Mwalimu Nyerere alitaka Tanzania ijitegemee, Mwinyi alitaka ubepari wenye kulinda tunu za kitanzania, Mkapa alisimamia uchumi unategemea uwekezaji na ubinafsishaji, Kikwete alisimamia Tanzania yenye demokrasia ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, sasa Magufuli anasimamia falsafa gani? nauliza hivi kwa sababu hotuba yake yote alitoa maono bila mikakati, sana sana alipoint out mapungufu na kusema atayarekebisha, ila hajaweka wazi msimamo wake kifalsafa, kubana matumizi siyo falsafa ni udhibiti wa fedha za umma, ukibana matumizi bila kuwa na mawazo ya kuzitumia hizo ela basi zitaliwa na mchwa, nadhani bado Magufuli hajajipambanua kifalsafa, bali ametaja matamanio yake anavyotaka Tanzania iwe.