Binti Maringo
JF-Expert Member
- Jul 4, 2007
- 2,804
- 98
Sasa Kelly01 akianza kutoa majina ya hao watu wengineo ni member humu huoni kama atakuwa anavunja sheria za JF au unalengo baya wewe elewa tu wapo wengi wanaishi maisha ya kikimbizi wkt home full shwangwe tu.
Mi narudi kule kule ninakobana kila siku, kila mtu kivyake vyake.Ulimwengu huu wa utandawazi, wa information overload, wa paradigm shifts, wa boundless opportunities, wa a world citizenry, mtu anakuwa na muda wa kuchunguza watu wanaishije? Ujue huyo maisha yake mwenyewe yamemshinda.
Moja ya sababu mimi naamua kukaa ughaibuni ni simply bongo sijaweza kuona kazi nitakayofanya as comfortably as what I am doing now, for the money I am getting now, nikaweza kujikidhi mwenyewe na familia yangu the way I am doing now. Kwa hiyo hiyo habari ya kubeba mabox siielewi on a personal level, na ninaposikia watu nyumbani wana generalize hivyo napata kushangaa kwa nini mtu afanye hivi -other than the obvious reasons za wivu wa watu waliopigwa chini visa kama alivyosema member mmoja hapo juu-
Lakini hata kama ningekuwa nabeba maboksi, that would have been the life I chose.Tumeumbwa tofauti na kila mtu ana priorities tofauti, kwa nini kujifanya nanny wa watu wazima wanaojua wanachofanya? Wanakuhusu nini wewe kama si kimbelembele tu?
Hizi tabia za kujuana sana zinaonyesha tu watu walivyokuwa fixated na maisha ya wenzao.Mwacheni kila mtu aamue aishi maisha yake, hata kama mtu anataka kuunga tela kwenda Andromeda Galaxy and the planets of Betelgeuse kutafuta makazi mapya huko poa tu, wewe inakuhusu nini? I mean hata kama ni mtu wa familia yako bado ana decision yake mwenyewe. Mbona mnataka wivu wenu uwafanye muwe kama watoto wadogo ambao hawajafika age of reason?
I salute you on this....sometimes unakuwa una make sense sana!....ila kuna wakati mwingine unakuwa unaniudhi......week hii yote naona unatema point tuu!....Abra kadabra!...
Tatizo lako nikikuudhi husemi, wewe unapenda kukubaliana sana, which may not be healthy.
Moja ya sababu mimi naamua kukaa ughaibuni ni simply bongo sijaweza kuona kazi nitakayofanya as comfortably as what I am doing now, for the money I am getting now, nikaweza kujikidhi mwenyewe na familia yangu the way I am doing now.
Kwa hiyo hiyo habari ya kubeba mabox siielewi on a personal level, na ninaposikia watu nyumbani wana generalize hivyo napata kushangaa kwa nini mtu afanye hivi -other than the obvious reasons za wivu wa watu waliopigwa chini visa kama alivyosema member mmoja hapo juu-
Mhhhhh!!!!Hili bifu kati ya mla vumbi na mbeba box.🙄🙄
Wewe uko kwenye kundi gani?
Sipo kwenye kundi lolote hapo, nipo kula nondozzzzzzzz tu.Zitakapoisha ndipo nitakapojua nichague kula vumbi au box.
dah, naona jamaa wa dhw wamevamia humu kwa kasi!
sina uhakika...mara ya mwisho kuingia ilikuwa too slow....the site may be dead by now!hivi hiyo tovuti bado ipo?
Nyie mnaowaambia watu warudi wawe kama Kevin mnajua history ya Kevin, income bracket ya familia yake, family connections zake na mengine kama hayo?
Hata kama Kevin hana degree, anayo pedigree, sasa waswahili wana msemo "ukitaka kumuiga Tembo kunya utapasuka msamba". Kuna wengine hatuna pedigree bongo tupo huku tumejibanza, na hata kama tungekuwa nayo hatuhusudu michongo ya migongo ya pedigree. Si kweli kwamba mtu yeyote mwenye jitihada anaweza kufanya hizi kazi, bongo kuna unwritten rules, ndiyo maana BOT walijazana kama ng'ombe mnadani.
Kwa hiyo tupe mfano wa mtoto wa Uswazi aliyefanza vitu, hapo kidogo utawagusa watu, ingawa mimi nasimama pale pale kwamba kila mtu kivyake vyake.
Lakini hawa watoto wa Upanga / Oysterbay friji open wameenda kwenye parties za Mkapa wakati Mkapa Waziri wa Utamaduni early 1980s huwezi kujilinganisha nao kabisa. Wengine majina yetu hayajulikani Rotary Club hapo sasa hatuwezi kujilinganisha na wenye networks za nchi.
Si mnaona wenyewe, huku Kevin Twisa sijui, huku nani Makamba sijui, hata wewe uje na videgree vyako vya Ivy League unaweza kuwa frustrated tu. Ndio maana kwa usawa huu tunajikita tu, Ma-Wall St, Ma-Silicon Valley, Ma-dirty basements, ma nursing homes, Ma-Batani, ma-Buruda, usawa wa Twiga mnyonge minazini hatutaki kuusikia mpaka kieleweke vizuri, humrudishi mtu.Na hivi rais ndiyo huyo officially taahira ndiyo kabisaaaaa.
Kama vile visoda vilivyokuwa vinasema, nakwambia "Jaribu Tena".