Heshima kwako Ab-Titchaz,
Siasa za kenya ngumu kuzielewa hivi huyu Ruto kama sijakosea alikuwa kambi ya Raila lakini siku za karibuni amekuwa akitofautiana na Raila wajuzi wa siasa za kenya naomba kujuzwa kulikoni.
Rais kibaki kuwakumbatia kina Ruto kunaashiria mikakati ya uchaguzi mkuu unaokuja hasa tukitilia maanani siasa za Kenya zimejaa ukabila.
Ngongo,
Heshima natangulzia mkuu na asante kwa swali.
Huyu Ruto alikua kambi moja na Raila lakini sababu zake zilikua za kibinafsi.
Ukifuatilia siasa za Kenya wakati wa Moi utakuta kwamba huyu bwana alikua
mwanafunzi chuo kikuu cha Nairobi na Moi alimtumia kupata kura ya vijana
wakati huo. Aliunda grupu la watu kwa jina YK92 ambao walitumika kuhonga
watu vijijini na hela ambayo ilikua inachapishwa na serikali ya Moi. Baada ya hizo
kura, inflation rate ya hela ya Kenya ilipanda sana. Aliyekua anapiga naye ubavu
mmoja alikua anajulikana kama Bw Jirongo. The group was so notorious mpaka
shilingi mia tano ya Kenya ilikua inaitwa 'Jirongo'. Eventually walifanikisha lengo
lao la kumrudisha Moi mamlakani and the rest is history.
Ilipofikia hizi kura za juzi huyu bwana aliungana na Raila akijua kua Raila atashinda
urais na by extension atamtetea kuhifadhi mali ya wizi alokua amejilimbikiza
wakati wa Moi. Hata hivyo kama tujuavyo Kibaki aliiba kura na ndoto ya bwana
Ruto haikukamilika. Kwa hivyo katika mahesabu yake ameona kwamba ni bora
arudi kambi ya Kibaki ambaye yuko mamlkani na kwa kiwango f'lani atamtetea
katika kuhifadhi mali aliojilimbikizia.
Jambo lengine ambalo limemfanya kumpiga Raila vita ni kwamba katika viongozi
wote waliopo Kenya kwa sasa ni Raila pekee ambaye yuko 'safi' na anajua
hatomuunga mkono katika maswala kadhaa ambayo anataka kufanya. Cha mno
pia kujua ni kwamba baada ya zile kura za '07, kulikua na fujo katika maeneo ya
bonde la ufa na inasemekana wakikuyu wengi waliouliwa na kupoteza mashamba
walisadiki kua mkono wa Ruto ulikuwemo. Kwa sasa kuna kesi ambayo ipo kule
Hague (ICC) na proskyuta mkuu Bw Ocampo atakapo tia timu Kenya mwakani,
Bw. Ruto na Bw. Uhuru Kenyatta watakumbwa na mashtaka. Kwa hivyo anaamini kua
Kibaki will not hand them over for prosecution but Raila will do it without fear or
favor.Kwa hivyo kutetea maisha yake ameamini it is safe to join Kibaki's Camp.
Kuhusu uchaguzi wa Kenya wa 2012, Mheshimwa Raila yuko mbele ya hawa
wagombeaji wote lakini ukweli ni kwamba wataziiba tena ilimradi kutetea mali
ya wizi walionayo hawa watu. Siasa za Kenya baada ya kura za '07 naweza
kusema wazi zimepita ukabila bali kwa sasa watu wanapigana dhidi ya familia
tatu:
Ya Kenyatta, ya Moi na ya Kibaki. Wakikuyu washachoka kutumiwa na hii
familia ya Kenyatta na wameamua they are going in a different direction from now
henceforth. Porojo za magazeti ndizo zinazotudanganya kua wakikuyu watampigia
mkikuyu mwenzao. Kem fikiria Kibaki alikua Rais na bado waliuliwa watu kibao na
kunyanganywa mashamba. Bado mpaka hii leo wamo katika kambi za wakimbizi
kila sehemu na hakuna mtetezi japo Rais ni mtu wao. Kimeeleweka kua familia ya
Kenyatta ina mashamba kibao kama mkoa mzima and it is very easy to settle hawa
marefujii wa kabila lao...swali linakuja mbona hawapati msaada??? Jibu: Ubinafsi
wa hizi familia umekua ukiwaziba macho siku nyingi na kwa sasa wameamua
tofauti.
Nadhani nimetosheleza swali lako kwa hili jibu.
Shukran.