Dahafrazeril
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,500
- 2,056
Sabalkheri wana JamiiForums !
Nimeanzisha uzi wangu kwa kusaili na nitamalizia kwa kusaili.Kusaili ni kuuliza maswali ya msingi.Binadamu yeyote mwenye ufahamu na Fikra angavu ni sharti asaili kila anachokiona, anachokisikia, anachokisoma nk.Baada ya hapo anakuwa ameondokana na kile alichokiita Prof Chachage "Collective imbecilization",kwa kiswahili chepesi "Kupumbazwa kihalaiki".
Katika jamii nyingi za Kiafrika hususan hapa nchini ni mara nyingi sana kuwasikia Ndugu, Jamaa na Marafiki wakiisema "Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi,Amen" ,"Rest In Peace" nk haswa pale wanapoondokewa na kipenzi chao.
Sijapata kufahamu kiundani asili ya haya maneno hapo juu.Aidha katika Vitabu mbali mbali vya Kiimani au hata visivyo vya kiimani (Non spiritual Books).
Kimaandiko 'Biblically",Mshahara wa dhambi ni Mauti.Ni toba ya kweli pekee itakayomuondoa mtenda dhambi katika moto wa jehanamu na siyo kingine.Mtenda mema roho yake itakwenda peponi huku mtenda maovu roho yake ikienda Motoni.
Pia,Sisi ni wana wa Mungu.Ni Mungu pekee ndiye hapangiwi cha kufanya na binadamu ila kwa rehema na busara zake pekee ndipo anasikiliza haja zetu na kuturehemu.Msingi wa hoja hii umekuja baada ya Kuisoma kisa cha Lazaro na tajiri (Luka 16:19-31) nakagundua kuwa Mwanadamu ana nafasi pekee ya kuomba sala ya toba na kukiri kiutakatifu na sala zake kusikika pale tu akiwa hai.Akishakufa kunakuwa na ukuta mpana sana kati ya sisi tulio hai na Aliyekufa hivyo uwezekano wa kumuomba Mungu aidha amlaze mahala pema peponi au siyo peponi ni maamuzi yake Mungu na siyo sala zetu.
Swali langu ni hili,Ni kipi kinachotufanya kuyatamka maneno haya?.Ni utamaduni,mazoea au ni kitu gani?.Kama maneno haya hayawezi kubadili chochote ni kwanini tujilishe upepo?.Kwanini tujipe-imani katika kitu kisichokuwa na uhalisia wowote?.
Nb:Wana JamiiForums hatuna budi kujenga utamaduni wa kutoa hoja zetu kwa kutumia mantiki badala ya jazba, na kwa kutumia vichwa badala ya mapafu.Hatari ya kuacha kutumia vichwa ni kwamba tutaingiza katika mijadala yetu mambo ambayo kimsingi hayahusiani kabisa na kile tunachokijadili, na matokeo yake ni madhara makubwa kwa JF.
Asalaam.