Kifua kubana. Msaada

BabaPrince

Senior Member
Jan 10, 2016
126
46
Habari zenu wan jf. Nina mtoto wa kiume umri miezi tisa sasa, amezaliwa hana tatizo lolote la kifua ila leo nimeshangaa kifua kimembana usiku mida ya saa tano hivi , nimeshindwa nimsaidieje maana sina uzoefu na matatizo ya kifua kwakuwa hajawahi kuwa na tatizo hilo kabla. Kikimbana anaonekana anavuta pumzi kwa shida sana, akinyonya kidogo kinaachia. Sijajua ni pumu au pneumonia. Naombeni msaada wenu ndudu zangu.
 
Usimlaze uchi usiku mvalishe nguo,pia asiwe anachezea maji sana wakati anaogeshwa aogeshwe haraka na maji ya uvuguvugu na atolewe haraka afunikwe na taulo,yaan ni baridi linamfanya abanwe kifua,mkinge na baridi
 
Asante mkuu. Ila hachezei maji wala halali uchi. Nadhani labda hilo la kuoga. Au huenda ni kubadili mazingira maana nimetoka juzi Kilimanjaro nimekuja huku Lushoto , baridi
 
Pia angalia dalili nyingine kama kikohozi, homa na mtoto kulia, na kama kuna sauti yoyote kama mluzi inatoka pale anapovuta pumzi.....ukiona hali si nzuri muwahishe hospitali....
 
Ana kikohozi ndiyo japo si kikali sana na si cha mara kwa mara. Sauti kama mluzi hakuna. Asante kwa ushauri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom