KICHERE :MENEJA WA TRA ATAKAYEFUNGA BIASHARA YA MLIPA KODI KUKIONA

KICHERE :MENEJA WA TRA ATAKAYEFUNGA BIASHARA YA MLIPA KODI KUKIONA

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Kamishna Mkuu wa Kodi Nchini, Charles Kichere amewaagiza Mameneja wake wa TRA Nchini kutofunga Biashara ya Mfanyabiashara kwa sababu ya kutolipa ama kulimbikiza kodi na kudai atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa hatua Kali juu yake.

Kichere amesema hayo katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo kimojawapo cha Television Nchini na kusema kuwa zipo njia mbadala za kukutana na Mfanyabiashara na kukubaliana naye jinsi ya kulipa kodi kuliko kumfungia Biashara yake.

"Mimi naumia sana kuona Biashara zikifungwa sababu ya kodi kwani unapomfungia Mfanyabiashara unakosa hata kile kidogo hivyo nimewaagiza mameneja wangu kutofunga Biashara Bali wafanye mazungumzi na wafanyabiashara jinsi ya kulipana"
 
Naona sasa ameamua kukwepa lawama , anajikosha tu. Watu wengi wamefungiwa biashara zao anakuja kusema hayo baada ya kuona mheshimiwa rais katoa neno? siku zote weledi unatakiwa utamalaki sio kutumia ubabe na ndio matokeo yake biashara zimeshafungwa. Hii ni sawa na kukumbuka shuka hali kumeshakucha ...
 
Umuhimu wa wafanya biashara baada ya Miaka 3 ndio unaanza kuonekana sasa, kina Yusuph Manji na Matajiri wengine walishafunga biashara zao na watanzania wenzetu kibao wamesharudishwa majumbani.
 
Mmechelewa amka....watu hawawaamini tena
 
Back
Top Bottom