa haina masuala ya msingi mteja anayopaswa ataarifiwe..

Naomba kuwasilisha na karibuni kwa kuniambia chaneli zilizopo kwenye kifurushi cha 'NYOTA'.
 
Karibuni sana wakuu,kifurushi nilichokuwa nalipia mara kwa mara cha UHURU kimeisha, nataka kujiunga hiki cha NYOTA
 
Continental hatulipi hata centi ila tunaangalia zaidi ya channel 24 zikiwepo chenell 3 za kenya Emmanuel SCOAN na Channel zote za International
 
Continental hatulipi hata centi ila tunaangalia zaidi ya channel 24 zikiwepo chenell 3 za kenya Emmanuel SCOAN na Channel zote za International

Safiiii,wana channel gani za series au movies,manake mie ndio mikato yangu hiyo??
 
Habari wakuu,

Mimi ni mtumiaji wa hiki king'amuzi cha Startimes. Kuna hiki kifurushi kipya kilichoingia sokoni hivi karibuni kinachoitwa 'Nyota', Kiukweli kifurushi hiki kimejali hali ya mtu wachini kabisa kwani bei yake ni poa ni Tshs.4,000/= tu kwa mwezi. Nawapa pongezi Startimes kwa kuangalia suala hilo. Kilichonisukuma kuweka uzi huu ni kuwa, nimejaribu kuangalia kwenye facebook page ya startimes, tovuti ya startimes, sijaona maelezo yoyote ya kutosha yanayoonyesha chaneli zilizopo katika kifurushi hiki.

Ombi langu kwenu ambao mnatumia king'amuzi hiki,naomba kujulishwa hiki kifurushi kina chaneli zipi ili kama vipi nijisubscribe huko nikiona zinanifaa.

Pia ushauri wangu kwa hii kampuni ya startimes ni kuwa, wawe na taarifa za kutosha katika tovuti yao juu ya huduma mbalimbali wanazotoa kuliko kuja humu na kujaza seva ya JF tu kama nilivyofanya hapa wakati maelezo nayoyataka nilipaswa kuyapata katika tovuti yao.Tovuti yao ina taarifa za zamani sana tokea kifurushi cha 'KILI' kilipokuwa hakipo.
Ni vema watu wao wa IT wafanye kazi yao sio wanalipwa mishahara tu huku tovuti ikiwa haina masuala ya msingi mteja anayopaswa ataarifiwe

Naomba kuwasilisha na karibuni kwa kuniambia chaneli zilizopo kwenye kifurushi cha 'NYOTA'

Ama Kweli Hayati Babu Yetu Kaacha Wajukuu Vichwa Kama Vile Alivyokuwa Yeye. Mwenyezi Mungu Amrehemu Huko Aliko Na Sisi Wajukuu Zake Tunapita Mule Mule Alikopita Yeye! Oya Kijana Narudi Kwako Kwani Umelazimishwa Kuwa Huko Startimes? Hamia Dstv Kijana Kwani Ndiyo Mpango Mzima ( Mmmmmmh! Hii Mikogo Yote Utafikiri Nina King'amuzi Vile Wakati Kutwa Nashinda Vibanda Umiza ). Dogo Wamekusikia Na Nadhani Msemaji Wao Aitwae Erick Yumo Humu Jamvini Hivyo Vuta Subira Kijana Otherwise Nisalimie Wote Hapo Mji Kasoro Bahari Morogoro. Vipi Wajumbe Wa Mkutano Mkuu Wa TFF Jana Hawakupindua Meza Kama Walivyotuahidi?
 
Continental hatulipi hata centi ila tunaangalia zaidi ya channel 24 zikiwepo chenell 3 za kenya Emmanuel SCOAN na Channel zote za International

Mtakapoanza Kulipishwa Msije Tu Mkatutolea Mapovu Humu! Nyie Subirini Tu Wanawavutieni Kasi Kimtindo.
 
Nashangaa sana katika kipindi hiki cha digitally, zilizokuwa free channel zinazolushwa pitia masafa ya satellite ndo zinauzwa kwa raia wa Tanzania
 
Ama Kweli Hayati Babu Yetu Kaacha Wajukuu Vichwa Kama Vile Alivyokuwa Yeye. Mwenyezi Mungu Amrehemu Huko Aliko Na Sisi Wajukuu Zake Tunapita Mule Mule Alikopita Yeye! Oya Kijana Narudi Kwako Kwani Umelazimishwa Kuwa Huko Startimes? Hamia Dstv Kijana Kwani Ndiyo Mpango Mzima ( Mmmmmmh! Hii Mikogo Yote Utafikiri Nina King'amuzi Vile Wakati Kutwa Nashinda Vibanda Umiza ). Dogo Wamekusikia Na Nadhani Msemaji Wao Aitwae Erick Yumo Humu Jamvini Hivyo Vuta Subira Kijana Otherwise Nisalimie Wote Hapo Mji Kasoro Bahari Morogoro. Vipi Wajumbe Wa Mkutano Mkuu Wa TFF Jana Hawakupindua Meza Kama Walivyotuahidi?

Hahahahaaaaaaaaa,Mkuu bwana,DSTV ya kishua hiyo kaka,bado sijafikia level hizo,ila inshallah,soon tu nitayapiga mtama maisha
 
startimes wamekosa soko

Aisee ni kweli mkuu naanza kuamini hili ulisemalo,hadi sasa sijapata kabisa jibu la swali langu,inaonekana humu wengi ni watumiaji wa ving'amuzi pinzani na startimes
 
Chanel ni za ajabu ajabu wala sikushauri ununue kifurushi hicho. Sio nzuri kiujumla. Endelea na kile cha elfu kumi tu angalau.
 
Chanel ni za ajabu ajabu wala sikushauri ununue kifurushi hicho. Sio nzuri kiujumla. Endelea na kile cha elfu kumi tu angalau.

Haina noma mkuu,nauchukua huu ushauri,ungeweza kunitajia hizo chaneli kama unazipata mkuu??
 
ST ZONE
ST SINO DRAMA
CITIZEN TV
E STARS
ST KUNG FU
ST SWAHILI
ST SPORTS FOCUS
CGTN
SMILE OF CHILD
ST MUSIC
WASAFI TV
TBN
IQRAA
 
Back
Top Bottom