Kifa ng'ong'o: mchezo wa kifo

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,784
Reaction score
6,183
KIFA NG’ONG’O-MCHEZO WA KIFO
Nakumbuka wakati nikiwa bado mdogo tulikuwa tunacheza mchezo uitwao “kifa ng’ong’o”. Mchezo huu ulifanywa kwa makusudi maalum ya kuonyesha ukakamavu na uhodari pamoja na kuvumilia adha mbali mbali..

Kwanza mchezo huu unafanywa na mtoto mmoja ambaye anajitolea “kufa” kwa muda na wenzake (sisi) huanza kumtekenya au kumshika shika na endapo atacheka ama kufumbua macho basi ameshindwa mchezo na ilimpasa mwingine aingie, Hata hivyo kama ilivyo michezo mingine, mchezo huu pia ulikuwa na maexpati wake…

Nakumbuka kulikuwa na dada mmoja ambaye alikua akiamua kufa ng’ong’o anakufa kweli! Yaani ilifikia hatua na sisi tukaanza kulia kweli, maana kila njia tuliyojaribu kumfanyia hakuamka wala kujitingisha! Ndipo vilio vilizidi mpaka watu wazima wakatukuta pale na si sisi wala “aliyekufa” wote tulichezea fimbo, zaidi ya hayo tulionywa tusijaribu tena mchezo huo hata mara moja…

Wakati mwingine wale maexpati walitumia kifa ng’ong’o kama njia ya kujilinda na adhabu shuleni , nakumbuka kipindi Fulani alikuja mwalimu mgeni shuleni na akamchapa mmojawapo wa “wafa ngo’ngo” na akafa saa ile ile, mwalimu Yule alihaha na ikafikia akawa anampigia magoti kumbembeleza aamke lakini hakuamka!

Hadi kengele ya kuruhusiwa bado hakukuwa na dalili za kuamka! Ikabidi amwagiwe maji lakini bado! Ndipo akabebwa kupelekwa hospitali kwa gharama za mwalimu! Na mwalimu Yule sikumbuki kama alishawahi kumchapa tena!

Hata hivyo katika mchezo huu wapo wengine ambao hatukuweza kabisa kufa ng’ong’o yaani ilikuwa ni vichekesho kwani hatukuweza kuvumilia kabisa kutekenywa, kushikwa ama kumwagiwa maji!

Nimekumbuka hadithi hii baada ya kilio kikubwa cha wafanyakazi kuhusu mishahara yao na stahiki mbali mbali, wakati hayo yakitokea serikali na TUCTA, zimekufa ng’ong’o hakuna hata mmoja ambaye anahusika na kusikia kelele hizi, pamoja na kutekenywa, kumwagiwa maji, mabango n.k bado imekufa ng’ong’o

........
nawatakia jumatatu njema
 
Ha ha ha ha.. Story yako Mkuu imeendana na hitimisho lako.. Bahati mbaya kwa wafanyakazi wa Tanzania, viongozi wao ni wanasiasa hata kama hawajionyeshi mubashara, lakini tunaona kwa matendo na kauli zao.. Juzi nimeona Waziri mkuu amekuwa quoted akisema mfanyakazi yeyote wa serikali anaeona mshahara haumtoshi atoke akatafute maslahi kwingine.. Kama ni kweli alitoa kauli hii, halafu vyama vya wafanyakazi vimekaa kimya, kauli yako ya kufa ng'ng'o inazidi kupata nguvu..
 
hicho ndio kifa ng'ong'o mkuu
 
Umenikumbusha kipindi niko shule mkuu niliitumia sana hii mbinu na nilikua salama na viboko.
 
Tucta wako kwa ajili ya kula michango ya wanachama na sio kutetea wanachama tena jamani! hela zetu tunakatwa zinaliwa na wezi tucta! Itangazwe kuwa wafanyakazi wanaotaka wanaweza kujitoa uone kama kuna ambae atabaki ndani ya dhuluma hii ya tucta!
 

Umewasahau hao 'WAFA Ng'ong'o" wanakadi za mtaa wa Lumumba?
 
Asante allan kwa kuiandika habari katika mvuto na ufasaha mkubwa.
Umeonesha busara nzuri kwenye mada yako.

Kipindi hiki mambo mengi yamekufa ng'ong'o.

Hadi CUF nao wamekufa ng'ong'o.

Ni kipindi kigumu cha mpito kuelekea katika, ama mafanikio au maangukio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…