Kifo siku ya harusi simulizi

Kifo siku ya harusi simulizi

JOLISHA

New Member
Joined
Jun 15, 2019
Posts
1
Reaction score
1
KIFO SIKU YA HARUSI
MTUNZI JOSHUA LIBERATH
0713111547 WHATSAPP

Ilikua siku ya jumatatu asubuhi Jesca aliamka akiwa mwenye huzuni sana ,hakujua ni kwa sababu yupo katika hali ile ,taratibu jesca aliamka na kutoka kitandani kisha alijikongoja na kuchukua maji ya kuoga na kuelekea bafuni ,baada ya kuoga jesca alimkuta mama yake mzazi akiwa tayari amekwisha andaa chai kwa ajili ya familia jesca tara

alivuta kikombe cha chai na kuanza kunywa chai
Mama mzazi wa jesca alipomtazama jesca aligundua kuna tatizo kwa haraka alimwuliza
``hey jesca mwanangu kulikoni mbona una huzuni sana kwani nini kibaya ???’’
``mhhh mama hamna tatizo ‘’
``mwanangu kuwa mkweli sasa unamficha mama yako mzazi nani mwingine utamwambia ‘’
``sijakuficha mama uchovu tu mama ake’’
``sawa mwanangu ngoja nielekee kazini nadhani umeona oda ya sweta nilizopewa na shule ya mitorombo kazi ni ngumu sana mwanangu’’
``sawa mama kazi njema ‘’
**********************************************************************************
Ilipofika majira ya saa sita mchana jesca akiwa anaendelea na kazi zake za nyumbani alisikia simu yake ikiwa inaita
Kwa haraka aliikimbilia alipotazama juu aliona jina la Mery ,aliichukua simu yake na kuipeleka masikioni asijue ni nini shoga ake mery atamwambia .alipoipeleka tu masikioni mazungumzo yalikua hivi
``woooooooo shoga ‘’
``nini Mery kuna nini dia mbona una raha sana kipenzi ‘’
``shogaaaaaa hatari sana yaaan tumepasua yaaan huwezi amini matokeo ya form six yametoka na umefaulu nimekuchekia una division one umepata daraja la kwanza my hongera zako’’
``wooooo can’t believe dia ya kweli hayo’’
``ndioooo honey hapo ni mwendo wa chuooooooo ‘’
``hongera sana ‘’
``hongera pia na wewe ‘’
``asante ‘’
Simu ilikatwa Jesca huku akirukaruka alikimbia hadi alipo mama yake alipomkaribia alijilaza chini huku akipiga kelele za furaha kweli lilikua ni jambo la kufurahisha sana kwake .
Mama mzazi pamoja na kaka na baba yake walimpongeza sana jesca kila mmoja alifurahishwa na mafanikio ya jesca
****************************************************
Siku zilienda hatimaye wasaa wa kujiunga na masomo ya elimu ya juu uliwadia jesca alipangwa kusoma chuo kikuu dar ..es…salaam hii ni kutokana na ufaulu mkubwa alio nao
Jesca alifurahi sana kwake yeye kusoma jijini dar ilikua ni jambo la heshima sana.Ilipofika siku ya kuwasili chuoni jesca alijiaandaa vyema tayari kwa ajili ya kuanza maisha mapya chuoni
Jesca alifika chuoni maisha ya chuo yalimwendea kwa ugumu sana katika siku zile alizokuwa pale hii ni kutokana na kutopata mkopo ambao hutolewaga na serikali kwa wanachuo
Jesca aliishi kwa shida sana kitendo cha yeye kukosa mkopo kilimnyima raha sana marafiki zake wengi walikuwa wakimtia moyo kuwa atapata mkopo kwani mkopo hutoka kwa awamu na ndio kwanza tu awamu ya kwanza.Maneno ya rafiki zake na jesca yalimtia moyo jesca aliamini atafanikiwa tu
********************************************************************************
BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA
Suala la jesca kukosa mkopo lilimnyima sana raha aliwasiliana na wazazi wake nyumbani na kuwaeleza hali halisi pia aliwataarifu wiki ijayo ataanza safari ya kurejea nyumbani hii ni kutokana na hali ngumu chuoni pale na wazazi wake kutokujiweza,mama jesca alisikia uchungu sana ila hakuwa na la kufanya juu ya mwanae alibidi kukubaliana na matokeo

Siku ya jumamosi jesca akiwa anakula katika hoteli ya chuo (kantini) kwa mbali alimwona kijana mmoja akimtazama sana ,jesca alipomwangalia kijana Yule aliachia tabasamu zito sana lililoyaonyesha meno yake yote ,jesca hakuwa na jinsi alibidi na yeye atabasamu,tabasamu la jesca lilimkaribisha kaka Yule na kumpa nguvu ya kusogea karibu kabisa nay eye
``hellow mambow’’
``safi mzima
``mzima kabisa waitwa nani dada angu’’
``naitwa jesca ‘’
``waooo jina zuri kama la mama yangu mdogo ‘’
Kwa aibu jesca alicheka
``hahah sawa bhana vipi wewe waitwa nani’’
``naitwa Solomoni niko chuo mwaka wa tatu sheria ‘’
``sawa nashukuru kukujua ‘’
``asante nami pia samahani lakini’’
``bila samahani’’
``twaweza badilishana namba’’
Solomoni alichukua namba za jesca kisha aliondoka maeneo yale
Jesca alibaki mwenyewe na kujiuliza ``duuuuuh hivi mimi nikoje fasta hivyo nampa mtu namba kwanza ananitakia nini huyu daaaah’’
Upande wa pili solomoni alikuwa akimwaza sana jesca maishani mwake hakuwai kumwona mwanamke mzuri kama Yule taratibu alijisemea ``huyu lazima awe wangu kama ni hela ipo nini kitanishinda mie khaaaa’’
Solomon alipofika mbele kidogo na chuo aliingia ndani ya gari yake kisha alichukua simu yake na kumpigia jesca
``hellow ‘’
``hellow nani???’’
``solo hapa ‘’
``ndio nani’’
Simu ilikatwa na jesca
Khaaaa huyu vipi mbona kakata ,kwa haraka Solomon alichukua simu yake na kuandika meseji kwa jesca ``hellow mumy tumeongea sasa hivi jamani ukanipa namba umenisahau ‘’
Ndani ya dakika tatu jesca alijibu ``ohoooo kumbe ni wewe ok piga ‘’
Solomon alichukua simu na kumpigia jesca
``hellow sory solo ‘’
``usijali uko wapi jesca ‘’
``nipo geti la mbele la chuo ‘’
``ok basi ngoja nakupitia na gari hapo natamani tuzungumze ‘’
``mhhh sawa ‘’
Jesca akiwa anashangaa alimwona solomoni akiwa na gari la kifahari sana solomoni akiwa kwa mbele kidogo alimnyooshea jesca mkono ishara ya kumwita
Jesca alimfuata ,solomoni alifungua mlango wa gari na kuingia kisha kuketi pembeni
Solomoni alimwanza jesca
``vipi mrembo ‘’
``mhhh solo toka lini mimi nikawa mrembo jamani’’
``ndio wewe mrembo yaan umeziteka akili zangu ndani ya masaa machache kabisa ‘’
``mhhh sawa bhana’’
Kitendo cha solomoni kumjia jesca na gari kilimchanganya sana jesca ,jesca alijikuta akimkubali sana solomoni hii ni kutokana na mwonekano wa kitajiri pia gari alilokuwa nalo
``sasa mumy wewe chuoni unaishi hostel au umepanga ‘’
``nipo hostel best’’
``mhhh kwanini hujapanga ‘’
``hela ndio tabu kwanza wiki ijayo narejea nyumbani kwani sina uwezo mie mkopo sijapewa daaah’’
``mhhh pole sana huwezi rudi usijali ‘’
Solomon alipomaliza kuongea na jesca alimpatia sh laki tatu kama matumizi .Jesca alipokea hela zile kwa kutetemeka maishani mwake hajawahi kushika hela kubwa kama ile kweli lilikuwa jambo la kushangaza
Jesca alimwaga solomoni kisha aliondoka sehemu ile huku akiwa haamini kilichomtokea aliona ni kama ndoto tu
Upande wa pili solomoni alibaki akimkata jicho la huba mtoto mrembo jesca ,alivyokuwa akitembea mwili wake wote ulitingishika jambo ambalo liliziamsha hisia za solomoni shauku yake kuwa na jesca ilizidi ,ama kweli siyo shepu tu hata sura yake pia ilivutia sana
Je nini kitaendelea
ITAENDELEA HAPA

WAWEZA IPATA YOTE WASILIANA NAMI WHATSAPP 0713111547
 
Back
Top Bottom