tryphone005
JF-Expert Member
- Jan 30, 2017
- 453
- 507
Nakumbuka nilikuwa naishi maeneo ya ununio, ni maeneo yenye bar za ufukweni na shughuli za uvuvi nyingi,
Nilikuwa na tabia ya kwenda ufukweni nyakati za usiku kuanzia saa moja, karibu na bar, ili kupunga hewa ya jioni. Nakumbuka kuna siku nilikuwa maeneo hayo ila kwa mbali kabla sijafika eneo langu, kagiza giza nikaona mtu kwa mbali mfupi mwenye kichwa kikubwa wastani, nilistuka nafsini, nikajua yule sio mtu ni kibwengo, kabla sijaamua kukimbia pale, alifika nilipo kwa speed ya ajabu na kunitazama sana huku akinipita kwa kasi nisijue la kufanya, alipotokomea ndipo akili ikanijia, nikaondoka kurudi kwangu!
Kesho yake nikaanza kupata matatizo ya kuona maruweruwe na kupata mikosi midogomidogo nikajua shughuli ishaanza.
Nikaenda kwa mtaalamu mmoja, akafanya mambo yake na kisha akanipa dawa fulani ya kuchoma na kunifundisha kawimbo eti ntakuwa nakaimba kila nikihisi kibwengo analeta maruweruwe, nikaona hii nayo kali sasa, nianze kumuimbia kibwengo tena! Nikagoma kumuimbia kibwengo! Siku iliyofuata nikajisalimisha kanisa fulani kwa mchungaji fulani wa kiroho, nikapata maombi na msaada wa kiroho, ile hali ikatoweka, nikakoma tangu siku ile kwenda ufukweni mida ya giza, SITAKI KUMUIMBIA KIBWENGO TENA!