Wadau naombeni mnifahamishe, nataka kupulizia dawa ya sulphur katika mikorosho yangu.
Ni wastani wa kiasi gani cha sulphur kinatumika kwa mkorosho mmoja? kilo?nusu? robo? nk
Asante sana mkuu. mikorosho ina kama uzao wa 5 sasa. imeshambuliwa na ukungu mweusi. ni nje kidogo ya DarHIYO MIKOROSHO INA UMRI GANI MKUU?? IMEANZA KUZAA??
SULPHUR NI POWDER.. KIPIMO NI WASTANI WA GRAM 30 KWA MAJI LITA 15 KUTEGEMEA NA STEJI YA UKUAJI WA MMEA NA PIA KUTEGEMEA NA KAMA TAYARI KUNA UGONJWA (FUNGUS) AU LA, KAMA TAYARI UNAUGONJWA ONGEZA KIPIMO MPAKA GRAM 50 KWA MAJI LITA 15. KWA PANDE ZA HUKO MTWARA/LINDI AMBAKO MIKOROSHO IPO NI VYEMA UKATUMIA RED SURPHUR..
GRAM 30 NI SAWA NA VIJIKO VIKUBWA VYA KULIA WALI VITATU (3),
PIA GRAM 30 NI SAWA NA GANDA MOJA LA KIBERITI (LILE GANDA ZINAPOKAA NJITI ZA KIBERITI, UKITOA NJITI ZILE UKIJAZA SULPHUR HAPO-UJAZO UKAWA FLAT HIZO NI GRAM 30)
KILA LAKHERI
Asante sana mkuu. mikorosho ina kama uzao wa 5 sasa. imeshambuliwa na ukungu mweusi. ni nje kidogo ya Dar
Hivi mabwana shamba siku hizi hakuna?