Kibiti, Pwani: Majambazi yaua Askari Polisi NANE(8)

Kwa hiyo uko Radhi polisi wauawe kwa dhana ulizokiwa nazo na hofu inayopandikizwa na wapinzani.

Polisi wanamadhambi yao lakini tusisherehekeye kuuawa kwa mwandamu hata kama humpendi.


Mimi sijasema nafurahia, nilichosema ni hiki nakwekea tena kwa wino mwekundu


Usisahau hao hao unaosema ni ndugu zetu wamewauwa na wanaendelea kuwauwa na kuwatesa ndugu zetu. Vyombo vya ulinzi vimekosa kabisa ushirikiano na raia kwa kulazimishwa kutumikia CCM.

Polisi na vyombo vyengine vya usalama vinahitaji kuundwa upya ili vifanye kazi kwa mujibu wa taaluma zao na sio kuwatumikia wana siasa wa CCM
 

Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa, askari polisi SABA wameuawa na majambazi huko Mkuranga, Mkoani Pwani.

Habari hizo zinasema kuwa, askari hao wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakijiandaa kuondoka kwenye lindo ambalo lilikuwa ni kizuizi cha barabarani ili warudi kituoni.

Imeelezwa kwamba majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana.

=====

UPDATES:

- Silaha zote (SMG) inadaiwa zimechukuliwa!

- Shambulizi limefanywa na mtu mmoja (jambazi/gaidi?)

=====

Came as a tip:

Jamani habari za usiku. Sisi huku BUNGU eneo la JARIBU mpakani tumepotelewa na askari saba(07) wa kikosi cha FFU.

Ilikuwa hivi:
Askari walikuwa wana-liviana ambapo section moja ilikuwa inatoka na nyingine inaingia. Sasa wakati hii inayotoka baada km 03, Jambazi/Gaidi lilikuwa limejificha porini karibu HIGHWAY baada ya gari kulikaribia jambazi/gaidi hili lilimshambulia dereva kwa mbele na gari kupoteza mwelekeo na kuanguka wakati huo jamba/gaidi liliendelea kushambulia.

Jambazi/gaidi alikuwa mmoja

=======

H. Crime Kibiti NR 62 MN 90 14/04/2017
Saa 02:30hrs kwa:
Upele Pwani (R) POL. Pwani (R) POL. Kibiti. Kbt/IR/337/2016.

Ilani ya kwanza

Kosa: mauaji (x)

Mnamo tarehe 13/04/2017 saa 18:15hrs huko Mkengeni kijiji cha Uchembe kata ya Mjawa tarafa na wilaya ya Kibiti (M) Pwani. Kundi la majambazi ambalo idadi yao bado haijafahamika wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la Polisi PT.3713 Toyota L/Cruiser na kuua askari nane ambao ni

1. A/INSP Peter Kigugu

2. F.3451 CPL Francis

3. F.6990 pc Haruna

4. G.3247 pc Jackson

5. H.1872 PC Zacharia

6. H.5503 PC Siwale

7. H.7629 PC Maswi

8. H.7680 PC ayoub.

Pia walimjeruhi askari no F. 6456 PC Fredrick kwa kumpiga risasi ya mkono wa kushoto na amepelekwa hospitali ya misheni Mchukwi kwa matibabu.

Baada ya majambazi hao kufanya mauaji kwa askari walifanikiwa kuchukua silaha tisa kati ya hizo SMG sita zikiwa na risasi 30 kila moja na long range tatu.

Awali gari ya polisi ilikuwa ikitokea Jaribu mpakani kwenye road block kuelekea Bungu, baada ya kubadilishana na shift nyingine ndipo walipofika maeneo ya Mkengeni sehemu yenye mteremko na majani marefu na kuanza kushambuliwa na najambazi kwa kupigwa risasi kioo cha mbele usawa wa dereva na kusababisha dereva kupoteza uelekeo na gari kuingia kwenye mtalo wa barabara na ndipo majambazi hao kufanya mauaji kwa askari.

Baada ya tukio hilo mahojiano yalifanyika na watuhumiwa waliokuwa wakishikiliwa na polisi ambao majira ya 02:15 hrs walienda kuonyesha eneo la msitu wa Kilima cha Mianzini barabara ya Nyamisati ambalo wahalifu hao hujificha.

Walipofika maeneo hayo walishambuliwa na majambazi hayo na kuwajeruhi wenzao waliokuwa mbele kwenda kuonyesha na baadaye walifariki dunia na ndipo majibizano ya risasi yakaendelea baina yao na polisi.

Katika majibizano ya risasi majambazi walifanikiwa kukimbia na kutelekeza silaha nne kati yao mbili za polisi aina ya polisi zenye no. Smg tzpl 10549 risasi 30, smg tzpl 26881630 risasi 30 na silaha mbili za majambazi smg moja na sar moja.

Eneo la tukio limekaguliwa na DCP Kashai, DCP Sabasi, SACP Mayala, ACP Ngoyayi, SSP Canute Msacky OCD - Kibiti na ASP Juma Kanena OC - CID Kibiti.

Miili ya marehemu imepelekwa hospitali ya taifa Muhimbili.

FCR/Maendeleo zinafuata.

Mwisho///////// toka: Crime (W) Kibiti

=======

IKULU, Rais Magufuli alaani mauaji ya Askari polisi 8 huko Kibiti mkoani Pwani. Ampa pole IGP na Askari wote kwa kuwapoteza wenzao.

Habari zaidi soma=>Rais Dkt. John Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa IGP na familia za Askari wote waliouawa

Walioua askari 8 wilayani Kibiti nao wauawa

FRIDAY , 14TH APR , 2017
Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwana jana usiku.

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo, Nsato Marijani

Akizungumza na wanahabari leo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao.

Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.

Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.

Amewataja askari waliuawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.

Kufuatia tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na waharifu wote katika maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.

Mpaka sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda kweny oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji… mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu tofati” amesema Marijani

Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00 jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni
Kamishna anasema Tanzania Hakuna ugaidi sasa wale masheikh kutoka Zanzibar ni Nani? Kama Tanzania Hakuna ugaidi naomba muwaachie wale masheikh mara moja.
 
Ni kweli police wetu hawana urafiki na raia wema,wao wanajiona ndio Mungu wa dunia
Unatoa hukumu kwa polisi wote kutokana na kitendo cha polisi mmoja aliye kukwaza!!!Mungu anakuona kama wewe ni muhalifu unayo haki ya kuwachukia kwakuwa Polisi wanachukia uhalifu na wahalifu haitafikia siku ambapo huitaji wa polisi utakoma uwapende usiwapende wapo
 
Je, unajua uonevu ulioambatana na Operation Uhai? Wewe unatizama tembo tu. Hujali kabisa kwamba watu wengi wasiokuwa na hatia walionewa, walipigwa, walibambikiwa kesi etc. Je, ni kweli "majangiri wote walitiwa mbaroni"? Je, ni kweli kwamba "tembo ni wengi sana"? Kama operesheni za kijeshi ndio suluhisho la ujangili wa tembo, mbona ujangili haukomi?

PS. Kuna mtu hapa ananidokeza kuwa wanajeshi ndio majangili wakubwa.
Ile operation ilisaidia sana ktk kudhibiti ule uhalifu na kama kuna wengine walikumbwa na ile operation ni kuwaida kutoka ktk operation zozote zile,Nakumbuka wauza samaki especially dagaa waliambiwa hawa wanakua wakubwa kwanini wewe unavua bado wadogo?

Walishikwa wengine wauza nyama pori nyati kwenye vibali vya kuwinda pia

Lakini all in all hayo hayakuwa na madhara sana kama madhara ya majingiri kwa Tembo.

Nakumbuka mpaka gari ya mkuu wa wilaya ilikamatwa usiku na meno ya Tembo inasafirisha na dreva wake alifungwa gerezani.Mkuu wa wilaya hakuhusika na huyo biashara ila dreva alinunuliwa na majingiri ili gari ivushe tu ktk kizuia cha maliasili wakiamini gari ya mkuu wa wilaya haisachiwi but huyo siku ilisachiwa.

Wale matajiri wengi wa meno ya Tembo hakuna walijuta kujihusisha ni ile biashara kwa jinsi ambayo walivyofanyiwa uchunguzi mpaka kuwapata sasa issue ilikuwa kuwabana zaidi ili watoe taarifa zaidi ndipo walipolijua Jeshi ni nini??

Operations za kijeshi nazipenda zinasaidia sana kustore peace mahali na kuwarudisha watu Pamoja.
 
Ila siwapendi mapolisi sijui kwanini! mzee Wangu nae aliniambia nisije penda polisi kisa walimpiga na kitako cha bunduki kisa wamemfananisha na waliyekua wanamtafuta kitu kinachomsymbua adi sasa.

Mimi pia nineshamwambia mwanangu asiwapende polisi
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Binafsi nawapapole wafiwa wotena mungu awapumzishemahari pema peponi wale waliopoteza rohozao huku wakiwa ktk kutekeleza majukumuyao.IMA kuhusu walitaka nn hao majambazi ,nazani walichokitaka ndicho walicho kichukua,nina maana roho za ndugu zetu na siraha ambazo watazitumia ktk matukio mengine zaidi,sote tumuombe Mungu atuepushe na mabalaa.
 
Unatoa hukumu kwa polisi wote kutokana na kitendo cha polisi mmoja aliye kukwaza!!!Mungu anakuona kama wewe ni muhalifu unayo haki ya kuwachukia kwakuwa Polisi wanachukia uhalifu na wahalifu haitafikia siku ambapo huitaji wa polisi utakoma uwapende usiwapende wapo


Ndugu yangu , mimi binafsi mwaka 1973 nilipata ajali ya gari , na bahati nzuri kama nusu kilomita kutoka kwenye ajali kulikuwa na kituo cha polisi. Wasamaria wema walinichukuwa na kunipeleka kituo cha Polisi.

kwa bahati Mkuu wa kituo alikuwepo chini , wakati huo , Aliponiona tu alinibeba na damu zangu na kuniweka kwenye gari yake haraka na kunipeleka hospitali.

kule hospitali hakuniwacha mpaka alihakikisha nimepatiwa matibabu na baada ya matibabu alinipeleka nyumbani kwetu.

polisi kama hawa wako wapi leo ???

Leo hii kuna ndugu zetu wamechukuliwa na polisi na kuteswa na wengine mpaka leo hawajarudi. katika hali hii unategemea kitu gani.

siku zote mtu huchuma alichopanda . hawa polisi walioawa ni watu walioingia kwenye system kwa shida tu . hata huo mshahara hauwatoshi . lakini ndio kifo hakikimbiliki.

ndio nikasema vyombo vya ulinzi vinahitaji kuundwa upya ili vifanye kazi kwa taaluma yao. Wasitumikie wanasiasa wa CCM
 
Duh?binadam tumekuwa wanyama kweli askar analinda usalama wako Leo mmemfanya awe hawaamini tena wanaowalinda jesh LA police na usalama was taifa letu limtafute jambaz hili mpaka lipatikane ni hatari sana kwa police wetu Mimi kama RAIA nalaani sana kitendo hiki mungu azilaze roho za marehem pema peponi
 
Ni matumaini yangu kuwa viongozi wenye dhamana watakapoanza kutumia akili haitakuwa too late
 
Kamishna anasema Tanzania Hakuna ugaidi sasa wale masheikh kutoka Zanzibar ni Nani? Kama Tanzania Hakuna ugaidi naomba muwaachie wale masheikh mara moja.
Inaonekana tukio limekukonga moyo.. Full shangwe kwako..
 
J
Naww acha point za kisisiemu sisiemu hapa.. Kwani suala la serikali kuhusika kwny utekaji na mauaji ya baadhi ya wateyea haki za watanzania. Spendag ile MTU unajikuta ccm mavi mavi yaani unatetea serikali wakati imepoteza mwelekeo
Haki ya mama.... nyie ndio msiotutakia sisi Watanzania mema kisa labda unaishi utumwani kwa weupe. Ila hamtaweza Mungu bado anapenda uwepo wa Tanzania na Watanzania.
 
Back
Top Bottom