Kibanda ni nani?

Kibanda ni nani?

sulphadoxine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
2,257
Reaction score
649
Nianze kwa kuombeleza msiba wa jicho moja la Absalom kibanda .Jicho hilo lilijeruhiwa na watu wabaya usiku alipotekwa na kupigwa na watu hao .Tumejulishwa kuwa madaktari wane walijitahidi sana kuokoa jicho hilo lakini wameshindwa na kudhibitisha kuwa jicho hilo limekufa rasmi.Kiungo kimoja na chamuhimu sana cha mwili wa kibanda kimetoweka.

Hatukuhudhuri mazishi ya kiungo hicho lakini inatosha tukiamini kuwa kiungo hicho hatunacho tena.Kimetoweshwa na watu waoga .

Kwa kuwa sasa ni wazi taifa letu linaangamizwa na ombwe la utawala,ni sahihi nikisema kuwa kutekwa,kupigwa na kuumizwa vibaya kwa mwenyekiti wa jukwaa la wahariri bwana Absalom Kibanda si,jambo la bahati mbaya.Lina dalili za kupangwa kwa makini na watu wenye akili za uharibifu.

Nasema hivyo kwa sababau ,Kibanda ana vigezo vyote vitatu ambavyo vimekuwa vinausumbua sana mfumo wetu .Na sifa moja ya watu dhaifu huwa ni kuwaondoa (eliminate) watu wanaonekana wana ujasiri wa kuwakosoa.

Vigezo vitatu alivyo navyo kibanda kiasi cha kuwavutia majasusi waliomteka na kumuumiza ni kwa kuwa MWANAHABARI,MNYAKYUSA NA NI MKRISTO.

Waandishi wa habari ni moja ya makundi ambayo kwa kawaida huwindwa na utawala dhaifu popote duniani
.Tawala hizo huanza kwa kuweka sheria kandamizi na kali kudhibiti uhuru wa habari.

Hilo linaposhindikana hutafuta mbinu ya kuwanunua ili waendane na utawala dhaifu na hilo likishindikana ndio utafuta njia ya kuwaondoa mmoja baada ya mwingine au kuwapa ulemavu utakao zuia wao kuendelea na kazi zao kwa ufanisi.

Mazingira yetu yanaashiria ya kuwa tumeishapitia hatua hizo kwanza kwa kuendekeza sheria kandamizi zinazokandamiza uhuru wa habari .Katika miaka saba iliyopita trumeshuhudia kufungiwa kwa magazeti kadha wa kadha kama mwanahalisi(mara mbili),kulikoni na hata mitandao ya kijamii.

Tumeshuhudia waaandishi wa habari wakiundiwa kesi za ajabu na kupelekwa polisi na mahakamani.Tumeshuhudia waaandishi wa habari wakipigwa,kunyang'anywa vitendea kazi na kuuawa na polisi.

Tumeshuhudia mara kadhaawaandishi wakishambuliwa na kuingiliwqa kaitka ofisi zao wakiwa kazini.Katika matukio haya yote ,hakuna mtu aliyekamata ,kushitakiwa na hataimaye kutiwa hatiani.Badala yake tumeona machozi ya mamba yakitiririka katika mashavu ya watawala kuomboleza majanga hayo yanayowapata wana habari.

Tumeshuhudia misururu ya magari wakienda hospitali kuwaona majeruhi na kutoa ahadi za kusaidia matibabu na zile za kuhakikisha wanakamata waliohusika.

Wenye hekima wanaamini kuwa serikali yenye mkono mrefu haiwezi kushindwa kukamata muhalifu ikishindwa kuna jambo .Imani hii imejengeka mioyoni mwa watanzania na haiwezi kufutika kwa ahadi hewa..

Kibanda ni mnyakyusa anayetokea Mbeya .Katika hali hii inayoshangaza watu wengi ,Mbeya ni mkoa ambako wanatoka watu wengi waliokumbwa na masaibu ya kutekwa ,kupewa sumu,na kuuawa katika mazingira tata.

Hata kama baadhi ya matukio hayana uthibitisho lakini watu wengi wamefanywa kuamini tuhuma chanzo cha masaibu yaliyowapata watu watokao Mbeya na kutishia maslai ya watawala.

Tumepata kusikia habari za mbunge wa kyela na waziri wa sasa wa uchukuzi DK.Harrison Mwakyembe ambaye inadaiwa alipewa sumu inayoendelea kuitafuna ngozi yake.Baada ya dana dana za polisi na kigugumizi cha kusema wazi chanzo cha ugonjwa wa DR.Mwakyembe ,serikali iliona ni vema apozwe kwa kupewa cheo kinachomnyima uhuru wa kuvunja kiapo cha uwajibikaji wa pamoja .



Kwasababu anazozijua,amethamini cheo kuliko uhai wake .Laiti angefuta tuhuma alizozimwaga hadharani kabla ajapewa vyeo hivi!.Tumewahi kusikia tetesi zinazo tatanisha kuhusu kuugua kwa Prof.Mark Mwandosya ,Mbunge Rungwe na waziri asiye na Wizara maalumu.

Msomaji Raia

Toleo la 285
13 Mar 2013










285_kibanda.jpg




NIANZE kwa kuomboleza msiba wa jicho moja la Absalom Kibanda. Jicho hilo lilijeruhiwa na watu wabaya usiku alipotekwa na kupigwa na watu hao.
Tumejulishwa kuwa madaktari wanne walijitahidi sana kuokoa jicho hilo lakini wameshindwa na kuthibitisha kuwa jicho hilo limekufa rasmi. Kiungo kimoja na cha muhimu sana cha mwili wa Kibanda kimetoweka.
Hatukuhudhuria mazishi ya kiungo hicho lakini inatosha tukiamini kuwa kiungo hicho hatunacho tena. Kimetoweshwa. Kimetoweshwa na watu waoga. Mola alaze mahali pema peponi, jicho la ndugu yetu Absalom Kibanda. Amina.
Kwa kuwa sasa ni wazi taifa letu linaangamizwa na ombwe la utawala, ni sahihi nikisema kuwa kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bwana Absalom Kibanda, si jambo la bahati mbaya. Lina dalili za kupangwa kwa makini na watu wenye akili za uharibifu.
Nasema hivyo kwa sababu, Absalom Kibanda ana vigezo vyote vitatu ambavyo vimekuwa vinausumbua sana mfumo wetu. Na sifa moja ya watu dhaifu huwa ni "kuwaondoa" (eliminate) watu wanaoonekana wana ujasiri wa kuwakosoa. Vigezo vitatu alivyo navyo Kibanda kiasi cha kuwavutia majasusi waliomteka na kumuumiza ni kwa kuwa ni mwanahabari, Mnyakyusa na ni mkristo.
Waandishi wa habari ni moja ya makundi ambayo kwa kawaida huwindwa na tawala dhaifu popote duniani. Tawala hizo huanza kwa kuweka sheria kandamizi na kali kudhibiti uhuru wa habari. Hilo Iinaposhindikana hutafuta mbinu ya kuwanunua waendane na utawala dhaifu. Hilo likishindikana ndipo huanza kuwaondoa mmoja baada ya mwingine au kuwapa ulemavu utakaozuia wao kuendelea na kazi zao kwa ufanisi.
Mazingira yetu yanaashiria ya kuwa tumeishapitia hatua hizo kwanza kwa kuendekeza sheria kandamizi zinazokandamiza uhuru wa habari. Katika miaka saba iliyopita tumeshuhudia kufungiwa kwa magazeti kadha wa kadha kama Mwanahalisi (mara mbili), Kulikoni na hata mitandao ya kijamii.
Tumeshuhudia waandishi wa habari wakiundiwa kesi za ajabu na kupelekwa polisi na mahakamani. Tumeshuhudia waandishi wa habari wakipigwa, kunyang'anywa vitendea kazi na kuuawa na polisi.
Tumeshuhudia mara kadhaa waandishi wakishambuliwa na kuingiliwa katika ofisi zao wakiwa kazini. Katika matukio hayo yote, hakuna mtu aliyekamatwa, kushitakiwa na hatimaye kutiwa hatiani. Badala yake tumeona machozi ya mamba yakitiririka katika mashavu ya watawala kuomboleza majanga hayo yanayowapata wana habari.
Tumeshuhudia misusuru ya magari wakienda hospitalini kuwaona majeruhi na kutoa ahadi za kusaidia matibabu na zile za kuhakikisha wanakamata waliohusika. Wenye hekima wanaamini kuwa serikali yenye mkono mrefu haiwezi kushindwa kukamata mhalifu, ikishindwa, kuna jambo. Imani hii imejengeka mioyoni mwa Watanzania na haiwezi kufutika kwa ahadi hewa.
285_kibanda2.jpg
Kibanda ni Mnyakyusa anayetoka Mbeya. Katika hali inayoshangaza watu wengi, Mbeya ni Mkoa ambako wanatoka watu wengi waliokumbwa na masaibu ya kutekwa, kupewa sumu, na kuuawa katika mazingira tata. Hata kama baadhi ya matukio hayana uthibitisho, lakini watu wengi wamefanywa kuamini tuhuma chanzo cha masaibu yaliyowapata watu watokao Mbeya na kutishia maslahi ya watawala.
Tumepata kusikia habari za Mbunge wa Kyela na Waziri wa sasa wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe ambaye inadaiwa alipewa sumu inayoendelea kuitafuna ngozi yake. Baada ya dana dana za polisi na kigugumizi cha kusema wazi chanzo cha ugonjwa wa Dk. Mwakyembe, serikali iliona ni vema apozwe kwa kupewa cheo kinachomnyima uhuru wa kuvunja kiapo cha uwajibikaji wa pamoja. Kwa sababu anazozijua, amethamini cheo kuliko uhai wake. Laiti angefuta tuhuma alizozimwaga hadharani kabla hajapewa vyeo hivi!
Tumewahi kusikia tetesi zinazotatanisha kuhusu kuugua kwa Profesa Mark Mwandosya, Mbunge wa Rungwe na Waziri asiye na Wizara Maalumu. Inashangaza kwa nini atafutwe kuangamizwa na watu hawa kama tetesi hizo zina ukweli wowote. Lakini kimsingi, tawala dhaifu na dhalimu huwaogopa sana watu wenye uwezo kiakili. Profesa Mwandosya anatoka Mbeya pia na ni yeye, serikali na Mungu wetu wanaojua nini chanzo cha ugonjwa wake.
Tulishuhudia kutekwa, kuteswa na hatimaye kutupwa porini kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka. Yeye pia anatoka Mbeya sawasawa tu na Kibanda pamoja na wengine niliowataja. Mpaka sasa amekaa kimya lakini kuna mawili yanayohitaji ufafanuzi kutoka serikalini.
Kwanza, kwa nini ililifungia gazeti la Mwanahalisi wakati lilikuwa linaisaidia serikali kujua ni kina nani waliohusika kumteka Dk. Ulimboka. Katika hali ya kawaida tungedhani baada ya watawala kusema serikali haihusiki na utekaji huo, basi serikali ingefanya kazi na Mwanahalisi katika kuwatafuta waliohusika maana Mwanahalisi lilionekana kujua ni kina nani.
Pili, kwa nini serikali haitoi taarifa juu ya uchunguzi ilioufanya kuhusiana na sakata hilo? Kukosekana kwa maelezo ya masuala haya mawili, kunauachia umma njia moja tu ya kulielewa suala hili- nayo ni kuwa, mtekaji anajulikana, mtekaji analindwa, na alitumwa kwa sababhu ambazo umma hauwezi kuzijua.
Ndipo likaja la David Mwangosi kuuawa mikononi mwa polisi. Suala hili liko mahakamani lakini itoshe kusema tu ya kuwa Mwangosi pia anatoka Mbeya na alikuwa ni mwandishi wa habari.
Sifa nyingine ya tawala dhaifu huwa ni kuua watu kwa mashinikizo ya imani za kishirikina na ndiyo maana baada ya utawala wa Idd Amin kuanguka, vilikutwa vichwa vya watu katika majokofu ya Ikulu na hata kutunza baadhi ya vifaa vya marehemu kwa sababu zisizojulikana.
Aidha, ilibainika kuwa utawala huo ulikuwa na kiu ya pekee ya kuua watu wa eneo fulani kwa sababu ambazo hazikuwa zikitajwa hadharani na wauaji hao. Baadhi ya wahanga wa tawala dhalimu na dhaifu huwa wanakatwa baadhi ya viungo vyao na wao kushiriki katika mazishi ya viungo vyao wao wenyewe! Nachelea kusema kuwa tunaelekea huko kwa sababu kiu ya viungo vya miili ya wana habari ni kubwa mno kwa sasa.
Absalom Kibanda ni Mkristo sawa tu na wengine niliowataja hapo juu. Siku za karibuni tumeshuhudia makanisa yakichomwa moto (takribani 54 mpaka sasa nchini kote). Tumeshuhudia wakristo wakifunguliwa kesi na polisi kwa kosa la kuchinja vitoweo vyao (takribani kesi 16 nchini kote).
Tumeshuhudia wachungaji na makasisi watatu wakiuawa (Mto wa Mbu, Geita na Zanzibar). Tumeshuhudia makasisi na maaskofu wakishambuliwa kwa risasi na silaha nyinginezo (Zanzibar, DSM na Mwanza). Tumeshuhudia serikali kupitia mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wakitoa amri za kidini kana kwamba wamegeuka makadhi. Tumeshuhudia mzaha wa kuyaambia makundi yanayohasimiana kidini kuwa yakae yamalize tofauti zao.
Tumeshuhudia vipeperushi na kanda za kuhamasisha mauaji ya viongozi wa dini huku serikali ikiwaambia viongozi wa dini wajilinde. Tawala dhaifu na dhalimu huwahofia sana viongozi wa dini na dini yao. Kwa hiyo yaweza kuwa hatari zaidi kuwa mwandishi wa habari na hapo hapo ukawa katika dini inayohofiwa.
Kwa kuwa haya yaliyotajwa hapo juu hayajapatiwa majibu, yametoa mwanya kuruhusu bongo mbalimbali kufikiria zinavyotaka. Mathalani, wapo waliosikika wakisema kuwa Kibanda amepata adhabu kwa sababu ama yeye, au mmoja wa waandishi wake, aliandika taarifa inayotuhumu dini fulani kuwa imeweka kambi ya kigaidi huko Ukerewe-Mwanza.
Kwamba, hata baada ya kuambiwa aombe radhi alikataa. Kwa nini basi kama hilo lilitokea, watu wasiamini kuwa kundi lililomtaka aombe radhi linahusika na utekaji wake?
Watu wengi wasomi kwa watu wa kawaida wanaanza kuona kwamba taifa letu limekumbwa na udini. Kwa hiyo ni sahihi pia kufikiri kuwa, hata kama haipendezi, kuwa suala la dini ya Kibanda lisipuuzwe. Hii hoja ni nyepesi kama dola yetu ilivyo nyepesi na inavyopenda majibu mepesi kwa maswali magumu.
Nimalize kwa kumtakia uponyaji wa haraka Absalom Kibanda. Jicho lake lililoharibiwa limesababisha hata vipofu wapate kuona kinachoendelea katika taifa letu. Damu yake iliyomwagika bila hatia itaharakisha harakati za kulipatia taifa letu dola iliyo imara na thabiti ya kulinda uhai wa watu wake.
Jicho la mwandishi ni jicho la jamii. Kumtia upofu mwandishi ni kuitia jamii upofu. Ni watawala vipofu tu wanaotamani kufanya kazi na waandishi vipofu.







[h=2][/h]

CHANZO CHA HABARI HII NI GAZETI LA RAIA MWEMA LA LEO 13/03/2013 UKURASA WA 4 NA MSOMAJI RAIA.
 
Nilisoma na Absalum Kibanda Musoma alliance yeye akiwa form four mimi form one, alikuwa mchezaji mzuri wa soka (Namba 4 kama sijakosea) na alikuwa mchezaji mzuri wa volleyball pia. Ila ninachokumbuka vile vile alikuwa ni muumini mzuri wa dini ya Kiislam. Nakumbuka alikuwa kiranja wa shule pia. Sasa ukristo wake unaongelewa hapo sijui aliingia lini.
 
Hapo kwenye nyekundu mi sielewi mantiki nini kama angekuwa upande wa pili wa kiimani isinge kuwa?au upande wa pili kama ni muandishi alafu ni tofauti na hizo red tatu za kibanda na anafanya yale yale kama ya kibanda katika uandishi nae ingekuwa tofauti.
 
Hapo kwenye nyekundu mi sielewi mantiki nini kama angekuwa upande wa pili wa kiimani isinge kuwa?au upande wa pili kama ni muandishi alafu ni tofauti na hizo red tatu za kibanda na anafanya yale yale kama ya kibanda katika uandishi nae ingekuwa tofauti.

Nakushauri tafuta gazeti la Raia Mwema usome habari kamili,
pengine unaweza ukawa na hoja nzuri zaidi...
 
Naona sasa watu washaanza kuchanganya mambo hapa.......Kuna hoja ya msingi unayoweza kuijenga kwa Kibanda kuwa mtu anayetokea Mbeya?! Watu wa Mbeya wanawindwa na nani?!
 
Mimi nafikiri suala si unyakyusa wake au ukristo wake (Kibanda nijuavyo si mkristo) nimeshasema awali kuwa nilisoma naye na alikuwa muislam safi . Labda hoja ingejikita kwa kazi yake ya Habari.
 
Mkuu ulianza vizuri ila baadae umeharibu
 
Mods ondoa uzi huu wa ukabila na udini. Asituletee chuki za ukabila na udini katika nchi yetu
 
Ukristu na umbeya wa kibanda hapa umekujaje? Ina mana waliomdhuru kibanda ni waislamu? Haya kuna taarifa kuwa kibanda mi muislamu na tena ni muislamu mshika dini hilo unalizungumziaje? Na je umefanya utafiti wa kina juu ya haya kabla hujaandika? Hapa tuliangalie hili suala kwa mawanda mapana zaidi kuliko kuleta propaganda za udini na ukabila kwani itakuwa ni ushindi kwa waliotekeleza udhalimu huu.
 
VID-20121228-00005 - YouTube

VIDEO; MIKAKATI YA MATESO YA KIBANDA NA MWANDISHI MWANDAMIZI WA GAZETI LA MWANANCHI; MHUSIKA MKUU HUYU HAPA. KWA MUDA SASA HAPA TANZANIA KUMEKUWEPO NA MATUKI... (SIJUI NDO NJAMA TU AMA EMBU CHEKI TU BT MIE SIAMINI)
 
Najua anapoishi, najua anapofanyia kazi, sio rafiki yangu lakini mara kadhaa tumekaa nae kwa bia na nyama choma.
Namuonea huruma na kumsikitia kwa maswahibu yaliyompata
 
Nakubariana nawe. Two wrongs do not make a right. Si vizuri kupandikiza chuki miongoni mwa jamii za watanzania. Huu ndio uchochezi by any definition. Unyakyusa na Ukristo wa Kibanda hapa havina nafasi kabisa na ndio maana mwandishi wa makala haya alijikuta anashindwa kuitetea hoja yake mara baada ya kuitaja katika aya ya tano. Ilibidi apotee ndani ya hoja mpaka alipoibuka tena kwenye aya mbili za mwisho. In fact, amejadili matukio ya waandishi kufanyiwa unyama kwani hoja na Unyakyusa na Ukristo umekosa mashiko hata ndani ya makala yenyewe. This is not fair.

Ukristu na umbeya wa kibanda hapa umekujaje? Ina mana waliomdhuru kibanda ni waislamu? Haya kuna taarifa kuwa kibanda mi muislamu na tena ni muislamu mshika dini hilo unalizungumziaje? Na je umefanya utafiti wa kina juu ya haya kabla hujaandika? Hapa tuliangalie hili suala kwa mawanda mapana zaidi kuliko kuleta propaganda za udini na ukabila kwani itakuwa ni ushindi kwa waliotekeleza udhalimu huu.
 
Nakushauri tafuta gazeti la Raia Mwema usome habari kamili,
pengine unaweza ukawa na hoja nzuri zaidi...

Nimelipata nasasa nafikili nitakuwa na hoja nzuri kama ulivyosema hii ndo HOME OF GREAT THINKERS.
 
Nimesoma makala husika mwanzo hadi mwisho. Anawataja ulimboka, mwangosi,mwakyembe,mwandosya na mwisho kibanda. Anahusisha matukio hayo na unyakyusa wao na ukristo wao. Kuhusu ukristo anaunganisha na mauaji ya wachungaji kule mto wa mbu,geita na kujeruhiwa na kuuawa kwa mapadre kule zanzibar. Nashindwa kumuelewa mwandishi, nitakuwa wa mwisho kumuelewa
 
Mleta hoja ni kama hana anchokijua.Sasa kama watu wanamfahamu Kibanda kama muislamu yeye kaupata wapi ukristo japo udini hapa hauna mantiki wala unyakyusa.Kuna taarifa pia inamtaja Kibanda kama MNDALI na si mnyakyusa.
 

Labda nitanabaishe kwanza kabla sijazungumza kuwa kitendo cha kushambuliwa mwaandishi wa habari ni cha kupigiwa kelele na mpenda maendeleo yeyote. Tunaomba serikali ifanye jitihada ya kila hali kuwakamata wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Tukirudi kwenye hii habari nadhani mhariri mkuu ana maswali ya kujibu na serikali ina wajibu wa kuchukua hatua dhidi ya gazeti hili kama itaona kuna makosa.

Labda nianze na Mnyakyusa mwandishi amechukua mifano ya akina Dr Mwakyembe na Professor Mwandosya. Halafu akaiconnect hiyo mifano na kilichotokea kwa ndugu yetu Kibanda. Hii ni conspiracy kwasababu a. Hadi leo hatujui kimetokea nini kwa Mwakyembe na mwenyewe in fact ametuonya tusiyazungumze sasa wewe kama mwandishi umejuaje wahusika ndio hao hao wapo kwa Kibanda? b. halafu utaipa uzito gani habari ya tetesi wakati za ukweli zipo? Medical report zao si zipo kazichukue ujue kiini cha ugonjwa ni nini badala ya kuleta conspiracy theory.

Twende kwenye Ukristo, kwanza mwandishi namtahadharisha umenukuu makasisi walioshambuliwa Zanzibar ukamuacha imam aliyeuwawa kule zanzibar je hili nalo lina uhusiano na ukristo? Vile vile nakushauri kasome gazeti moja linaloitwa Fahamu uelewa kinachoendelea kuhusiana na Padri Mushi ambacho FBI wamekigundua kabla hawajaondoka nchini. Nakushauri kabla hujaconclude kudai aliuwawa kwasababu ya ukristo wake kalisome kwanza gazeti la Fahamu Machi 12-18 ufahamishwe kinachoendelea.

Wasia wangu kwa serikali:
Kuhusu hii habari nawaomba waifanyie uchunguzi ikibidi hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika. Habari kama hii ni sawa na uhaini na uchochezi kwani mwandishi amenukuu matukio akiyafananisha na Kibanda. Hii ni hatari kwani hili gazeti lilijichotea sifa ya kusomwa na wengi nikiwamo mie. Sasa sio sote wenye kufahamu wakasoma wakaelewa kilichonena na kupima taarifa yake. Mwandishi ameandika tu pasina kufanya uchunguzi wa makini wa taarifa alizozinukuu. Hii ni hatari.

Ni ushauri tu nilikuwapo!!!
 
Udini, ukabila, havina maana cha msingi ni kuwatafuta hao wanaotumwa na mkubwa wao wateke watu na kuwapiga. Lakin bado eti mnasema hii ni nchi ya amani, iko wap hiyo aman?
 
Back
Top Bottom