Kibubu hakina dili kama M-Pesa ni rahisi hivi

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
663
1,165
Kama una hela yako ambayo umeiweka tu kwenye kibubu ambacho hakizalishi na una lengo la kufanya vitu baada ya mwaka au miezi kadhaa ijayo ipo njia rahisi ya kufanya ingia kwenye Simu yako piga *150*00# chagua namba 4 lipa kwa M-Pesa
Kisha chagua namba 5 Lipa Hisa za Vodacom weka namba ya kumbukumbu unayoipokea kupitia SMS baada ya kuhakiki Hisa unazohitaji na gharama zake

Ukimaliza thibitisha baada ya kukamilisha muamala wako utatumwa Maxcom Hawa ni mawakala wanaofanya kazi na DSE baada ya muamala wako kuthibitishwa utapokea SMS kuthibisha kuwa umekwisha nunua hisa za Vodacom

Utaona ni Jinsi gani 85000 uliyotaka kuiweka ndani ya kibubu itakavyozaa baada ya muda mfupi.

kwa jinsi bei inavyoongezeka ktk Hisa kuna uwezekano mkubwa mwakani muda kama huu bei ya hisa za Vodacom moja itakuwa mara mbili zaidi ya bei ya sasa, kwa kifupi ukija kuziuza hisa ulizonunua wakati huu wa Ofa basi mwakani zitakuwa mara mbili zaidi.

Niweke wazi mimi ni mwanahisa wa soko la hisa la Dar es salaam na Masoko mengine hii ni fursa kwetu lazima tuwe na uwezo wa kuvutia mitaji ya kutoka nje ya nchi na kuileta ndani ya nchi ni utamaduni mzuri wa kuweka akiba na uwekezaji mzuri hata mbuyu ulianza kama mchicha.
 
1st to reply,,,kuwekeza ni vzur ila kwa sasa wacha nipige jembe kwanza nitakuja baadae huko,,,
 
Muwaambie watu pia hisa hupanda bei na kushuka, hivyo kuna kupata faida na kula hasara.
Mfano mzuri ni sasa wakati his a zipo kwenye mauzo. He, aliyenunua mwaka jana kwa lengo la kukuza mtaji, atauza kwa being aliyoitarajia mwaka huu au kipindi hiki?
 
Mfano mzuri ni sasa wakati his a zipo kwenye mauzo. He, aliyenunua mwaka jana kwa lengo la kukuza mtaji, atauza kwa being aliyoitarajia mwaka huu au kipindi hiki?

Mwaka jana alinunua bei gani na mwaka huu atauza bei gani? Je mhusika alikuwa na utaalamu wa kukadiria bei mwaka huu itakuwa kiasi gani? Kuna malipo ya "broker" na makato ya kodi ya mapato.

Hoja yangu ni kwamba wananchi wanapohamasishwa kununua hisa waambiwe ukweli kwamba faida haina uhakika wa 100%. Hii kampeni ya hisa za voda inafanyika na inatoa picha ya uhakika wa faida (haya ni mawazo yangu).
 
Back
Top Bottom