Ziko hospitali gani?Nani amekwambia kuwa maiti za hao magaidi zitapewa ndugu zao na upelelezi haujakamilika?
sasa inawezekana vipi raia wa kawaida wana silaha kama SMG, ingekuwa mapanga sawa.Wamewahisi halafu wakauwauwa?
Kwa hio wewe unaweza kutembea na SMG alafu usihisiwe kuwa ni mhalifu;Hivi tutadanganywa mpaka lini? Eti saa tatu usiku. Wahalifu halafu hapohapo wanahisiwa. Alikuwaje mhalifu? Alihalifu nini? Mlipiga risasi gizani? Hakuna wananchi jirani walishuhudia tukio? Miili iko wapi? Mbona tunaona picha mchana kweupe halafu tunawaona FFU tu na magari? Hizo silaha walizopata ziko wapi? Jamani hebu acheni kutufanya watoto basi. Hata sisi tunajua kujumlisha au kuunganisha nukta. AAARRRRRGHHHH TOO MUCH SASA
Kwa hio na wewe una SMG?ujinga usio na mfano..unaua Raia kwa kuhisi?? mi mwenyewe nikiona POLISI hua nakimbia na sijaiba wala sijakaba mtu ila SARE tu za mapolisi zinanikimbiza..ina mana na mimi ningekua kibiti saivi ningeweza kua mmoja wa WANAODHANIWA..shenzi kabisa!
Idadi ya watu katika Kikundi = 6Mmmh! "Kikundi cha watu sita wote kwa pamoja kushambulia polisi alafu wa 4 wakauwawa lakini silaha zilizo kutwa ni 2!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Acha fikra finyu. Jiongeze. Think twice n outside the box acha kuwa brainwashed. Fill the jigsaw puzzle first.Kwa hio wewe unaweza kutembea na SMG alafu usihisiwe kuwa ni mhalifu;
maana ukiwa na smg either wewe ni askari au wewe ni mhalifu, sio raia.
na vita ni muda wowote kama unataka mchana tu ndo watu waende maporini tutafeli mzee.
mchana ndo watu wameenda kufanya uchunguzi.
kazi isipofanyika unalalamika, ikifanyika unalaumu; Basi nenda wewe kibiti mchana ukarushiane risasi na wahisiwa.
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.
Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.
"Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji" Alisema Sabas.
Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.
Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
Chanzo: ITV
Unawaza puzzles tu mzee, vitu vingine ni common sense.Acha fikra finyu. Jiongeze. Think twice n outside the box acha kuwa brainwashed. Fill the jigsaw puzzle first.
Hivi ni kweli Hali ndivyo ilivyo ama naota?Kama habari hii ni kweli lipo tatizo
Kudhania tu hakumfanyi mtu kuwa na hatia na adhabu!
Ziko hospitali gani?
Kweli unaamini polisi makini kama hao wanaweza kuuwa ushahidi wa jinai kama hii?
ww unacho taka kujua hapo ni nini haswa?? au HUKUPENDA majambazi kuuwawa??Ukifikiria kwa makini hakuna anaeshabikia mauaji, sisi tunachotaka maelezo yafanane na ukweli wananchi wapate matumaini kuwa punde kutakuwa shwari, hivi majambazi na hatakama majangili wata take cover na watupe risasi pasipo kujeruhi imagine tendo lenyewe usiku, ok jeshi letu liko makini zaidi wao walipowaona walikuwa wakwanza kuteka cover na kuwapiga adui ndani ya dk 30! Fine adui walikuwa 6 na bunduki 4 ama 2 peke yake! Wawili walifanikiwa kukimbia na siraha ama watupu! Na hakuna technologia ya kujua hizo siraha 2 zimefanya tukio gani na gani?
mashaka yako nini? Polisi wa TZ wapo vizur sana, usije ukaomba kukutana na moto wao mkuuKwa jinsi navyowajua wale wauaji WA kibiti kuanzia ktk uvamizi Wao WA vituo vya polisi,ambush zao za magari ya polisi eti wameshambuliwa Bila Wao kumjeruhi hata polisi mmoja?na kwa jinsi navyowafahamu polisi kuanzia kale ka mkasa ka zombe,na siraha wanazotangaza wamezirudisha baada ya kuporwa kwao na kumbe ni uongo,Nina mashaka na Hao waliouawa kama kwel ni wahusika.