KIBALI CHA KUWINDA WANYAMA PORI

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,519
Kuna utaratibu iliyowekwa na Wizara ya Maliasili kuwa ifikapo tangu tarehe 1 Julai mpaka tarehe 31 Desemba kila mwaka Wizara inatoa kibali kwa atakayeomba kwa kulipia na aina ya mnyama anayetakiwa kuwindwa. Lakini kwa siku za karibuni wananchi wanayoishi kando kando ya mbuga zetu hasa Serengeti wamekuwa wakikamatwa na Maaskari wa wanyama Pori wakiwa na nyara za Serikali kama nyama, ngozi, pembe nk. Inawezekana ule utaratibu wa kuwinda kwa vibali haupo tena ndiyo maana hawa wananchi wanakamatwa mara kwa mara na nyara za Serikali. Chukulia Wilaya ya Serengeti wananchi wanaishi kando kando ya mbuga na wanyama wanazaliana kwanini wasipewe vibali na Serikali ili kuwinda kwa ajili ya kitoweo kwa muda utakaowekwa. Kama suala la vibali halipo tena linatakiwe litazamwe upya ili kusaidia wananchi wapate kuwinda kwa vibali.
 
Back
Top Bottom