Kibiti: Polisi inapoamua ku 'balance' matukio kwa kukamata viongozi wa CUF.

Unaweza kuchekelea hili suala la kuuwawa baadhi ya watu lakini mwisho wake kicheko kitageuka kuwa kilio.

Wanasiasa wameanza kulifanya ni suala la kisiasa lakini wenye uelewa mpana wanafahamu hili sio suala la kisiasa pekee.

This is low level terrorism.
Alshabab Kenya walianza hivi hivi,boko haram Kaskazini mwa Nigeria walianza hivi hivi.
Hao waliopo Pwani ni magaidi full na wadhibitiwe haraka kabla hawajaenea zaidi.
Naona wamelelewa sana
Nina wasiwasi hata hao panya road wanaweza kuingizwa kwenye ufadhili wa mikono ya magaidi.
Ninawaza tu.....
 
mtatiro unacheza ngoma usiyoijua. hivi sasa wanakuona covinient kua na wewe lakini iko siku watakutwanga na wewe risasi. serikali ilizembea itikadi kali kuenezwa misikitini hadi mafunzo ya kivita sasa ndio tunavuna tulichopanda.
Kwahiyo ni vita ya kidini??? Na hao ITIKADI KALI wenyewe wanalenga ccm tu sio wakristo??? Hivi hizi chuki za kidini mtaacha lini??? Mkifika huko kwenye udini trust me mtakoleza moto zaidi badala ya kuuzima
 
Leo P wamekuwa kama waandish wa habar eti wana-balance story, bahat mbaya wkt wanamchukua yule mwnykt wa cuf gar yao nyeupe ilionekana live
 
Nahisi mwisho wa haya yatakuwa ni hatari
Haya mambo yashageuka ya kisiasa
Kama ni kweli nitamzarau igp.
Yaani ndio ziara yake ameenda kuwafundisha polisi wafanye hivyo?

Jamani naomba tuondoe siasa ktk hili
Nilisha sema polisi wa sasa ni weak, tangi walipo amua kuwa wana siasa, hivyo waweza ku deal wana siasa wenzao wahalifu hawawawezi........rejeeni kufungwa kwa vituo vyao kila ifikapo saa 12 jioni.
 
Acheni kuwasema waislam kwa vitu visivyowahusu.
Ukiondoa askari waliouawa, nani mwingine ambaye si muislam ameuawa rufiji toka haya mauaji yaanze? Kila upande wanaokufa ni waislam! Polisi wanaua waislam na magaidi wanaua waislam!
Sisi ndio tunaotakiwa kulia ktk Hili na sio kishutumiwa.
So far hakuna report ya who is behind this, hakuna details za motive ya hao magaidi so what mtatiro is saying ni kuwa hatuwezi kushika watu wa cuf kwa kuwa hamna grounds zozote zinazoonesha motives za kisiasa in that case wala waislam sababu hakuna motives za kidini.
Kama ingekuwa motives ni za kidini then wangeshambulia makanisa ya kibiti na mkuranga ambayo ni machache mno, why wanashambuliwa viongozi wa serikali tu?
Mkiwalazimisha waislam waingie kwenye huu mgogoro kama maeneo mengine duniani wanavyofanya, definetely they will na Hii italeta balaa. Unajua mtu akisingiziwa na kuwa victimized mara nyingi hujenga chuki na hutenda hayo huku siko tunakotaka kufika.
Please WAACHENI WAISLAM KWENYE HILI, HALITUHUSU NA HUO SIO MSIMAMO WA WAISLAM WA TANZANIA.......
Umenena vema. Kukimbilia kuhukumu bila uthibitisho kutapunguza nguvu ya kupambana na tatizo.
 
Polisi wanakamata washukiwa wa uhalifu ambao wanaweza kuwa CUF, CCM au ACT. Msiingize siasa kwenye hili jambo
Umemsikia Waziri wa Mambo ya ndani? Anasema kuwa hakuna jambazi atakayemwua mwanaCCM tu. Kwa hiyo mauaji haya ni ya kisiasa.

Nilimshangaa sana. Kama ni ya kisiasa, ni chama gani kinapambana na CCM kwa mtutu wa bunduki? Hivi waziri anajua kuwa hawa wahalifu kuna wakati hutafuta njia ya kupunguza umoja wa mnaofanyiwa uhalifu ili kuounguza nguvu? Kama mbinu ikiwa imekaa hivyo, haoni wanaanza kufanikiwa? Kauli hii ya waziri itawapa nafasi gani vyama vya upinzani katika kushirikiana na umma wote kupambana na uhalifu huu? Siku zote vita huhitaji umoja, na hasa vita vya ndani.
 
TAARIFA MPYA KUTOKA MKURANGA/RUFIJI/KIBITI.

Wenyeviti wetu wawili mitaa (CUF), Ndg. Kazi Mtoteke wa Mtaa wa Ikwiriri Kati na Ndg. Jumanne Kilumike wa Mtaa wa Ikwiriri (wilayani Rufiji) wametekwa na "watu wasiojulikana" (vyombo vya Dola) lakini hata OCD na RPC wanatangaza eti wametekwa na watu wasiojulikana.
Tofauti na wale wauaji wa Polisi wetu 8 na viongozi 30 wa CCM, Watekaji wa sasa wanakuja na magari hadi jirani na nyumba ya mtekwaji (Kiongozi wa CUF), kisha wanaingia nyumbani kwake wakiwa wamejifunika nyuso na wakishampata kiongozi waliyekuwa wanamsaka wanaondoka naye.
Hii ni oparesheni ya vyombo vya Dola na mimi on the truth I will speak it as it is maana unaishi kwenye nchi ambayo uongo na unafiki are the orders of the day. Wakishaondoka eneo la mji wa mtekwaji wanaingia kwenye gari walilokuja nalo na kuondoka.
Siku 6 zilizopita chama chetu kilianza kuripoti masuala ya Rufiji/Kibiti/Mkuranga na wapo watu walianza kutukejeli bila sababu. Sisi kila tunachozungumza ndiyo hali halisi. Kinachoendelea kwenye wilaya hizo hivi sasa siyo wale wauaji walioleta madhara makubwa, kwa sasa matukio ya utekwaji wa viongozi na uumizaji wa raia yanafanywa na vyombo vya dola, na tuna ushahidi huo. Hivi sasa idadi ya viongozi 12 wa CUF hawajulikani walipo, wanafuatwa majumbani na kutekwa "na watu wasiojulikana".
On my opinion, kazi ya kusaka wale wauaji wa Polisi wetu na viongozi 30 wa CCM imekwama au imeshindikana, na sasa vyombo vya dola vinatafuta JUSTIFICATION ili kum-please RAIS na hata kumdanganya IGP mpya. Kama wauaji HALISI wameshatoroka, hawapo, au wamekimbia hebu tuelezwe ukweli, tusifichane. Haiwezekani sasa kilichobakia ati ni kuwasaka viongozi wa CUF wa matawi, wa kata, wa wilaya, wenyeviti wa kiserikali wanaotokana na CUF kwenye vitongoji, vijiji, mitaa na madiwani wa CUF.
Kwamba ati WAUAJI wa viongozi zaidi ya 30 wa CCM wawe ni viongozi wa CUF! Ajabu kweli kwel! Kwamba yale majambazi/Janjaweed/Mungiki/Intarahamwe (call them any name), yaliyovamia na kuua polisi wetu wasio na hatia na kupora SMG (Bunduki) zote ati hayo mavamizi ni viongozi wa CUF. Na kwa hiyo eti oparesheni ya sasa ya kuyasaka MAUAJI imegeuka kuwa kamata kamata ya viongozi wa CUF. I am so sad for my country and I am speaking it loudly kuwa RPC wa Pwani na timu zake za Opareshenj wanamdanganya IGP, wanamdanganya RAIS na wanafanya haya kui-please CCM ambayo imeondokewa na zaidi ya viongozi 30 wasio na hatia.
The truth must be spoken as it is!
Julius S. Mtatiro
Mytake!
Ushabiki wa kuacha kushughulikia chanzo halisi cha tatizo na kuwasaka wauaji na kuamua kuingiza siasa kwenye mauji haya, ni lazima tujiandae kulipa gharama kubwa zaidi. Binafsi naona mpasuko mkubwa unaoletwa na viongozi kupitia tatizo la kibiti. Chondechonde.....we are planting the seeds for our own destruction! Menye masikio na asikie.
 
MWENYEKITI WA KITONGOJI WA (CUF) APIGWA RISASI NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA.

Jana usiku Katika Oparesheni ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wamempiga Risasi Mwenyekiti wa Kitongoji wa CUF pamoja na raia mwingine, huko Nyamisati, Kibiti.
Mwenyekiti huyo ni Moshi Sefu Machela na ni mwanachama. Na baada ya kumpiga risasi vyombo hivyo vya ulinzi vilimkokota na kuelekea naye kusikojulikana na hali yake haijulikani.
Kinachotokea Rufiji/Mkuranga/Kibiti hivi sasa ni Dola kwenda kulipiza kisasi kwa raia wasio na hatia ( hususani Viongozi wa CUF) ili kufuraisha na kutuliza nafsi za ndugu jamaa na marafiki wa raia waliouawa ambao wengi wao walikuwa viongozi wa CCM.
Hadi sasa viongozi zaidi ya (20) wa CUF wameshakamatwa bila sababu, wanateswa na kisha kiachiwa bila kufunguliwa mashtaka. This is very bad and shameful indeed.
Unapotaka kuwafutalia JANJAWEED wanaowaua viongozi wa CCM kwa kuwatesa viongozi wa CUF unajenga visasi huko mkoani Pwani. Sijui nani anavifundisha vyombo vyetu kuwa mbinu yao hii ya kikatili na ya kuumiza watu wasio na hatia itakuwa na tija.
I am so worried kuwa taifa letu linaelekea mahali kusiko salama.
Julius S. Mtatiro
09/06/2017
Nimeandika hapa kuwa sioni tofauti ya watekaji wa kibiti na wauaji na wale waliomteka Ben Saanane!! Ukiona vyombo vya dola vinapambana na wananchi ujue Dola limeshindwa kazi@@
 
Back
Top Bottom