Kichefuchefu katika mafanikio ya serikali ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kichefuchefu katika mafanikio ya serikali ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jingalao, Sep 28, 2012.

 1. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,389
  Likes Received: 10,563
  Trophy Points: 280
  Namuangalia mheshimiwa sana John Pombe Magufuli akijipambanua kwa kutuhabarisha juu ya miradi ya barabara inayoendelea kutekelezwa jijini Dar na kwengineko nchini.

  Ni ukweli usiopingika kuwa kwa kiwango kikubwa serikali ya awamu ya nne imefanikiwa sana katika kufanikisha ujenzi wa mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami.

  KICHEFUCHEFU NI HIKI HAPA...

  Katika miradi yote alitotaja Magufuli nimesikitishwa sana kusikia miradi yote ni kwa misaada ya wahisani kama vile world bank,USA, Japan, Korea n.k

  Hii inamaanisha serikali yetu imeshindwa kutumia RASILIMALI tulizonazo kujenga hayo 'mabarabara'

  Ukienda kwenye sekta nyingine kama afya, kilimo au elimu utakuta hali ni hiyo hiyo tu, mambo yote ni kwa msaada wa watu wa nje.

  Pamoja na maendeleo tunayoyaona lakini inatia kinyaa kuona hatuna tulilolifanya kwa nguvu zetu wenyewe.

  Ni lini tutasikia mafanikio ya nchi yetu kutokana na rasilimali zetu?


  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 2. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Unashangaa nini? hii ndio Tanzania. kila bajeti inaposomwa utaona matumizi yanazidi mapato.kwahiyo kila mwaka ni lazimz eidha kwenda kukopa ili kubalance mambo. hakuna wakati tulipo zalisha ZIADA.Je. kuna matumaini ya kuondokana na umasikini kama kila mwaka unatumia zaidi ya ulivyo zalisha??? kwetu sisi kitu kama kubana matumizi,kuongeza uzalishaji ni vitu tusivyo vitumia ili kufikia mafanikio. tunadhani wajomba watatuletea kila kitu pamoja na maendeleleo. FIKRIA KIDOGO, Una familia lakini kila upatapo mshahara unatumia wote na unakopa kido ili mwezi uishe,je kutakuwa na matumaini famila hii kuondokana na umasikini??
   
 3. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,917
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Pointi nzuri, lakini unasahau kuwa hata kukua kwa CHADEMA ni kwa hisani ya CDU (Christian Democratic Union) cha Ujerumani.
  Lakini nyie hamjengi barabara wala zahanati kwa wananchi.
  Hii inatia kichefu chefu zaidi.
   
 4. h

  holypotato Senior Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 107
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  inachoweza sirikali yetu sikivu ya sisiem ni kununua ma vx-v8 na kulipana maposho mazuri kwa rasilimali zetu... Ila si kwa miradi ya maendeleo...
   
 5. h

  holypotato Senior Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 107
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kuna mkuu wa IMF na wataalam wengi walitoa warning kuwa ni hatari mnapofikia mahali mnakopa for recurrent expenditure.... Ila mazuzu yetu yanasema kukopa sio tatizo!! The future might be very tough...
   
 6. D

  Deofm JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tiachane na siasa, turudi kwenye uchumi, Hivi hizo kodi zinazokusanywa kwa mabilioni kwa mwezi huwa zinafanyia nini? Hii hali tutaendelea nayo hadi lini? bila kujali ni chama gani kinatawala: je kwa hali hii tunaweza kusimama mahali popote tukasema kuwa Tz ni chi huru?
   
 7. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,917
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Kodi inayokusanywa wala haitosheezi matumizi yetu kama Taifa.
  Tunakula kwa ziada kuliko tunavyozalisha wenyewe, pengo la matumizi ndio tunaomba omba kwa wageni ili watunusuru.
  Hilo nakiri ni tatizo kubwa na si tatizo linaloweza kutatuliwa na mtu yeyote katika muda wa miaka mitano au kumi.

  Serikali ya CCM haijaweza kutatua taizo hili katika miaka iliyokaa madarakani,sembuse majigambo ya CDM kuwa itataua matatizo yote ikipata madaraka.

  Serikali yoyote itakuta matatizo yale yale ya umasikini, njaa, magonjwa, dhuluma(kutokana na ukosefu wa haki).
  Hayo ni ya msingi kabisa ambayo ilani ya CCM imeyaweka mbele, lakini utekelezaji wake ni mgumu.
  Tukienda kukamia maendeleo hapo sasa ndo hata chenji hatuna.

  CDM kwa kulinganisha haijaweka wazi mipango yake ya kuondoa umasikini ,ujinga, na magonjwa kitaifa, ikiwa ni pamoja na kuondoa dhuluma.
  Wamejaa lawama tele kwa chama tawala, kitu ambacho kila mtu mwenye uwezo wa kuongea anaweza.

  Mipango ya maendeleo kitaifa ndio haieleweki, kile tulichosikia cha sera ya majimbo hakina kichwa wala miguu kitaifa.

  Ati wapewe nchi, just for the fun of it.
   
 8. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wivu tuuu
   
 9. D

  Deofm JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wewe hueleweki, kwa kuwa ni mwana siasa tena kada wa ccm. kama unaona ccm na cdm hawana sera za maana kwanini usizungumzie vyama vingine, kwani tz tunavyo vyama zaidi ya18, mbona huzungumzii hivyo vingine? mtazamo wangu ni kuwa hatuwezi kupata maendeleo bila kuwa na viongozi wenye mtazamo wa taifa kwanza mimi baadae, nadhani tungebadilika na kila mmoja akaanzia pale alipo, kama kiongozi anafanya jambo la kudhalilisha taifa wate tumzomee kwa pamoja bila kujali ni mwezetu au la. hapo kila mmoja ataogopa kuwa fisadi, lakini kama mtu anaiba na ushahidi upo, anavuliwa tu madaraka na kifungo feki kama cha liumba, hakuna atakaeogopa kuchukua fedha atakapopewa dhamana ya kuzilinda, kwani nikichukua bilioni 50, halafu nikafungwa mwaka mmoja nina shida gani nikirudi naanza kutumbua pesa zangu bila tatizo. kwa hilo naomba utafakari, kama wewe ni mmoja wao basi nakuomba utuonee huruma sisi watanzania wenzako.
   
 10. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Hiyo haitapendwa humu jamvini kwani wapenzi wengi wa chadema jamvini wamedevelop a 'holier than thou' attitude
   
 11. HAMIS MOHAMED

  HAMIS MOHAMED JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  uwe CUF,CHADEMA,CCM,TLP,NCCR,TADEA au UDP, ukweli unabaki palepale kama nchi tunakopa zaidi ya tunavyoweza kurudisha ni UTATA.
   
 12. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Well said Junior! you see things more clearly than some members here. May be it due to your residing up at the highest peak dar and can see tomorrow clearer than most
   
 13. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,917
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Hao ambao wamedevelop a "Holier than thou" attitude have never been thinkers and probably will never be.
   
 14. Jilanga

  Jilanga JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  TANZANIA NI NCHI HURU, LAKINI HAINA VIONGOZI BALI WATALA! Nyerere alisisitiza sana juu ya watawala wasiozingatia sheria ndio chanzo cha uozo wote! Tafiti zaonyesha miaka michache ijayo hali itakuwa mbaya zaidi kutoka na shiling kupungua thamani, kutokuwa na hakika ya ajira, kupanda mfumko wa bei n.k!
   
 15. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2013
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,389
  Likes Received: 10,563
  Trophy Points: 280
  nashangaa kuwaona wapibzani wakisifia serikali kuhusu wizara ya bw magufuli bila kuhoji madeni yanayoliangamiza taifa!

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 16. SirChief

  SirChief JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2017
  Joined: Jun 23, 2014
  Messages: 1,705
  Likes Received: 923
  Trophy Points: 280
  Chadema wanakusanya kodi nchi hii?,Hao CCM wanatumia hela za wahisani kujenga barabara au ni kodi zetu?.Mbulula kama hizi za lumumba zipo nyingi sana nchi hii,No wonder tumefika hapa tulipo.
   
 17. SirChief

  SirChief JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2017
  Joined: Jun 23, 2014
  Messages: 1,705
  Likes Received: 923
  Trophy Points: 280
  Kwo wewe kwa akili zako hizo umeona ni point ya msingi sana hiyo?,hahahaha aise no wonde CCM inapendwa na vilaza,Hebu nikuulize,ile misaada ya wahisani huwa mnatumia kujenga haspitali/ barabara au mnatumia kulipana posho na kuhonga watu?...CDM wanakusanya kodi nchi hii?.Mnakuwa wajinga hadi kufikiri
   
 18. jos black

  jos black Member

  #18
  Aug 19, 2017
  Joined: Aug 9, 2017
  Messages: 24
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 5
  Inatakiwa uelewe ni mambo gani yamefanywa kwa msaada na mambo gani yamefanywa kwa rasilimali zetu ni kweli kuna mambo mengi yamefanywa kwa msaada lkn sio yote ndugu mengine ni rasilimali zetu zimetumika.
   
 19. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2017
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kwanini usianze na kuulizia enzi za mwalimu[TZ ilikuwa inapata misaada mingi], Mzee Mwinyi, Mzee Ben na JK. Mbona mnamsakama sana JPM kwa hili?
   
 20. The Proudly African

  The Proudly African Senior Member

  #20
  Aug 19, 2017
  Joined: Jun 22, 2017
  Messages: 140
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
Loading...