Ukweli Unaponya
Member
- Mar 14, 2013
- 12
- 10
Kisa cha kweli..
Tayari kwa kulazimishwa nimekuwa yatima,nilikuwa kwenye msiba wa rafiki yangu mkubwa Mama yangu.ALIPIGANIA maisha yake vya kutosha lakini ugonjwa wa kansa ya matiti ukamshinda nguvu na kumuua na hakuna cha kufanya.
Moyo wangu ulikuwa unauma sana na mara kadhaa nilishindwa kupua vizuri,nakumbuka siku nilipotoka chuo kwenda kumuona mama hospitali,alikua anaumwa sana lakini tabasamu lake usoni liling'aa kama mwezi mwangavu akicheka na kunichekesha lakini akinisisitiza kusoma kwa bidii kuwa na hekma, busara na upendo kwa wakati wote wa maisha yangu.
Nilimsogelea mama kitandani alipokua amelala nikamwambia 'Mama nakupenda sana nataka bado kuishi na wewe usiniache peke yangu please'' ' Mama huku akicheka akaniambia sitakuacha peke yako mwanangu rudi chuo kesho tutaonana tena'' inauma sana kwani hiyo ndiyo siku ya mwisho kuongea na mama yangu kipenzi wakati huo mama ndie alikua ngome yangu kwani baba alikua amekwisha fariki miaka miwili iliyopita.
Nilikuwa namebaki na dada yangu ambae alikua na mtoto mchanga wa miezi miwili na kaka yangu mambae nae ndo kwanza kafunga ndoa wiki moja iliyopita.
Tukiwa kanisani,niliinua macho yangu nikamtazama kaka yangu pembeni sura yake imejaa simanzi mkono wake wa kuume amemshika mke wake,kisha nikamuangalia dada yangu kaweka kichwa chake mabegani mwa mume wake ambae mikono yake ilikuwa imeshika mtoto mchanga kabisa,harafu nikaangalia msaraba uliokuwa umeandikwa ''MAGRETHY'' jina la mama yangu na jeneza lilokuwa mbele yangu... hapana! sikuwa naamini kama kabisa kuwa mama katuacha na hatuko nae tena.
Mara kwa mshangao nikasikia mtu ananishika bega,nikageuka haraka kumtazama nikaona sura ya mwana dada mzuri na mlembo sana akaniambia..''Pole sana Rick,hata mimi mwaka jana nilimpoteza mama yangu kwa ugonjwa huu'' kisha akanikumbatia na kusimama nyuma yangu,nilishangaa sana,sikuwa namjua lakini yeye alionekana kunifamu vizuri
Baada ya misa,tulianza safari ya kwenda makaburini,ndugu,jamaa,marafiki,majirani na watu mbalimbali waliuwa nasi wakitufariji na kutoa mchango wa hali na mali nilishangazwa sana na upendo waliotuonyesha,wanachuo wenzangu na walimu hawakuwa nyuma wote walikuwa pamoja na mimi.
Wakati mgumu na mbaya kwangu ulikuwa ule wakati wa kuondoka baada ya kumaliza mazishi,nilishindwa kuondoka pale kaburini na kumuacha mama peke yake nililia sana sana,nikamulilia Mungu afanye muujiza wa kumfufu mama yangu lakini wapi.. haikuwezekana.
Nikiwa nimeinamia kaburi la mama nilikuwa imezungukwa na watu wengi ngugu zangu,kaka na dada,marafiki na wanachuo wenzangu,mara yule dada(mrembo alinistukiza kanisani) akatokea katikati yao,akaniamusha, akachukua kitambaa chake safi akanifuta machozi yaliyokuwa yakitililika kama maji akanikmbatia huku akinibembeleza kwa sauti ya upole na maneno yenye nguvu za ajabu akaniongoza hadi kwenye gari kurudi nyumbani.
Tulifika nyumbani na mambo ya msiba yaliendelea,baadae ilibidi nimuulize yule dada wewe ni nani na ulinifahamu lini? akajibu..'mimi naitwa MERRY nilikufahamu wakati unakuja kumuona mama yako hospitali,mimi na mama tulikuwa tunafahamiana mama yako alikuwa anamtembelea mama yangu wakati anaumwa na kila alipokuja nymbani alinikuta na hata baada ya mama kufariki mama yako aliendelea kunotembelea na kunijulia hali,alikuwa mtu mwema kwangu'' aliniambia menge sana na akaanza kulia...
Hata hivyo yote kwa yote,tulijipa moyo na Mungu alitupa nguvu katika wakati wa kipindi chote kigumu na kikubwa zaidi kuliko vyoote kwa sasa mimi Rick na Merry ni wachumba tunapendana sana tunatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
Nafikiri pamoja na mambo mengine MERRY ni zawadi kutoka kwa mama yangu na aliposema ''sitakuacha mwenyewe mwanangu'' alimanisha,na kweli hajaniacha peke yangu kaniacha na Merry kipenzi changu.Nampenda sana Merry na yeye ananipenda,Mungu tupe uzima na nguvu.
PUMZIKA KWA AMANI MAGRETHY...
PUMZIKA KWA AMANI MAMA YANGU MPENDWA...NAKUPENDA SANA.
Your son Rick..
LIKE & SHERE & COMMENT kuonyesha heshima na upendo.