Kibao 'This Is America' cha Childish Gambino chaweka historia katika tuzo ya Grammys

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
2,554
2,000
Childish Gambino ameweka historia katika tuzo ya Grammy kwa kushinda nyimbo bora, na rekodi bora ya mwaka kwa kibao chake This Is America.

Ni mara ya kwanza wimbo wa mtindo wa rap umeshinda vitengo vyote viwili - licha ya kwamba Gambino hakuhudhuria tuzo hiyo

Ni msanii wa kwanza kutohudhuria tuzo hiyo ya "big four" ya Grammys tangu Amy Winehouse mnamo 2008.

Gambino - anayejulikana pia kama Donald Glover - aliwashnda wasanii kama Drake, Lady Gaga na Bradley Cooper katika vitengo vyote.

Kendrick Lamar na SZA, Brandi Carlile, Zedd, Maren Morris na Grey ni miongoni mwa walioteuliwa kuwaia tuzo hiyo.

This Is America, iliyoambatana na video yenye ujumbe mzito, ilizusha mjadala ilipotolewa mnamo Mei mwaka jana.

Imeangazia uwakilishi wa watu weusi nchini Marekani na ubaguzi wanaokabiliwa nao.

Wakati tuzo kwa rekodi ya mwaka inatambua kila mtu aliyehusika na kibao, akiwemo msanii, maproduza na mafundi, tuzo ya kibao bora humuendea mtunzi.

Mtunzi mwenza wa This Is America Ludwig Goransson alipokea tuzo hizo kwa niaba ya Gambino.

Amesema hajui ni kwanini Gambino alikataa kuhudhuria lakini ameeleza ni muhimu kiasi gani kutambua wasanii wa mtindo wa rap na hip-hop katika tuzo hiyo ya Grammys.

This Is America pia imejishindia tuzo ya video bora ya muziki ulioshirikisha rap na nyimbo.

Rapper 21 Savage, mmojawapo ya washirikishi katika kibao hicho , hakuweza pia kuhudhuria pia sherehe hyo kwasbaabu anazuia na maafisa nchini Marekani kutokana na mashtaka ya kutumia viza iliyomalizika muda nchini.

Msanii huyo mzaliwa wa Uingereza na anayeishi Atlanta- aliteuliwa pia kwa tuzo mbili kwa uwezo wake.




_101276570_1de27.jpeg



BBC
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom