LWENYI
JF-Expert Member
- Jul 4, 2013
- 1,839
- 2,175
Salamu ndugu zangu wana jamvi.
Nianze kwa kusema Ee Mungu niepushe na pepo la General Galadudu
Niende moja kwa moja kwenye maada, ni hivi.
Kwa muda mrefu nimekua nikitafuta mtu tunayeendana kwa ajili ya kuanzisha naye mahusiano na kuandaana kwa ajili ya ndoa na ni ukweli kwamba nimekua muangalifu kwa kiasi kikubwa tu kwakua mimi naamini katika ule msemo wa kawia ufike.
Sasa katika pitapita zangu na majukumu ya hapa na pale nilifanikiwa kwenda mkoa fulani kwa ajili ya project fulani na sikuwa peke yangu bali team ya watu 13 wadada 7 na wanaume 6 nilipokutana na wana team Wenzangu nilikua muangalifu sana kwa kuwa sikutaka kujiingiza kwenye mazoea mabaya na mtu yeyote hii ni baada ya kujipa likizo ya mahusiano kwa muda.
Baadae kidogo teammate walianza kuzoeana na kutaniana na mimi nikawa naenda nao vizuri tu ila kuna watu walianza kumechisha watu nadhani mnafahamu matani huwa yapo tu. Basi ghafla na mimi nikabambikwa mate wangu hapo wakaanza kumuita Mrs mimi
Sasa mimi najua tabia za matani ukiwa mkali ndipo unataniwa zaidi hivyo basi kuua so na mimi nikawa nachagiza kwa mbwembwe kwa kumtania muhusika mwenzangu, lakini sikuwahi kuwa na interest naye kabisa.
Basi kadri siku zilivyoenda ndivyo tulivyokuwa tukiendelea kuzoeana na kutaniana muda mchache baadae akaja member mpya kwenye team yetu kwakweli mtu huyu nilipomuona tu siku ya kwanza nilimuelewa sana she is black, cute, humble mbali na yote hayo pamoja na kwamba alifika usiku kesho yake asubuh nilishangaa kumuona kanisani nikavutiwa sana, kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo nilivyozidi kugundua mambo mapya ya ndoto zangu kutoka kwake mara tukaanza kuzoeana na kuwa marafiki
Kumbuka teammate bado wananitania na huyu dada mwingine, huyu dada mpya alinifanyia kitu ambacho sitakuja kukisahau siku nilipoumwa tangu siku hiyo nikajiapiza kwamba kama nitaoa siku moja basi Mungu na anipe yeye kuwa mke wangu. Tangu hapo nikaanza kuwa karibu naye na nikagundua pia anapenda kuwa karibu na mimi muda mwingi ambao tuko free.!
Kumbe nyuma ya pazia alimfuata huyu dada wa kwanza ambaye nataniana naye akamuuliza dada X eti ni kweli una mahusiano na LWENYI? Dada X akawa mkweli na kunikana lakini akagundua kwamba dada Z anataka kufanya kweli, ooh God.
Tangu hapo akaanza kubadili gia angani akaanza kunifanyia vitu tofauti na mwanzo mbaya zaidi akaanza mashindano na huyu mgeni Z na akaenda mbali zaidi na kuja kuniamba live kwamba ananitaka.
Roho inaniuma najihisi nisiye na bahati najiona mtu nisiye na future kwakua hii sasa ilianza kuwa ligi kati ya wawili hawa ubaya huyu mgeni hawezi battle na aliwahi kuondoka kabla yetu hivyo tukabaki na huyu mwingine X
Siisahau siku ambayo Z aliniambia wazi kwamba walikua wakishindana na x kunipata hii ni baada ya kumgusia mawili matatu kuhusu ninayojisikia juu yake siku hii ilikua ni siku ambayo X alishinda room kwangu kwa Muda mrefu sana, kadri siku zilivyoenda X akawa ananishawishi mpaka ilifika siku uzalendo ukanishinda nikafanya yale ya General Galadudu nafsi inaniuma sana sikuwahi kutaka iwe hivyo baada ta hayo akaanza juhudi za kutaka teammate wote wajue natoka naye ooooh noooo, nimejitahidi sana kuzuia ila nahisi wameshahisi kitu.
Sijapata mrejesho wa mgeni Z kama zishamfikia hizi Mungu anisaidie nipate cha kujitetea kwakua huyu ni mwanamke wa ndoto yangu tunaenda sawa kwenye vitu vingi sana ni mwanamke niliyemsubiri kwa zaidi ya miaka mi3 baada ya kuvunja mahusiano yangu yaliyopita sitaki ifike miaka mi 2 zaidi bila kujua nani nitatengeneza naye familia ilhali tayari Mungu aliniletea mbele ya Macho yangu
Nichukue fursa hii kumuomba Mungu anisamehe na wanajamvi mnishauri
Wenu katika mapenzi.