Chrisludos
Senior Member
- Oct 12, 2012
- 135
- 41
Nianze kukiri kuwa Raisi Pombe ameanza vizuri katika uongozi wake wa serikali ya awamu ya 5, naamini akidendelea hivi serikali atakayoiunda itafanya kazi kweli kweli katika kusimamia taasisi zilizo chini ya serikali na kutatua shida mbali mbali za wananchi.
Hakutakuwa na kufanya kazi kwa mazoea, na imani yangu maendeleo yataonekana.
Angalizo ni kuwa hata raisi mstaafu wa awamu ya nne ndugu Jakaya, pia alianza kwa moto huuhuu....isije kuwa nguvu ya soda tu kama watu wanavyosema huku mitaani.
Ila kama asiporudi nyuma hata baada ya kuteua baraza la mawaziri, basi mambo yatakuwa shwari kwa upande mmoja ambao ni kuifanya serikali yake iwajibike hasa kwa wananchi wake, kwani hata tabia za watumishi katika ngazi zote zitabadilika na ufanisi wao ktk kuhudumia wananchi utaonekana.
Kete mbili ambazo atabakiwa nazo ni;
1.Ukuzaji wa pato la taifa na uchumi.
Kama Raisi anatakiwa awe na serikali yenye nguvu kifedha ili aweze kuhudumia wananchi wake ipasavyo.
Inambidi aendelee kuvitumia vyanzo vya mapato vilivyopo mpaka ktk uwezo wake wa juu kabisa na pia abuni vyanzo vipya vya mapato.
Katika kuvitumia vyanzo vilivyopo itambidi pia kupitia mikataba mingi mibovu ambayo tuliingia ktk awamu zilizopita hapa anaweza kugusa maslahi ya watu na mataifa mengi makubwa, itambidi awe jasiri sana.
Lakini pia ili aweze kubuni vyanzo vipya vya mapato, Mh Pombe anatakiwa kuwa na maono na pia awe na washauri wataalam anaowaamini bila kusahau kujifunza kutoka katika mataifa yaliyo na yanayoendelea.
Kwa kuanza, uteuzi wake wa waziri mkuu na waziri wa fedha utato dira ya anapoelekea.
2. Kete ya pili na muhimu pia ni kukibadilisha chama chake cha CCM, hii inaweza kuwa kazi ngumu zaidi.
Inategemewa 2017, atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa CCM...
Baba wa taifa aliwahi sema "chama legelege kitazaa serikali legelege" ni kweli kwakuwa ukiondoa bunge, chama tawala kina nguvu kubwa ya kuisimamia serikali katika kutekeleza ilani yake, lakini si kwa CCM ya sasa ya wapigaji madili.
Pia bila kusahau katika kuchagua wasaidizi wake katika serikali, asilimia kubwa atawatoa hukohuko katika chama chake. Nafasi ya kupata wasaidizi wabovu katika CCM ya sasa ni kubwa sana.
Punde baada ya kupewa uenyekiti, itambidi ateue viongozi imara sana kumsaidia kiuongozi katika chama.
Hayo akiyafanya vema, naamini tutapiga hatua kwa haraka zaidi.
Mungu ibariki Tanzania.