mzee wa kijiwe
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 947
- 690
Serikali, Bunge na Mahakama ni mihimili mitatu mikuu au rasmi ya dola!
Kila mhimili umewekwa kwa jinsi ambavyo utakuwa huru kutimiza majukumu yake bila ya kuingiliwa na mhimili mwingine.
Nguvu ya mihimili hii imejificha nyuma ya vyombo rasmi vilivyowekwa ili kuipa mihimili hiyo uwezo na mamlaka ya kutekeleza majukumu yao bila ya vizingiti.
Kwa upande mhimili wa kwanza yaani Serikali, nguvu yake imejifisha kwenye Jeshi la Polisi, hawa ndio waliowekwa kuhakikisha amri halali za serikali hazipuuzzwi na raia. Ukiondoa Jeshi la Polisi serikali ni sawa na mkusanyiko usio na nguvu yeyote.
Jeshi la wananchi yaani JKT au JW, sii Mali ya mhimili huu, hili ni Mali ya dola nzima na sii serikali tuu. Na ndio maana wengi hushindwa kutofautisha Kati ya Polisi na Jeshi. Kwa kifupi IGP hana Uhuru mpana kwenye kutekeleza amri za serikali wakati ambapo Mkuu wa Majeshi anaupana wa kuhoji na kukataa amri zisizo sawa toka serikalini.
Nguvu au kiburi cha Mahakama ni Magereza, ukiondoa magereza mahakimu, majaji watabaki wanacheza ngoma ya kitoto. Kila MTU anaogopa kufungwa, hata watawala. Kushikwa na Polisi sii jambo la kushitua na kwa wasomi wa sheria wengi hulidharau Jeshi la Polisi kwakuwa wanajua nguvu yao kisheria ni ndogo sana, wanakamata wanakuhifadhi na wanqkukabidhi kwa mhimili huu wa pili, yaani Mahakama. Serikali zote hupenda kuivuta mahakama iwe karibu nao kwa usalama wao, lkn Mahakama inayojitambua hujitofautisha na Serikali kila siku.
Mhimili wa tatu ni Bunge, hawa kiburi Chao kikubwa kilo kwenye kutunga sheria. Hapa panawapo kiburi hata !mbele ya serikali na mahakama. Serikali hupewa misingi yake ya kiutendaji na mhimili huu, Mahakama hutekeleza sheria na luzitafsiri sheria zilizotungwa na Bunge. Wanapokutana ndani ya ukumbi wa bunge kwa ajili ya kutekeleza jukumu hili, mihimili yote miwili iliyobaki hukaa mguu sawa kwasababu hapo ndipo jeuri ya wote hutokea, jambo jema sana ni kwamba, wananchi wa kawaida hawana uwezo wala nguvu juu ya mahakama na serikali Bali wana nguvu sana kupitia mhimili huu wa tatu!!
Kama serikali haituelewi na Kama mahakama hazieleweki, wananchi tusibaki tunalalamika, hapana! Nguvu yetu haipo katika vyama vya siasa, wala kwa watawala, twendeni Dodoma, twendeni bungeni, twendeni kwa wabunge wetu tuliowachagua hawa watatuelewa tuu!!
Siku zote Polisi sii rafiki wa mwananchi, wala Mahakama kiuhalisia sii rafiki wa mwananchi, bunge ni rafiki yetu wananchi!
Tukijua jinsi ya kulitumia bunge nchi yetu itasonga mbele!!
Kwa maneno machache niseme nguvu ya bunge ni wananchi!!