Kiasili kila mtu ni mwizi, umewahi kuiba kitu gani baada ya kupitiwa na shetani?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,579
44,821
Uwizi ni kitendo ambacho inatokea unakifanya muda wowote na kuiba haichagui umri wala jinsia.Hata nyinyi greater thinkers hakuna ambaye hajawahi kudokoa. Maofisini huko tunaibiana kalamu, flash n.k na wengine ndo kabisa wanaiibia serikali kwa michongo.

Kwenye bar huko tunakokunywa kunywa tunaviziana sometimes barmaids wanatupiga ila na wenyewe wakijichanganya unashangaa anakurudishia chenji isiyo yako unapiga kimya.

Ebu kiri hapa jukwaani umewahi kuiba kitu gani baada ya kupitiwa na shetani pengine ulikuwa na shida ndio maana ulidokoa.
 
Kuiba zaka na sadaka, inapaswa tumrudishie alietoa lakini kwa matendo yangu nikala zaka badala ya kumrudishia aliyenijaalia hivyo nimemwibia Mungu lakini najitahidi kuacaha hali hiyo na naendelea vyema

Waamini tusisahau kutoa zaka na sadaka🙏🏿, Bwana ameahidi tumjaribu kwa njia hiyo tuone kama hatatufungulia madirisha ya mbinguni na kutumwagia baraka isiwepo nafasi ya kutosha
 
Back
Top Bottom