Kichaka cha mwongozo wa speaker

Kwaroz

Member
Aug 30, 2009
55
10
kwa siku zakaribuni watanzania wengi hawajafurahishwa na mambo yanayoendelea ndani ya bunge nami nikiwa mmoja wao. Jambo hili linaendelea kuzidi, kusimamiwa na kuasisiwa na speaker au muongozo mbunge ndani ya siku husika. kitukinachoonekana kuwa kinahasisiwa na CCM kwa kuwa wao wapo wengi bungeni na inaonyesha kwamba CCm wamekuja na mpango huo ili kuonyesha kwamba wapinzani wanaleta fujo, hawafati kanuni ndani ya bunge na hawafai kuwa wabunge.

lakini cha ajabu ni kwamba watanzania wanapokea mambo hayo kwa kinyume na kile wabunge wa CCM wanavyofikilia kuwa wameeleweka au wamefanikiwa kwa hilo. mbinu hizo za CCm inaonekana dhahiri kuwa inawajenga wapinzani kwa kuwa wanazungumza mambo ya msingi na yale yanayowagusa watanzania wa kawaida na maisha yao kwa ujumla.

kwa mtazamo wangu ni afadhali wanaoongoza bunge wangesimamia kweye kanuni kulikoni hivi sasa anaamua kwa shinikizo la walio wengi mpaka anashindwa kutimiza wajibu wake ndani ya bunge. kichako hicho cha mwongozo wa speaker kinawapa nafasi wapinzani kuwa mashujaa wa taifa kwa bunge la 2011/2012 kwa kuonyesha umahiri wao. zifuatazo ni baadhi ya kauli zilizotaka kupatiwa muongozo lakini mpaka sasa miongozo hiyo haijahitimishwa ndani ya bunge;
1. Godless Lema - Waziri Mkuu kadanganya bunge
2. Tundu Lissu - Waziri kadanganya bunge
3. Mch. Msingwa - Msafara wa magari ya waziri mkuu
mingine unaweza kuongezea maana kila siku kuna jipya

CHANGAMOTO/MCHAKATO
kupitia mapito hayo utaratibu huo unatoa mafunzo yafuatayo kwa watanzania
1. wanapata picha na uelewa wa kutosha aina ya wabunge waliowachagua
2. wanaelewa taratibu kanuni za bunge
3. bunge linaamsha hali ya watanzania kudai na kupigania haki zao
4. bunge limekuwa ni mwanzo wa mapambano ya kifikra na kuondoa uoga wa kudadisi mambo hadharani bila woga
5. bunge kuwa sehemu ya mchakato wa awali katika kupigania kuipata Tanzania wanayohiitaji na mengine mengi tunaweza yataja

Hizi ni fikra haziitaji mtu kukurupuka katika kujibu, kuna wakati najiuliza hizi hawa wabunge huwa wanakaa chini ni kutafakari wanachokifanya au noi bora liende siku ipite nipate sitting allowance?
 
Kwa hali ilivyo sasa hivi ni kama zaidi ya majimbo yaliyo chini ya ccm yako wazi. Wabunge wa ccm watakuwa wachache sana 2015. Wamekuwa mabubu/waoga kutetea wapiga kura wao.
 
Back
Top Bottom