Kidogo amgandamize mama wa mpangaji mwenzake

Kidogo amgandamize mama wa mpangaji mwenzake

BatteryLow

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Posts
446
Reaction score
149
Jamaa yangu huyu ni mtundu sana toka tunasoma sekondari. Juzi hapa amezua balaa nyumbani kwake na hana amani hadi leo hivi. Kisa chenyewe ni hivi: Jamaa yangu anaishi nyumba ya kupanga, self. Fence ni block lakini ukuta mmoja umejengwa vyumba vi 4 vya single. Single moja anaishi chalii mmoja na mke wake na hawajajaliwa mtoto. Mama yake huyo chalii anapokuja kumsalimia kijana wake huwa anaombewa sehemu ya kulala kwa yule rafiki yangu mtundu. Sasa sikiliza vizuri alivyoharibu. Huyu mtundu kumbe anachepuka na h/girl wake humo humo ndani ya li self. Siku moja mke wa jamaa hayupo, mpangaji chalii mama yake kaja, jioni kaandaliwa chumba cha kulala kwa huyu mtundu. H/girl bwana akampeleka yule mama wa watu kwenye kile chumba anacholala yeye kwa kuwa kilikuwa kisafi kwavile kinatumika kila siku, yeye akenda kulala kingine kilichokuwa hakitumiki kila siku. Jamaa anarudi usiku ameshatwika viroba vya kutosha ni direct hadi room ya h/girl, akapanda kitandani, kanyanyua shuka kajikunjia humo ndani kamkumbatia mama wa watu kisawasawa na mguu kampandishia kiunoni. Mama wa watu acha apige kelele, "wewe baba niache utaniua na hivi nilivo mbovu!" Jamaa alitoka nduki akaenda chumbani kwake na hakuwa na amani hadi leo.
 
Na wewe ulikuwa wapi..umesimulia kama ulikuwemo kabisa au its you?
 
Weka picha!

akina shigongo hawakuwepo kwani?
 
Ni rafiki yangu aliniomba ushauri afanyeje, nikamwambia kauka kama hakuna kilichotokea kwa sababu yule maza hawezi kusema kwani atakuwa amejiaibisha , na kweli hadi leo haijasikika na yule maza alisharudi kijiji longi na yule mpangaji na kidemu chake walishahama.
Na wewe ulikuwa wapi..umesimulia kama ulikuwemo kabisa au its you?
 
Ni rafiki yangu aliniomba ushauri afanyeje, nikamwambia kauka kama hakuna kilichotokea kwa sababu yule maza hawezi kusema kwani atakuwa amejiaibisha , na kweli hadi leo haijasikika na yule maza alisharudi kijiji longi na yule mpangaji na kidemu chake walishahama.

kama walishahama ye hana aman ya nini mbona maelezo yanakinzana
 
Hiyo stori mbona ya zamani saaaaaaaaana. Lete nyingine hapo hamna kitu.
 
Back
Top Bottom