Kibaha Vijijini kunani?

Feberia

JF-Expert Member
Aug 5, 2013
528
250
Wanajamvi habari

Napenda kuwasilisha kero kubwa kwa watumishi wa halmashuri ya Kibaha Vijijini ambapo watumishi walio wengi wanafanya kazi kwa kujituma na pindi juhudi zinapoonekana wengi wa wakuu wa vitengo ambao wanahofu ya kuondolewa na watendaji wanaojituma basi hutengeneza maneno au majungu ya kuwahamisha vituo kwa kuwakomoa.

Idara zinazoongoza ni afya na Elimu. Hapo kuna kujuana kwa wakuu wengi na ambao wametengeneza mtandao wakukaa muda mrefu hata kama taarifa zipo TAKUKURU watu hawa wamewanunua na kufanya wanavyotaka na hata muda mwingine kutuma namba za simu kwa wahusika mfano usalama wa taifa na kuwapigia simu watumishi na kuwaambia mtahamishwa mpelekwe mbali na mji kama ni adhabu.

Kwa wale ambao wanaogopa uhamisho wanatoa HONGO ambazo huwafanya wasihamishwe kwa kuwataka watoe kuanzia kiasi cha Tsh 200,000/= na zaidi.

Uhamisho umetolewa kwa watumishi kwa kusema ikama lakini wengi wamebaki katika vituo vyao kwa kutoa fedha na wengine wakuu wao wa vituo wanatangaza au kusema muuache kuongea ukiona mbwa kapanda juu ya mti anamwenyewe. Wapo ambao ni wakuu wetu wa ofisi wanamiaka zaidi ya 7 na wengine 15 ambao wameogeuza ofisi kama mali zao kwa kupokea rushwa
 

rongai

JF-Expert Member
Jan 27, 2014
462
500
hapa kazi tuu mkulu anasema uzalendo kwanza haya ngoja waje. hivyo vituo ni vya. kazi. ama
 

rongai

JF-Expert Member
Jan 27, 2014
462
500
hiyo halmashauri kwanza mkuu wa wilaya. mmoja ila halmaahauri 2 kibaha mji na. vijijini. navwakurugenzi 2 duuuuu nchi ina mambo hiii na halmashauri ya kibaha vijijini. ofisi.zipo. kibaha mjini kwenye halmashauri ingine kwann wasihamie. karibu na wananchi wao kama huko mlandizi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom